TAARIFA ILIYOIFIKIA GLOBU YA JAMII HIVI PUNDE TOKA VISIWANNI ZANZIBAR,INAELEZA KUWA KUNDI KUBWA LA WATU WANAOLIUNGANISHA KUNDI LIFAHAMIKALO KWA JINA LA UAMSHO,AMBALO LIMEKUWA LIKIUPIGA VITA MUUNGANO WA TANZANIA NA ZANZIBAR,LIMEVAMIA KITUO KIKUU CHA POLISI CHA MADEMA KISIWANI HUMO USIKU HUU  NA KUSABABISHA VURUGU KUBWA,WAKITAKA KUACHILIWA KWA KIONGOZI WAO ALIEKAMATWA JIONI YA LEO KWA KUONGOZA MHADHARA BILA YA KUWA NA KIBALI CHA SERIKALI.

HALI HIYO IMESABABISHA VURUGU KUBWA KITUONI HAPO HUKU ASKARI POLISI WA KITUO HICHO WAKILAZIMIKA KUTUMIA MABOMU YA MACHOZI ILI KUWATAWANYA WATU HAO AMBAO WENGI WAO WAKO NA SILAHA ZA JADI AMBAZO NI MARUNGU,MAPANGA NA MAWE ILI KUPAMBANA NA ASKARI POLISI KITUONI HAPO.

GLOBU YA JAMII INAENDELEA KUFUATILIA TAARIFA HIZI KUPITIA RIPOTA WAKE ALIOPO VISIWANI HUMO,HIVYO TUVUTE SIBIRA KWA SASA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 41 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 26, 2012

    mungu awajaliye kila salaam na kheri na baraka tele wazanzibari wote na inshallah inchi yetu tutaipata inshallah kwa mungu hakuna kubwa tumeshachoka kudanganywa na kuzulumiwa kama watoto yatina no no no more

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 26, 2012

    Asiyetaka muungano atafute nchi nyingine akaishi.Hao ni wahuni,wachukuliwe hatua kali

    David V

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 27, 2012

    Inaskitisha kuona SMZ inayavumilia makundi ya namna hii.

    Ni kweli kuna uhuru wa kujieleza na kutoa maoni lkn. sio kama UWAMSHO wanavyofanya.

    Serikali iwe makini, Al-shabab na Boko-kharam walianza hivi hivi, sasa hali imekuwa mbali mbaya!

    ReplyDelete
  4. Acheni upumbavu nyie ... dhulma yote hiyo inayofanyika bado munaona tuna deserve ... we deserve better. Uamsho niwaislam kama nyie wanao taka haki za wazanzibari kwa jumla ... na waislam karibia wote wakiwemo unguja , pemba , mtwara na baadhi ya mikoa wanawa support kwa kutetea haki za zanzibar

    wanaotaka muungano a.k.a muumizano.. nawatafute nchi nyengine.

    stonec!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 27, 2012

    Watanganyika mambo ya Zanzibar hayawahusu wacheni kuongea longo longo kama hamutaki kuwa support Wa Zanzibari kupata uhuru basi bora mukae kimya hayawahusu,

    PAMBANA NA MAFISADI UPATE HAKI YAKO NA UTAIFA WAKO WA KITANGANYIKA

    ReplyDelete
    Replies
    1. AnonymousMay 27, 2012

      Ahsate sana,jibu ulowapa nzuri sio matusi ni ukweli umewambia juu ya haki ya znz
      Asotaka kufahamu basi abaki na choki zake binafsi juu ya uhuru wa weziwe.mbona wao hawaunngani wakawa kabila moja wote.
      Munatuletea mawazo ya kijandawazimu tukubali kufuta urai wetu na mutupatie kabila mutujulishe tutakuwa kabila gani tujuwe la kuchaguwa.

      Delete
  6. AnonymousMay 27, 2012

    Vunja huo Muungano, kama hawataki kwanini tuwang`ang`anize? tuvunje muungano, potelea mbali, DWLLWGAF? certainly no.
    Mtanganyika

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 27, 2012

    Mtoto akililia wembe mpatie..wazanzibara naona sasa waacheni hao wazanzibari watoke zao, lakini hawatoishia hapo huo ubanguzi wao, na pale watakapoa anza kujitafuna kikamilifu hakuna kuwapokea wale watakaokimbilia kutafuta hifadhi kwa wazanzibara.

    Sioni kwanini wanakumbatiwa kiasi hicho..

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 27, 2012

    Mtoto akililia wembe mpatie..wazanzibara naona sasa waacheni hao wazanzibari watoke zao, lakini hawatoishia hapo huo ubanguzi wao, na pale watakapoa anza kujitafuna kikamilifu hakuna kuwapokea wale watakaokimbilia kutafuta hifadhi kwa wazanzibara.

    Sioni kwanini wanakumbatiwa kiasi hicho..

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 27, 2012

    Muungano umeshavunjwa na marekebisho ya katiba ya znz.lakini Mh Kikwete hataki kuweka sahihi,analeta ujanja wa katiba mpya

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 27, 2012

    Sisi na watanganyika nani wabaguzi zaidi ? Zanzibar wameweza kuunda serikali ya pamoja.bila hata mataifa ya nje kuwapo.
    Jaribuni kama mutaweza hilo lakuwa na serikali ya pamoja.kama hamuto chinjana kila siku munapigana visu kwa ardhi.

    ReplyDelete
  11. Wadau mtatusamehe kwani quality imepunguzwa saaaaaana ili tuweze ku i upload online. Kuhusu habari kwamba movie yetu ni ya kichawi kama za Nigeria mbona hili sio swala jipya kwa filamu za Tanzania? Halafu filamu yetu sio ya kichawi bali inaeleea habari za kale na sio habari ndani ya magorofa na majumba ya starehe (modernity)

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 27, 2012

    Mleta habari anasema waandamanaji wamechukuwa silaha za kienyeji.Hili litawapa Polisi kutumiya nguvu za ziada.Ukweli waandamanaji walikuwa na nidhamu ya hali ya juu na kama kawaida polisi wanawapiga mabomu ya machozi.

    Wazanzibari wanahaki kupewa fursa ya kupiga kura , kuamuwa kama wanautaka Muungano au la .Rais kikwete kafanya kosa kubwa kuwazuwiya watu wasiujadili Muungano.Vipi utazungumziya katiba mpya bila kuuzungumza Muungano.Hata watu wa Tanzania bara wanayohaki kuchaguwa kama wanautaka au laa.
    Mwalimu Nyerere, katamka kwamba ikiwa Wanzanzibari wataamuwa kuukataa Muungano hatowapiga mabomu, Raisi Kikwete asiwe na kigugumizi juu ya suala hili.Wazanzibari wametoka woga kusema juu ya Muungano, wakati ndio huu watanzania tubadilike.

    Mtanzania Ughaibuni

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 27, 2012

    wazanzibari wananini? hata wakataka waachiwe nchi hizo karafuu za kuchuma mojamoja zitalisha wangapi? kazi hawawezi wamebaki majungu tu wanadanganywa na nchi za kiarabu mnafikiri mkijitenga watawasaidia? hapo mlipo mnabaguana hali hii ni wapemba na wa unguja je mkiwakaribisha warabu si ndio kwanza mta malizana. mungu awasaidie awafungue macho na akili mpate kuwaelimisha watoto wenu sio kukaa hapo mnarogana tu.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 27, 2012

    huu ni muungano wa tanzania na zanzibar, au wa tanganyika na zanzibar?
    Nyie watanganyika acheni ujinga huo, hebu tuachieni tupumue tena

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 27, 2012

    wamesahau kama kuna unguja na pemba,Nje ya muungano hakuna Zanzibar.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 27, 2012

    hawa wahuni wanatumia mwanvuli wa dini,hawa jui hata muungano maana yake nini? Mipaka ya unguja na pemba ni wapi na ipi? wasome kwanza History au warudi kwa wagerman watapewa siri hiyo Nzito.

    ReplyDelete
  17. Hivi wanzazibar wanadhani wao wananini zaidi kuwazidi bara? wadhani bara inawaibia hivi ni nini cha kuiba zenji? hawana ardhi, wamekataakusoma kazi kupiga umbea tu, karafuu na magofu vitawapleka wapi znz? acheni ujinga muungano ni manufaa ya zenji coz bara hamna hata kitu kimoja mnachoongeza. Ngoja muachiwe afu muone.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 27, 2012

    Wala msiumizane Zanzibar yenu mtaipata. Hata sisi hatuwahitaji. Tulifikiri umoja ni nguvu lakini kama mnataka kusimama peke yenu ruksa. Ni haki yenu.

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 27, 2012

    Mie naona wa wapewe nchi yao, wawatoe wachaga wote wanaowapelekwa vitimoto, pombe na mikwaya yao hio, kila kitu kuombea taifa kumbe wanataka kueneza ukristo zanzibar kama walivyoharibu Tanganyika, msikubali wafukuzilieni bali.
    Kisha na huku wapewe Tanganyka yao ya kaskazini.

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 27, 2012

    "Vunja huo muungano, kwanini tuwang'ang'anize" Mwenzetu vipi, unaziona lkn. gharama wanazolipa kenya kwa kuwa jirani na Somalia?

    Tuonee huruma mkuu... tuna matataizo mengi, kupambana na ugaidi hatutaweza! US na EU, maji ya shingo!

    Tupo karibu sana kijografia na pia ni vigumu kumtofautisha mtu kama wa mafia, lindi mtwara tanga na hata tabora na hawa jamaa.

    Ngoma ikidata hii UWAMSHO watatawala Z'bar na hawa hawana tofauti na alshababu au alkaida.

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 27, 2012

    hivi mkishavunja huo muungano,wale ndugu zenu wa kariakoo dar s salaam wataenda wapi na maduka yao?mana huwezi kufanya biashara kwenye nchi ya wengine hadi ufate taratibu za uhamiaji,wataweza.au mnajifanya jicho pembe mnaona nusu mengine hamuyaoni?
    kweli mtoto akililia wembe mpe,nina rafiki yangu huku UK kaniambia kanunua majumba kigamboni,kwani dar es salaam kwao?ana haki gani ya kununua nyumba kwenye nchi za watu wkt ww ni migrant.kazi kwenu wazanzibar

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 27, 2012

    Waacheni Wazanzibari na Zanzibar yao. Hapa sio kulilia wembe ila ni uhuru uliomezwa nusu karne.

    Uhuru wa Zanzibar utapatikana lazima mkitaka msitake, mkipenda msipende na hata kama mkikejeli kwaa vijembe vichafu na uchochezi.

    Muungano ulianza kuvunjwa na Serikali ya Tanganyika kwa kuifanya katiba ndio sheria mama ya muungano na ndipo walipoengeza mambo kutoka 11 mpaka kinehe.

    Zanzibar Moja, watu wake ni wamoja

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 27, 2012

    Mchangiaji no. 2, Dacid V, kwani wewe uliambiwa kuungana ni 'lazima'?! Acha kufikiri kwa kutumia pua wewe. Tumia kichwa/ubongo!

    Na mara hii hamtoweza kutugawa tena kama alivyotugawa 'baba yenu wa taifa' na sera zake za 'kusadikika'. Hapa tunataka zanzibar yetu tu, na nyinyi kaeni na tanganyika yenu.

    'You can fool some people sometimes, but you can't fool all the people all the time'>

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 27, 2012

    Ama kweli ukitaka kumuua mbwa,mpe jina baya kwanza! Yaani wazanzibari wanadai haki yao, basi kuna washenzi wengine wameanza kuhusisha 'movement' hiyo na udini. Wanasahau kwamba wanaotaka mvurugano(muungano) uvunjike ni wazanzibari,ambao coincidently imetokea kuwa wengi wao ni waislamu. Hebu jaribuni kutofutisha baina ya tui na maziwa, nyie 'vizigo'!

    Halafu wasiokuwa waislamu ndo wamezoea kutupachika majina mabaya sisi (wazanzibari)ili tusite kupigania haki zetu. Lakini this time mtachina. Mpaka kieleweke. Choka kutawaliwa na Tanganyika.

    Na inaonekana pia, kuna wachangiaji hawajui historia ya Zanzibar vizuri. Kwa taarifa yenu kabla ya mvurugano (muungano) huu, Zanzibar ilikuwa na uchumi mzuri na ilikuwa imeendelea zaidi ya Tanganyika. Saivi mmeshatutawala, tumekuwa masikini wa kutupwa.

    Na wewe mchangiaji unaeleta siasa za nyerere hapa, ujue zimeshapitwa na wakati! Mpaka kiti chetu cha UN mmekiiba nyie!

    Tuwacheni tupumuweeeeee....!!

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 27, 2012

    Basi kama ndiyo hivyo, dhambi hii na iwatafune tu wanaojitenga. Ee, wapate uhuru wa kutawanyika na kuvurugana kama watakavyo. Kama huvumilii watatu, sioni vipi utamvumilia hata mmoja. Jijue wewe ni mkorofi, na mkorofi lake ni upweke.

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 27, 2012

    And we claim to be ' Nchi ya Amani na Utulivu'! Watanzania wabara na visiwani ' UNAFiKi na UZANDZIKI' utatumaliza!

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 27, 2012

    Wanzibari acheni akili potofu mnashawishiwa na wasokuwa na akili timamu na ni ubaguzi leo muungano ukivunjwa mtakulana nyama wenyewe kwa wenyewe mtaanza kubaguana kama somali na wale ndugu zenu wa kariakoo na ilala mnafikiri watarudi kusikiliza ujinga kwa wasio na elimu kamili kufanya kazi hamfanyi kukaa vibarazani hata hao mamwinyi walikuwa wanajituma acheni akili potofu tafuteni cha kufanya nci sio yenu wajinga nyinyi mlikuta kalakabho na ubwezo wenu poleni

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 27, 2012

    MWALIMU ALISEMA KWELI; kuna Waunguja na wapemba, Wazanzibari na Wazanzibara .
    Unayetetea kujitenga upo ktk kundi gani kati ya hayo manne ???

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 27, 2012

    Ata sisi watanganyika wa kweli tunataka muungano uvunjike

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 27, 2012

    Wazanzibari! Who has the right to Zanzibar??? So those with Omani descendants and Iranian blood along with Yemeni blood have the rights or ???? I think we are heading to some ethnic cleansing if we are not careful! First the common enemy is Bara or watanganyika, break off the union. Next in line is Pemba vs Unguja, kicked off wapemba from Zanzibar. Later original Zanzibaris and those with mix blood. Smells like another revolution. Frankly being a Tanganyika I can't give a hoot about this small island and I am surprise why they think the majority of Watanganyika really care about them. All those radical movements under the umbrella of Uhamsho will raise their true head soon. Sharia law etc will come in place and I can foresee immigration issue heading towards Bara. Who are we kidding here, let them have their union less headache for us! They depend more on Tourism and Karafuu, well with radical groups like that soon tourism will disappear. The sad part is that there a people in the background with relatives in the Middle East thinking that the island will be turn into Arab paradise. Think again. Good luck wanzibari and I guess it time we start looking at those denying the rights of Watanganyika in Tanganyika soon. Or maybe we are much smart than that!

    Mtanganyika who does not know where is Zanzibar and who is Zanzibari!!

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 27, 2012

    Hi!Natafuta mke awe anatoka Pemba ama Unguja mwenye umbile la kuvutia na rangi ya kimanga.Awe tayari kuish Shinyanga, Asiwe na siasa za CUF na CCM ambazo ni zakinafiki, ila awe na msimamo wa MUAMSHO kimaadili . mshahara wangu kwa mwaka ni tsh 45,025,000/=.

    ReplyDelete
  32. AnonymousMay 27, 2012

    Mchangiaji wa mwisho hapo wewe unaona kuwa na kiti UN ni dili unajua maana ya UN na the real purpose ya UN au unaona kwa nje tu. Kile ni chombo cha nchi Tajiri kutetea interest za corporations zao. wewe Ukiwa na kiti UN utafaidi nini?. Umeona Syria japo ni member?

    ReplyDelete
  33. AnonymousMay 27, 2012

    Waacheni wajitenge tuanze ku-export umeme na vyakula, Tanesco ipate hela ya kununua mitambo zaidi tumalize tatizo la umeme.

    ReplyDelete
  34. AnonymousMay 27, 2012

    kukosa elimu jambo baya sana ,poleni sana uvivu wenu wakazi na kuwakumbatia waarabu wa muscat ,na tende zao zitawapeleka wapi ,bora mjitenge muuanze kuchinjana vizuri

    ReplyDelete
  35. AnonymousMay 27, 2012

    Nyie watanganyika mbona munaongea vitu kama mbumbumbu, mnamtisha nani nyie wsws wenu ni kuwa sisi mkituachia tutaendelea. Malaysia waliwambia maneno ya kijinga kama hayo mnayosema nyinyi waliwambia mutakufa kwani hata maji ya kunywa walikuwa wanaitegemea malaysia, hebu angalieni wako wapi singapore, Sisi wazanzibari hatutowategemea hata kiberiti. Tuacheni tupumuwe na wele wake kikwete tunaomba umuenzi Mwalimu Nyerere kwani alisema wazanzibari wakitaka nchi yao sitowapiga mabomu. eweje wewe unaanza kutuuwa
    aluta kantinua

    ReplyDelete
  36. AnonymousMay 27, 2012

    Hahahaha eti tuwaache mpumue, hivi nyie zanzibar mnanini hasa mpaka tuwang'ang'anie?? Elimu hamna, madini hamna, wanyama pori hamna, ardhi hamna, umeme hamna, akili hamna kutwa kuchwa vijiweni kunywa kawaha, na vijana kibao wamekosa mwelekeo wamebaki kula unga na kuoana. kwendeni zenu

    ReplyDelete
  37. AnonymousMay 27, 2012

    time will tell...none senc 4 me..this is only benefit for politicians...waznz, hakuna kitakachobadilika hata mkijitenga..pia kumbukeni kuwa umoja na ni guvu..nadhani wengi wao hawajui wnachokitaka hasa..wapo wenye hoja na ambao wako tayari kuzijadili lakn wengi wao hawataki muungano lakn hawana hoja...wanadai kudhulumiwa, unadhulumiwa nini?.kitu cha un kina faida gani kwake hajui ila anakitaka...wameshiba mapembe hawa,,risasi hazijalia siku nyingi..subirirni

    ReplyDelete
  38. AnonymousMay 27, 2012

    time will tell...none senc 4 me..this is only benefit for politicians...waznz, hakuna kitakachobadilika hata mkijitenga..pia kumbukeni kuwa umoja na ni guvu..nadhani wengi wao hawajui wnachokitaka hasa..wapo wenye hoja na ambao wako tayari kuzijadili lakn wengi wao hawataki muungano lakn hawana hoja...wanadai kudhulumiwa, unadhulumiwa nini?.kitu cha un kina faida gani kwake hajui ila anakitaka...wameshiba mapembe hawa,,risasi hazijalia siku nyingi..subirirni

    ReplyDelete
  39. AnonymousMay 27, 2012

    Tena wafanye wagunge virago waondoke hagutaki kuwaona kianzia kkoo,ilala,mpaka magomeni fanyeni muondoke wala urojo nyie mmelegea kama mlenda.

    ReplyDelete
  40. AnonymousMay 27, 2012

    jamani si waache tu na zanzibar yao!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...