Basi la abiria la Kampuni ya  Muro Investment, lenye nambari za usajiri T 820 BEY lillilokuwa likitokea Jijini Mwanza kwenda jijini Dar es Salaam, limewaka moto na kuteketea  kabisa maeneo ya Maseyu Mkoani Morogoro. Ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 1:15 usiku jana, haikusababisha madhara kwa abiria isipokuwa mali zao zote ziliteketea kwa moto huo. Basi hili ni la pili kwa kuteketea kwa moto ndani ya wiki hii baada ya Basi la Sumry kuteketea kwa moto  Mkoani Dodoma.Picha na Father Kidevu Blog.
 Mmoja wa wahusika wa basi hilo alidai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni hitilafu ya umeme iliyotokea katika gari hilo. Inadaiwa kuwa gari hilo lilipata hitilafu katika taa na walipofika mjini Morogoro walifanyia marekebisho na kuendelea na safari na walipofika maeneo hayo ya Maseyu likashika moto.
 Magari yakipita pembeni ya basi hilo lililokuwa likiteketea kwa moto na hapakuwa na askari wala magari ya zima moto yaliyoweza kuwahi kufika na kuzima moto huo ulioliteketeza basi hilo kabisa.
Wakazi wa Maseyu na wasafiri wakiangalia basi hilo likiteketea kwa moto.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 10, 2012

    Hili basi lilikuwa na matatizo tangu ijumaa ya tarehe 4..Mi nilikuwa msafir na basi la Lucky Star kutoka Mwanza Ticket No 3181(ni kampuni moja na Princess Muro)na lenyewe likutokea Mwz..kufika Misungwi boc anapiga simu "Tufaulishwe'from lucky star to princess muro kisa tilikuwa wachache ilhal tumelipa elf 45..(princess Muro nauli ni 35,000)..Tukakataa.so wakaenda na basi lao likiwa na matatizo ,kioo kina crack,nk..na mashahidi ni madereva wa Lucky star ambao walikuwa wanaongea live kwamba hilo basi lina matatizo..Ushauri wangu wa bure kwa wamiliki wa mabasi,kama hamuwezi kuyafanyia service magar yenu ni bora muache biashara kuliko kuweka roho zetu rehani kwa maslah yenu na ubahili wenu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 10, 2012

    Mdau wa kwanza hata mimi nilikuwa najiuliza hivi haya mabasi huwa yanafanyiwa service au kuchekiwa kisawasawa?

    Jamani musihatarishe maisha yetu kwa sababu ya faida za muda mfupi. Kila kazi ina ethics zake na wamiliki munatakiwa kufuata hayo.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 10, 2012

    Jamani sio Hilo tu sisi tumesafiri na basi la sumry tarehe 9/5/2012 kwa ticket namba 31941kutokea mwanza kwenda dar kwa kweli tulifika kwa neema ya MUngu Kwani tokea tunaondoka nyegezi lilikuwa limechomoka propela huko chini tumeharibikiwa mara mbili misigiri na manyoni na kutufanya tulale kwenye basi na kufika kesho yake. Hivi kweli tunapishana na mtu aliyetoka Kampala? Wamiliki wa vyombo vya usafiri kuweni makini mnahatarisha maisha ya watanzania kwa tamaa zeni. Mimi sipandi tena mabasi haya ya sumry kuelekea kanda ya ziwa

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 10, 2012

    Eeeh Mungu tunakuomba umsaidie mmiliki wa mabasi ya Scandinavi arudi uwanjani na kutupatia huduma saaaafi ya usafiri. Mara nyingi najiuliza huyu mmiliki lipi lilimfika hakuna basi linaweza fikia huduma zake. Mwaka jana nilibahatika kufika uingereza nikagundua huyo mmiliki wa scandinavia alishapita mitaa hii akaona style ya kuendesha mabasi, huduma za makonda nk. Jamani makonda wa scand walikuwa wasafi na wana lugha nzuri sana lakini hawa wengine hata waige vp hawawezi makonda wanatukana ovyo hawana ustaarabu ni wachafu nk. Nakumbuka scand tuliwahi fika mahali dereva akaona jiwe kubwa barabarani ambalo labda lingeweza kuleta ajali kwa hao wengine wasiojali njiani alisimama akamwambia konda akalitoe so sweet. EWE MMILIKI WA SCAND POPOTE ULIPO UJUE TUNAMISS SANA HUDUMA YAKO HATA UKISEMA NAULI NI KUBWA TUTAJITAHIDI TUPANDE TUKIJUA TUTAFIKA SALAMA KULIKO KUPANDA VYA BEI NAFUU HALAFU ROHO MKONONI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...