Gari aina ya Suzuki yenye nambari za usajili T 525 BWK ikiwa imeigonga bajaj yenye nambari za usajili T 581 BQY jioni ya leo na kusababisha dereva wa Bajaj hiyo kujeruhiwa.chanzo cha ajali hiyo ni kukatika kwa kamba iliyokuwa ikitumika kuivuta gari hiyo na kupelekea mtu aliekuwa anaiongoza gari hiyo iliyokuwa ikivutwa na pikipiki nyingine ya matairi matatu (haipo pichani) kushindwa kuiongoza gari hiyo na kufikia hatua hii.
Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa baada ya gari hiyo kuigonga bajaj
Wasamalia wakiongea na Dereva wa Bajaj ambaye alirushwa kutoka kwenye chombo hicho hadi nje na kumfanya kujeruhiwa katika mikono yake na eneo la kichwa.
Hii ndio pikipiki yenyewe iliyokuwa ikiivuta gari hiyo.
Mashuhuda wakiangalia tukio hilo.
bongo tambarare....haahaaa!!sasa kweli hiyo kamba toka lini ikavuta gari?hapo alieumizwa hata kulipwa halipwi inakula kwake tu na samahani kibao.....
ReplyDeleteDavid-Muni
Manchester