Habari iliyoifikia Globu ya Jamii muda mfupi uliopita,inaeleza kuwa Mbunge wa Jimbo la Rombo kwa Tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeo (CHADEMA),Joseph Selasini (pichani) amepata ajali ya gari jioni hii katika maeneo ya Bomang'ombe wakati akitokea Arusha kuelekea Moshi.
Imefahamika kuwa Mbunge huyo amejeruhiwa huku Mama yake aliekuwemo kwenye gari hiyo akiwa amepoteza maisha.
Chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika mpaka sasa,tunaendelea kufuatilia na tutapeana taarifa zaidi hapa hapa.


oooooh.....
ReplyDeletePoleni sana. Mungu awajalie wapone haraka.
ReplyDeleteBara bara zinatumaliza sasa watanzania.
Poleni sana wanafamilia.
ReplyDeleteMungu awapumzishe waliotutangulia na awape afya na nguvu waliosalimika..
Mhe Selasini poleni sana kwa lililowafika. Mama yetu apumzike katika raha ya milele. Amen. Ichube
ReplyDeleteNa nyie magwanda hamtulii kutwa mko huku huku eh! Sasa mtasema ni magamba ndiyo wahusika?
ReplyDeleteni huzuni sana haswa ikizingatiwa walikuwa wanatoka kumzika ndugu yake mbunge ambaye ni Padre. familia imepotezana watu wawili kwa mpigo, Mola awape subira
ReplyDeletepoleni sana ndugu zetu Mungu awatangulie katika muda huu Elibariki Gideon.
ReplyDelete