JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

TAARIFA KWA UMMA
BODI YA USHAURI YA WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA (TFS) YATEULIWA
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Khamisi S. Kagasheki (Mb) kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa Sheria ya Wakala wa Serikali (Executive Agencies Act) Sura 245 amewateua wajumbe saba (7) kuunda Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (Tanzania Forest Service - TFS). Aidha, Waziri Kagasheki amemteua Bibi. Ester Mkwizu kuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo.
Wajumbe wa Bodi hiyo ya Wakala wa Huduma za Misitu ni kama ifuatavyo:-
1. Bibi. Esther Mkwizu – Mwenyekiti, kutoka Sekta Binafsi (Tanzania Private Sector Foundation), Dar es Salaam;
2. Bibi. Gladness Mkamba - wa Wizara ya Maliasili na Utalii;
3. Eng. Bonaventura T. Baya – wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC);
4. Bw. Sosthenes Sambua - wa Dar es Salaam;
5. Prof. Yonika Ngaga - wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine, Morogoro;
6. Prof. Himid Majamba - wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam - Sheria; na
7. Bw. Rawson Yonazi – wa Dar es Salaam.
Uteuzi wa Bodi hiyo ni kwa kipindi cha miaka mitatu (3) tangu tarehe 1 Desemba 2011 hadi 30 Novemba 2014.
George Matiko
MSEMAJI
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
17 Mei 2012
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...