Wadau wetu wengi wamekuwa na shauku kubwa ya kuiona ile filamu ya "Mazimwi ya Nyakanga" iliyo tayarishwa na kampuni ya Kinkwin creative solutions (hhtp://www.kinkwin.com). Tunawaomba radhi sana wadau kuwa matayarisho ya filamu hiii yamechukua muda mrefu ili tuweze kuwapa kitu kilicho kizuri na sasa tumeweza kutekeleza azma hiyo. Tunayo furaha kubwa kuwajulisha kuwa filmu yenyewe imekamilika na inatarajia kuwa madukani kuanzia mwishoni mwa mwezi wa sita.
Filamu ya Mazimwi ya Nyakanga inaelezea maisha ya jamii ya zamani na mahusiano ya binadamu na Mazimwi. Kama wengi walivyokuwa wanatarajia, filamu hii ni ya kipekee kwani imetengenezwa kwa utaalam mkubwa na imesheheni visa vya kila namna, hasa effects nyingi za kushangaza na vilevile za kufurahisha.
Jambo kubwa na la muhimu ambalo wadau watalipenda katika filamu hii ni kuwa, filamu yenyewe imezingatia sana maadili ya Kitanzania. Ni filamu ambayo wazazi na watoto wanaweza kuitazama kwa pamoja na haina mambo ya wakubwa ambayo yanaweza kumfedhehesha mzazi mbele ya mtoto. Pia tumejitahidi sana kupunguza makali ya effects ili watoto wasitishike sana. Kwa kusema ukweli, mambo mengi yamezingatiwa ndani ya filamu hii na tumejaribu sana kufuata ushauri wa wataalamu wengi wa ndani na nje ya nchi.
Kwa sasa Kampuni yetu ya Kinkwin imetanguliza sokoni filamu zao mbili, ziitwazo Bijampora na Filongo ambazo nazo ni za kuvutia sana. Pia filamu ya Mazimwi ya Nyakanga itafuatiwa na ile filamu nyingine bomba zaidi iitwayo Kisa Cha Binti Binadamu na Zimwi ambayo ipo jikoni kumaliziwa
Tunapenda kuwahakikishia wadau wetu kuwa filamu za Kampuni ya Kinkwin zina ubora wa kipekee. Kampuni yetu ni kubwa na ina wataalamu walio bobea katika kuandaa hadithi nzuri, kuandika scripts na kutengeneza filamu kufuatana na utaalamu unao kubalika. Pia tuna vifaa vya kisasa kabisa katika kutengeneza filamu zenye ubora na tunawashirikisha wasanii walio bobea katika tasnia ya filamu Tanzania na kuinua vipaji vipya.
Jamaa wataleta mabadiliko makubwa ya tasnia kama mwendo ndio huo. Hii kampuni sijawahi kuisikia. Inapatikana wapi hapa Tanzania?
ReplyDeleteMwaaaaaaaah!
ReplyDeleteKitu kinaonekana kimetulia. Nahitaji kopi yangu mara moja ikitoka? je kutakuwa na uzinduzi ama itaingia madukani kinyemela? Inatengenezewa hapa Dar ama ulaya? nitapata wapi address ya hii kampuni ni ode kopi yangu moja kwa moja? Asante Michuzi kwa kutuletea hiki kitu maana nimeiangalia sasa ni mara ya tano
mtauza online pia sie wa nje ya nchi tuone?
ReplyDeleteCool!
ReplyDeleteWhere can I get this movie? It looks like the movie I saw from Africa known as " The gods must be crazy" kind of. Where can I get a copy?
Marie Stewart
Edmonton, Canada
Watengenezaji filamu za kulipua wajifunze hapa. Inaonekana jamaa ni wakali kinoma. Natamani niione filamu nzima.
ReplyDeletenimeangalia nimeumia macho picture quality ipo very poor.
ReplyDeleteI hope dvd, video etc hazipo hivi.
angalieni picture quality jamani labda inabidi mrekebishe.
hapo tu ndio mnapokosea move za kichawi?, harafu mnasema watanzania wanasubiri kwa hamu muvi ya kishenzi kama hii tumeisha ona sana kwa wanaigeria aina hii ya move na ilikua zamani sasa hivi hata wanaigeria zimewaboa hebu muakti move za kawaida plse
ReplyDeletePicha quality itakuwa imepunguzwa.
ReplyDeleteHii filamu ni nzuri wachana na ma haters. Kila kitu wao ni kupinga tuuuu. Hawajaona filamu nzima tayari walisha iponda. Wacheni kukatishana tamaa
ReplyDeleteKutakuwa na waosha vinywa wengi watakao ioshea vinywa kazi ya hawa jamaa lakini ukweli ni kuwa jamaa wanajitahidi tena sana.
ReplyDeleteNinaisubiri kwa hamu
effect sijaipenda, na quality yake sio nzuri, pia mpangilio wa visa sijaupenda. wajaribu kuweka effect ambazo zinavutia, wale mazimwi walizo na effect zao zio za ukweli waboreshe hizo effect.
ReplyDeleteSiyo mbaya. Ila ni filamu inayotisha, sidhani kama itakuwa nzuri kuangaliwa na watoto. Kuna jamaa mmoja kati ya hao waigizaji anafanana sana na Will Smith!!!!!!!!!!
ReplyDeleteJAMANI KWA NINI UTANZANIA NI KUDUMISHA UTAMADUNI WA KISHENZI "UCHAWI" KWELI NDIO MUAMKO WA MTANZANIA KATIKA KARNE HII? KWA HIO UCHAWI UHALALISHWE IWE KAWAIDA? HAYO NI MABO YA UTAMADUNI WA KIAFRIKA MIAKA YA 1130 ILIOPITA ,BADO TU MPAKA LEO? KWA NIN I KAMA MNAWEZA UCHAWI WA KUWANGA NA KURUKA NA KUMROGA MTU MSIWEZE KULETA SAYANSI ANGALAU YA KUTENGENEZA MASHINE YA KUSAGIA UNGA + AU KUTENGENEZA ANGALAU SINDANO YA KUSHONEA . MIMI KAMA MTANZANIA NAPINGA HICHO KITU NA WALA SIONI HAJA YA KUSHEHEREKEA UPUUZI KAMA HUO WA KICHAWI
ReplyDeleteTUNAWAOMBA RADHI WADAU KWAMBA ILITULAZIMU KUPUNGUZA QUALITY YA FILAMU SAAAANA ILI TUWEZE KUIPANDISHA KWENYE YOUTUBE (UNAJUA TENA KWIKWI YA INTERNET). TUNAWAHAKIKISHIA KWAMBA QUALITY YA FILAMU HII NI YA HALI YA JUU NA RANGI NA SAUTI VINAONGEZEWA VIONJO KITAALAMU HIVYO USIBABAISHIWE NA QUALITY UNAYOIONA. HII NI PROMO TU. PIA KUNA WALE WANADAI HII NI FILAMU YA KICHAWI. LA SIVYO. HII NI FILAMU INAYOELEZA MAISHA YA KALE. EFFECTS HAZIWEZI KUWA REAL, MAANA KAMA NI KUWA REAL BASI MTU ACHOMWE KIUKWELI. HIYO INAWEZEKANA?
ReplyDeletePIA USIBABAISHWE NA MPANGILIO WA SCENES AMA EFFECTS KWANI HII NI PROMO TU. UTAMU WA CHUNGWA UPO NDANI YA CHUNGWA NA SIO KWENYE KOKWA. UTATHIBITISHA HILI UKIITAZAMA FILAMU YENYEWE.
HATUENDEKEZI UCHAWI kwenye FILAMU HII. HADITHI YA FILAMU YENYEWE ni ndefu na INAONYESHA MTU ALIYE MUUA NDUGUYE KWA UCHAWI ILI ASHIKE MADARAKA LAKINI MWISHONI ANAAIBISHWA NA ANANYANGANYWA MADARAKA KWA AIBU. TUNACHOFUNDISHA NI KUWA UBAYA HAUNA FAIDA. HATA LEO KUNA WATU WENGI (HATA WALE WANAOJIITA WAKRISTO WALIOBOBEA ) BADO WANAKWENDA KWA WACHAWI AMA WAGANGA KUTAFUTA DAWA ZA KUANGAMIZA WENZAO. UCHAWI UPO NA NIA YETU NI KUUAIBISHA UCHAWI. FILAMU NZIMA INA STORY INAYOELEWEKA NA NI NZURI MNO. UKITAKA KUJUA STORY YENYEWE ITAZAME KWENYE PAGE YA KINKWIN.COM
ReplyDelete