Na Cheni Che-Mponda
Wadau, leo hii mtu wa rangi yeyote akija Marekani, anaweza kula sehemu yoyote, kwenda shopping sehemu yoyote na kuishi sehemu yoyote anayotaka bila kujali rangi.  Ni hela yako tu.  Lakini si miaka mingi uliyopita maisha hayakuwa hivyo kwa watu weusi. Weusi walibaguliwa Marekani kutokana na historia ya Utumwa. Ingawa utumwa ulifutwa mwaka 1865, ubaguzi dhidi ya weusi uliendelea. Ulipungua baada ya Civil Rights Acts (14th Amendment) ya mwaka 1964.

Miaka ya 1950's mwishoni  na 1960's nchi za Afrika zilianza kupata Uhuru.  Nchi hizo zilikuwa zinaleta Mabolozi kuwakilisha nchi zao.  Mabalozi na wafanyakazi wa ubalozi hizo walikuwa wanaleta familia zao. Walipohamia Marekani walishangaa ubaguzi uliokuwepo.  Kulikuwa hakuna kujali kuwa wewe ni balozi. Ukiwa ni mweusi, hivyo mtu wa chini tu. Ubaguzi huo ulisbabisha Waziri Mkuu wa Urusi wa wakati huo , Nikita Khrushchev,kuomba Umoja wa Mataifa uhamishwe nje ya Marekani!  Ilibidi Rais John F. Kennedyaingilie. Ubaguzi katika restaurant na mahoteli ulipigwa maarufuku katika sehemu kadhaa Washington, D.C. na Maryland. Fikiria ubaguzi ulikuwa ni shida kiasi kwamba Rais Kennedy alisema kuwa waafrika wapande ndege wakiwa wanasafiri kutoka New York hadi D.C. ili waepuke matatizo ya kibaguzi.

Ubaguzi ulivyokithiri na wazungu walivyoona ni haki yao kubagua, weusi mwenye Mgahawa moja alisema, "Mwache Rais Kennedy awalishe hao WaAfrika! Mimi sitaki kupoteza biashara yangu!"

Mambo ya Ubaguzi dhidhi ya waafrika ulifika kilele, mwaka 1961, Balozi Malick Sow wa Chad alipoenda kula katika restaurant iitwao Bonnie Rae Diner. Alinyimwa huduma na kupigwa na mhudumu kutokana na rangi yake. Balozi Sow alikasirika na kulalamika hadi White House. Yule mhudumu aliyemnyima huduma alipohojiwa na LIFE magazine alisema, "Mimi sikujua ni Balozi. Nilidhani ni mwesui (n-word) wa kawaida!"

Habari ya Baolzi Sow, ulikuwa ni habari ya kimataifa. LIFE magazine ambayo kipindi kile kilikuwa kama CNN ya leo, iliandika habari hizo. Weusi waliporuhusiwa kula mezani pale sawa na mzungu, LIFE magazine walikuwepo.  Baba yangu, Dr. Aleck Che-Mponda, ambaye wakati ule alikuwa katika uongozi wa Chama cha Wanafunzi wa Afrika wanaosoma Marekani na Bayo Adekayo wa Nigeria walikuwa wa kwanza kuhudumiwa.

Mnaweza kusoma habari kamili katika toleo ya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Hi Michuzi, asante sana kwa kuposti. Waafrika waliokuwepo miaka ya 1950's 1960's Marekani walipata shida sana kutokana na ubaguzi. Walichangia katika mapambano na weusi (African Americans0 waliopo Marekani. Kutokana na mchango wao, leo hii maisha ni afadhali zaidi kwa mtu wa rangi yoyote. Tusisahau tuliptoka.

    Chemi

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 08, 2012

    Hawakutokomeza ubaguzi kwani bado upo na sehemu nyingine wa wazi kabisa. Ila walisaidia.

    Babu yangu alikuwepo kwenye haya mapambano ya kibaguzi pia na namshukuru sana, ingawa alitishiwa maisha na kulazimika kukimbilia Tanzania.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 08, 2012

    Sasa wazungu wanakuja huku kwetu kutaka rasilimali zetu. Na sisi tuwabague?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 08, 2012

    Ni kweli kuwa ubaguzi wa rangi umepungua KIDOGO USA. Hata hivyo, naomba nitoe mifano miwili kuonyesha ubaguzi dhidi ya weusi bado upo. (1)Katika miaka ya 1980's, huko Boston, rafiki yangu Mtanzania alikuwa na mwenzake wa Swaziland wakati wa summer wakirudi chuo kikuu. Kwa bahati mbaya wakapita katika mtaa mmoja wa wazungu watupu. Akatokea mzungu mmoja na bunduki akawasimamisha. Akawaambia hamjui kuwa "niggers" hawatakiwi hapa? Wao wakajibu kuwa wao ni wageni hawakulijua hilo. Yule mzungu aliposikia lafudhi yao akajua wao si wamarekani. Akawasamehe na kuwaonya. Katika mazungumzo yao, mzungu akawaambia "I didn't know they had niggers in Tasmania and Switzerland"! (2)Mimi na mke wangu 2008, tulikuwa New Jersey (one of the least racist states in USA) katika gari letu. Bahati mbaya tukajikuta katika enclave moja ya trailer park ya ma-rednecks (makabwela au walalahoi wa kizungu). Katika kutaka kumuuliza mzungu mmoja njia ya kwenda Princeton, mzungu akatujibu "We don't wanna see any f***** nigger here!" Kidogo wakatokea wazungu wengine watatu. Hayo matusi waliotutukana sithubutu kuyaandika popote. Ndugu Anonymous wa 08:02:00 AM 2012. Jibu ni kuwa SISI TUSIWAIGIE KWA KUWABAGUA WATU WENGINE. We must hold the upper moral ground. Mahatma Ghandi alisema "An eye for an eye will leave all of us blind". Au kama kule UK wanavyosema "Two wrongs don't make a right". Aidha roho, nafsi na akili isiyo na chuki ni bahati ya wanaadamu waliosalimika kiroho. Ashakum si matusi. Tuwaachie ma-racists waanike chupi zao zenye kinyesi hadharani. Tusiwaige kwa hilo.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 08, 2012

    Miaka hiyo hiyo mnayosema,mimi nilikuwa naenda Makerere.Nilikuwa nimevaa sports jacket na tai, niliingia hoteli moja Nakuru. Mzungu akamwambia mbantu aje kuniarifu kuwa "sorry no service for your kind"

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 08, 2012

    Ubaguzi hupo na unaendelea kuwepo.Ila Chemi labda umetoka Bongo au umelelewa Bongo unaona Amerika kwako paradiso,ila ukiongea na Wamerkani weusi watakuwambia ubaguzi hupo.Kosa kubwa lilikuwa ni mwafrika kuuzwa utumwani na kununuliwa minadani.Ambayo ilifanywa na wachifu wa kiafrika na Wazungu.Umasikini na ombaomba ya viongozi wetu wa kiafrika inazidi kuchafua image ya Mtu mweusi kwa ujumla.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 08, 2012

    Wazungu mkiwabagua na wakiondoka huko si mtakufa maana hamna kitu kinachofanyika bila wao huko Bongo kweusi,mapema tu wataanza kuwachimbia vyoo vya kujisaidia.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 08, 2012

    Uzuri wa wafrica si watu waoga, wamesambaa kila kona ya dunia, na wamekua nai changamoto kwa jamii ya watu mbalimbali, hao wazungu wenyewe wa marekani wakija uko kwao ulaya walikotokea, wanawaona wafrica wamejaa kibaoo, kwa hiyo mtu mweusi kila kona dunia ya leo, na mpenda maendeleo vile vile, na anajituma

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 08, 2012

    Mpaka sasa ubaguzi upo mkubwa sana hapo Marekani. Mwafrika bado anaonekana ni mtumwa tu. Yapo maeneo waafrika hawaendi. Nimeyaona haya kwa macho yangu nilipokuwa huko hivi karibuni. Ubaguzi wa rangi ni jambo la dhahiri katika Marekani ingawa sheria zinasaidia kwa kiwango fulani.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 08, 2012

    Ubaguzi wa rangi upo hadi leo hii tena hapo hapo Zanzibar na Bongo. Mbona kuna hoteli mwaziita eti za kitalii na wazawa hawaruhusiwi? Tena msiende mbali ni hapo hapo bongo/Zenji!!!
    Mbona waarabu/wamanga hapo bongo ukitaka kuwaolea dada zao hawataki?

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 09, 2012

    Hao wamanga wewe usiende kichwa kichwa eti unataka kuoa. Wewe piga chini mtu avimbe juu hapo hawana jinsi ndoa ya mkeka mapemaaaa...lol

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...