
Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL),Ephraim Mafuru akikabidhi cheti cha Ushiriki wa Semina ya Siku moja ya Mafunzo Maadili ya Biashara kwa Mmiliki wa Mtandao Jamii wa 8020fashions,Shamimu Mwasha katika hafla fupi ya kukabidhi vyeti hivyo jioni ya leo jijini Dar.katikati ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL,Teddy Mapunda.

Mwanalibeneke Josephat Lukaza akipokea cheti chake kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL),Ephraim Mafuru. pili kulia ni Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Mawasiliano (SBL) na kulia ni David Shayo wa (SBL)

Mroki Mroki kutoka blogu ya Father Kidevu kushoto akipokea cheti chake.

Mwendeshaji wa Libeneke la Mtaa kwa Mtaa,Ankal Othman Michuzi nae alishiriki semina hiyo na kulamba nondozz yake.

Mkurugenzi wa kampuni ya R&R Caroline Gul kushoto akipokea cheti chake.

Ankal Ahmad Michuzi akipokea cheti chake kutoka kwa Ephraim Mafuru Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) mara baada ya kumalizika kwa semina ya Mablogger kuhusu usimamizi na maadili ya upashaji wa habari na masoko katika uendeshaji wa blogu na mitandao mingine, iliyofanyika leo kwenye makao makuu ya kampuni hiyo iliyoko Oysterbay jijini Dar es salaam, katikati ni mkurugenzi wa mawasiliano wa kampuni hiyo Teddy Mapunda.

Mwanalibeneke wa Fullshangwe blog,John Bukuku akipokea cheti chake kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL),Ephraim Mafuru mara baada ya kumalizika kwa semina ya Mablogger kuhusu usimamizi na maadili ya upashaji wa habari na masoko katika uendeleshaji wa blogu na mitandao mingine, iliyofanyika leo kwenye makao makuu ya kampuni hiyo yaliyoko Oysterbay jijini Dar es salaam, katikati ni mkurugenzi wa mawasiliano wa kampuni hiyo Teddy Mapunda.

Mkurugenzi wa mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti Teddy Mapunda akifafanua jambo katika semina ya uendeshaji wa mitandao na maadili ya upashaji wa habari za masoko katika blogu na mitandao mingine.

Mablogger mbalimbali wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri katika semina ya uendeshaji wa mitandao na maadili ya upashaji wa habari za masoko katika blogu na mitandao mingine.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...