- Kila upande wa Muungano uchimbe Mafuta na Gesi Asili yake na Mapato yawe ya Serikali ya upande husika.
- Shughuli za Utafutaji kwenye vitalu vyenye mgogoro ziendelee mara moja
- Zanzibar ianzishe Shirika lake la Mafuta (PetroZan)
- Katiba mpya itofautishe utafutaji (upstream) na Biashara (uchimbaji, midstream na downstream)
Moja ya suala linalosubiriwa kwa hamu kubwa katika mjadala na hatimaye uandishi wa Katiba mpya ni suala la Mafuta na Gesi Asilia kuwa jambo la Muungano au liondolewe katika orodha ya mambo ya Muungano. Suala hili limezusha mjadala mkubwa sana mara kwa mara nchini Tanzania kiasi cha lenyewe kuwa ni hoja ya wale wasiotaka tuwe na Dola ya Jamhuri ya Muungano Tanzania.
Wakati Muungano unaanzishwa mwaka 1964 Mafuta na Gesi hayakuwa masuala ya Muungano. Nimeangalia katika Hati ya Muungano ambayo ilikuwa ni sehemu ya Katiba ya Muda ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1965, suala hili halikuwamo katika orodha ya mambo Kumi na Moja ya Muungano. Nyaraka nilizoziona zinaonyesha kwamba suala la Mafuta na Gesi Asilia liliongezwa katika orodha ya Mambo ya Muungano mwaka 1968. Kuna watu wanahoji kihalali kabisa kwamba nyongeza ya jambo hili ilifanywa bila kufuata taratibu na hivyo kufanywa kinyemela na kuna wengine wanasema jambo hili lilifuata taratibu zote za kisheria ikiwemo kupigiwa kura na Bunge la Muungano na kuungwa mkono na theluthi mbili ya Wabunge kutoka pande zote za Muungano.
Katika moja ya vikao vya Bunge katika Bunge la Tisa, aliyekuwa Naibu wa Waziri wa Nishati na Madini Ndugu Adam Malima alileta kumbukumbu za mjadala Bungeni (Hansard) za mjadala wa suala la Mafuta na Gesi ili kuthibitisha kwamba jambo hili halikuuingizwa kwenye Katiba kinyemela.
Wakati umefika kwa Watafiti wa Masuala ya Muungano wakapekua nyaraka hizi na kutwambia ukweli ulio ukweli mtupu wa namna suala la Mafuta na Gesi lilivyoingizwa katika orodha ya mambo ya Muungano. Hata hivyo, jambo hili sasa ni jambo la Muungano kwa mujibu wa Katiba na ni dhahiri kuwa WaTanzania wa Zanzibar hawafurahiswhi nalo na hivyo kuazimia kupitia Azimio la Baraza la Wawakilishi kwamba jambo hili liondolewe kwenye orodha ya masuala ya Muungano. Kwa vyovote vile Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inapaswa kutoa uamuzi wa mwisho utakaomaliza mjadala huu.
Jambo la kusikitisha ni kwamba licha ya Bunge la Muungano kuamua kuongeza suala la Mafuta na Gesi asilia katika masuala ya Muungano, mwaka mmoja baada ya uamuzi huo likaundwa Shirika la Maendeleo ya Mafuta Tanzania (TPDC) kwa amri ya Rais wa Jamhuri ya Muungano (establishment order). Shirika hili halikuanzishwa kwa Sheria ya Bunge au kwa Sheria ya Makampuni kama yalivyo Mashirika mengi ya Umma hapa nchini bali kwa amri ya Rais ya mwaka 1960. Katika amri hii ya Rais, Shirika la TPDC halikupewa ‘mandate’ ya kimuungano. Shirika hili mipaka yake ilianishwa kuwa ni Tanzania bara peke yake. Hivyo suala la Muungano likawekewa Shirika la Tanganyika kulisimamia!
Kama ilikuwa ni bahati mbaya au makusudi au kupitiwa kwa viongozi wetu wa wakati huo ni vigumu kujua lakini huu ni mkanganyiko mkubwa ambao ulipaswa kurekebishwa mapema sana.
Shirika la TPDC limekuwa likifanya kazi ya kusimamia Sekta ya Mafuta na Gesi ikiwemo kutoa vibali vya kutafuta mafuta, kuingia mikataba na Makampuni ya kimataifa na kuisimamia mikataba hiyo. Miongoni mwa mikataba hiyo ni kwenye maeneo ambayo kama isingekuwa Muungano yangekuwa ni Maeneo ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Mbaya zaidi Mikataba yote ya utafutaji na uchimbaji Mafuta inafanywa inaingiwa na Waziri wa Nishati na Madini Wizara ambayo sio ya Muungano. Hakuna hata eneo moja ambalo taratibu zimewekwa kwamba pale ambapo eneo hilo ni eneo lilikuwa chini ya himaya ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar basi mikataba isainiwe na Mawaziri wawili wa sekta hiyo kutoka kila upande wa Muungano.
Ni dhahiri kwamba kama ni kusahau hapa kulikuwa na kusahau kukubwa ambako hakustahmiliki kwa mtu yeyote mwenye upeo achilia mbali mwananchi wa kawaida wa Zanzibar ambaye anaona anaonewa na kugandamizwa na Bara.
Mnamo miaka ya mwanzo ya 2000, Shirika la TPDC liliingia mikataba ya Vitalu kadhaa vya Mafuta miongoni vya vitalu hivyo ni vitalu nambari 9, 10, 11 na 12 mashariki ya visiwa vya Pemba na Unguja. Vile vile Shirika na Wizara ya Nishati waliingia mkataba mwingine katika Kitalu kilichopo kati ya Pemba na Tanga (mahala ambapo kumekuwa na dalili za wazi za kuwapo Mafuta kutokana na kuonekana kwa ‘Oil sips’ mara kwa mara.
Vitalu 9, 10, 11 na 12 vilipewa kampuni ya Shell ya Uholanzi na kitalu cha kati ya Tanga na Pemba walipewa Kampuni ya Antrim ya Canada ambayo baadaye waliuza sehemu ya Kampuni yao kwa Kampuni ya RAK Gas kutoka Ras Al Khaimah huko United Aarab Emirates. Kwa kuwa Vitalu hivi vipo katika eneo la iliyokuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar kabla ya Muungano, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilikataa shughuli zozote kufanyika mpaka suala la Mafuta na Gesi kuondolewa katika orodha ya Mambo ya Muungano lipatiwe ufumbuzi.
Uamuzi huu wa Serikali ya Zanzibar ni uamuzi ambao ungechukuliwa na Serikali yeyote ile yenye mapenzi ya dhati na watu wake. Uamuzi huu ulileta mjadala mpana sana katika masuala ya Muungano na ambao hawana taarifa waliubeza sana. Hata hivyo suala hili likafanywa ajenda katika vikao vya masuala ya Muungano vinavyoitwa Vikao vya Kero za Muungano. Miaka kumi suala hili linajadiliwa na Maamuzi hayafanyiki! Hivi sasa kila suala lenye kuangukia kwenye Katiba husukumwa huko na hivyo kutoa ahueni kwa wanaogopa kufanya maamuzi.
Katika medani za uchumi kila suala lina muda wake. Masuala ya utafutaji wa Mafuta ni masuala yanayoongozwa na msimu na kuendelea kuchelewa kufanya maamuzi juu ya suala hili kunalitia hasara Taifa, Hasara ya Mabilioni ya Fedha na hasara kubwa zaidi ya kufahamu utajiri uliojificha chini ya Maji ya Bahari inayozunguka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hivi sasa Pwani ya Afrika Mashariki inarindima (trending) katika utafutaji wa Mafuta na Gesi asilia. Huko Msumbiji Makampuni mbalimbali yamegundua Gesi asilia nyingi inayofikia zaidi ya futi za ujazo trillion 107 (107TCF) kwa makadirio ya chini. Hapa Tanzania utajiri wa Gesi asilia uliogunduliwa hadi hivi sasa na kutangazwa umefikia futi za ujazo trillion 20 (20TCF) ambazo ni sawa na utajiri wa thamani ya dola za kimarekani trillion 6. Makadirio yanakisiwa kuwa Tanzania kuna futi za ujazo trillioni 85 (85TCF) za Gesi Asilia katika eneo la Kusini kuanzia vitalu namba 1 mpaka namba 5 ikiwemo vitalu vya nchi kavu na vile vya Songosongo.
Iwapo kasi ya utafutaji mafuta itaendelea kama sasa katika kipindi cha miaka 2 ijayo Tanzania itaweza kuwa kati ya nchi mbili za Afrika zenye Utajiri mwingi zaidi wa Gesi Asilia. Hivi sasa Nigeria ndio inaongoza kwa kuwa na futi za ujazo trillion 189 (189TCF) ikifuatiwa na Algeria na Angola ambazo zote zina utajiri wa juu kidogo ya 100TCF kwa Algeria na chini ya 100TCF kwa Angola. Msumbiji sasa imeifikia Algeria na kushika nafasi ya pili.
Katika masuala ya Mafuta na Gesi hatua ya kwanza ni kujua kama utajiri huu ambayo kitaalamu inaitwa gas exploration. Shughuli za utafutaji zinapandisha sana thamani ya nchi na eneo la nchi. Kwa mfano hivi sasa kitendo cha Kampuni ya Uingereza ya BG/Ophir na ile ya Norway ya StatOil kupata mafanikio makubwa katika utafutaji wa Gesi asilia kumeongeza thamani ya Pwani ya kusini ya Tanzania katika medani za utafutaji (Exploration Activities).
Hata hivyo kama ilivyogusiwa hapo juu, shughuli za Utafutaji ni shughuli za msimu. Pia huchukua muda mrefu wa kati ya miaka 5 mpaka 10 kati ya kutafuta, kupata na kuanza kuchimba. Hivi sasa ni muda wa pwani ya Afrika Mashariki. Ni lazima kuhakikisha kwamba vitalu vyote vilivyogawiwa hivi sasa vinafanyiwa kazi. Hata hivyo vitalu vingine vyovyote visigawiwe kwanza mpaka hapo matunda ya vitalu vya sasa yaonekane. Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini imependekeza kusimamisha kugawa vitalu vipya. Matokeo ya utafutaji katika vitalu vya sasa yakiwa mazuri kama ilivyo sasa, thamani ya vitalu vipya itapanda sana na nchi itakuwa na nguvu ya majadiliano (strong negotiation position) dhidi ya makampuni makubwa ya mafuta.
Tufanyaje kuhusu vitalu vilivyogawiwa katika eneo ambalo lina mgogoro kuhusu suala la Muungano? Sio kazi rahisi lakini imefikia wakati tuamue. Kwa kadri nionavyo, Itabidi kuwe na maamuzi ya mpito (interim decisions) na maamuzi ya muda mrefu.
Kwanza, ni lazima kukiri tulipokosea. Hata kama ilikuwa ni sahihi kiutaratibu kuweka suala la mafuta na Gesi katika orodha ya mambo ya Muungano, haikuwa halali Shirika la TPDC lenye mipaka ndani ya Tanzania bara kuingilia ugawaji wa vitalu na kuingia mikataba katika maeneo ambayo ni ya Muungano. Ni Taasisi ya Muungano tu ndio inaweza kushughulikia suala la Muungano na sio vinginevyo.
Ilikuwa ni dharau kubwa sana kwa Waziri wa Nishati ambayo sio Wizara ya Muungano kuingia Mikataba katika eneo la Zanzibar (ambapo kikatiba tumelifanya eneo la Muungano) bila kushauriana na kukubaliana na Waziri wa Nishati wa Zanzibar. Kukiri kosa sio unyonge, ni uungwana. Hata tukifanya vikao milioni moja chini ya Makamu wa Rais, bila kukiri kosa hili tatizo hili na mengine ya aina hii hayataisha.
Pili, ni vema kukubali kwamba shughuli za utafutaji katika vitalu vyenye mgogoro ziendelee kwenye hatua ya utafutaji tu. Kama mafuta au Gesi ikipatikana, uchimbaji usianze mpaka uamuzi wa mwisho kuhusu suala hili uwe umepatikana. Pia ninapendekeza ufumbuzi wa mwisho hapa chini. Kuchelewesha utafutaji ni hasara kwa pande zote za Muungano kutokana na taarifa za kijiolojia zitakazopatikana na hivyo kupandisha thamani ya nchi hizi mbili kijiolojia.
Hata hivyo, utafutaji huu katika eneo lenye mgogoro kati ya pande mbili za Muungano ufanyike baada ya mkataba wa PSA kufanyiwa marekebisho makubwa. Marekebisho hayo ni pamoja na Mkataba kusema wazi kwamba shughuli za uchimbaji zitafanyika iwapo tu makubaliano ya kugawana mapato ya Mafuta na Gesi kati ya Serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar yamefikiwa. Pia Mkataba uzingatie maendeleo ya sasa ya kusini mwa Tanzania na hivyo mkataba uboreshwe kwa faida ya nchi ikiwemo kutolewa kwa ‘signature bonus’. Hii ni Fedha inayotolewa na Kampuni za utafutaji Mafuta kwa Serikali kabla ya utafutaji kuanza. Kiwango hutokana na majadiliano na kukubaliana. Nchi zenye jiolojia iliyopevuka hutumia njia hii kuongeza mapato ya Serikali.
Mkataba pia useme kinaga ubaga kwamba utasainiwa na Mawaziri wa pande mbili za Muungano na kwamba Kampuni inayofanya utafiti itatoa taarifa zake za Utafiti sawia kwa Mawaziri wote kwa mujibu wa vipengele vya mkataba.
Kwa upande wa maamuzi ya muda mrefu, ushauri wangu ni kwamba; kwa maana ya kuandikwa kwenye Katiba mpya ni kwamba Suala la Mafuta na Gesi Asilia liendelee kuwa suala la Muungano kwenye eneo la usimamizi wa Tasnia na leseni za utafutaji (Upstream Regulatory mechanism). Hili ni eneo linalohitaji usimamizi wa dhati kabisa na kwa pamoja pande mbili za Muungano zinaweza kufanya vizuri zaidi.
Eneo la Uchimbaji na hasa kugawana mapato ya mafuta na Gesi (Profit Oil) lisimamiwe na kila upande wa Muungano kivyake. Biashara ya Mafuta isiwe jambo la Muungano na hivyo kila Upande wa Muungano uwe na Shirika lake la Mafuta na Gesi ambalo litashiriki kama mbia wa Mashirika ya Kimataifa katika uchimbaji, usafirishaji na uuzaji wa Mafuta na Gesi Asilia. Mapato yanayotokana na Mafuta (Profit Oil) na kodi nyingine zote isipokuwa mrahaba (royalty) yawe ni masuala yanayoshughulikiwa na Serikali ya kila upande wa Muungano kwa mujibu wa Sheria ambayo Serikali hizo zimejiwekea.
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma ilipendekeza Bungeni kwamba kuwepo na Mamlaka ya Mafuta na Gesi Asilia Tanzania (Tanzania Petroleum Authority) ambayo itakuwa ni msimamizi (upstream regulator) kama suala la Muungano. Mrahaba wa Mafuta na Gesi ambao sasa ni asilimia 12 ya Mapato ya Mafuta itakusanywa na Msimamizi huyu na ndio mapato pekee katika tasnia ya Mafuta na Gesi yanapaswa kuwa mapato ya Serikali ya Muungano.
Kamati pia ilipendekeza kuanzishwa kwa Shirika la Mafuta na Gesi (Petroleum Tanzania - PetroTan) ambalo litakuwa mbia kwenye Makampuni ya utafutaji na uchimbaji wa Mafuta na Gesi kwenye Vitalu vya Tanzania bara. Mapato yote ya vitalu vya Tanzania bara na kodi zote isipokuwa Mrahaba zitakwenda kwa Mamlaka za bara tutakazo kuwa tumeamua baada ya Katiba mpya kuanza kazi. Hivi sasa TPDC inafanya kazi hii mpaka Zanzibar jambo ambalo hata kwa akili ya kawaida halipaswi kukubalika.
Aidha, napendekeza kwamba Zanzibar ianzishe Shirika lake la Mafuta sasa. Jambo hili halina haja ya kusubiri vikao vya kero za Muungano kwani ni dhahiri TPDC haina mamlaka,ushawishi na uthubutu kusema uhalali wa kusimamia vitalu vya Mafuta vilivyopo Zanzibar.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ipeleke muswada katika Baraza la Wawakilishi kuanzisha Shirika la Mafuta na Gesi la Zanzibar (Petroleum Corporation of Zanzibar – PetroZan) ili liweze kushiriki katika utafutaji na uchimbaji wa Mafuta Zanzibar. Lakini Pia PetroZan ilinde maslahi ya Zanzibar katika tasnia hii kwa kujijengea uwezo wa kusimamia ugawaji bora wa Mapato kutoka katika Mafuta na Gesi Asilia.
Kama Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inachelea kuanzishwa kwa Shirika hili, Wawakilishi wa pande zote (CCM na CUF) wapeleke muswada binafsi kuunda Shirika la Mafuta la Wazanzibari. Hawatakuwa wamevunja Katiba ya Muungano kwani hivi sasa hakuna Taasisi yenye mamlaka ya kusimamia Tasnia hii kwa Upande wa Zanzibar.
Wakati haya yote yanafanyika, shughuli za utafutaji Mafuta na Gesi katika vitalu vilivyopo katika eneo la Zanzibar na hasa vitalu namba 9,10,11 na 12 na katika kitalu cha kati ya Pemba na Tanga ziendelee kufuatia marekebisho ya Mkataba wa Utafutaji. Utafutaji wa Mafuta una faida zaidi kwa Nchi hizi mbili kuliko kwa Kampuni za Mafuta kwani uwekezaji wa Kampuni pekee na nchi zitapata taarifa za kijiolojia zitakazosaidia mikataba ya baadaye kuwa bora zaidi.
Wakati nasisitiza kwamba tuendelee na utafutaji katika vitalu tajwa, katika Katiba mpya, utafutaji wa mafuta usimamiwe na Taasisi ya Muungano. Uchimbaji na biashara ya Mafuta ufanywe na kila Serikali ya kila upande wa Muungano. Mafuta kuwa jambo la Muungano halafu kusimamiwa na Shirika la Tanganyika na Wizara ya Upande mmoja ya Muungano ndio chanzo cha mgogoro. Suluhisho sio kuifanya TPDC kuwa Shirika la Muungano, bali kila upande upewe uhuru wa kusimamia uchimbaji, Biashara na mlolongo mzima wa tasnia ya Mafuta (value chain from midstream to downstream) isipokuwa utafutaji (upstream). Hili ndio suluhisho la kudumu ninaloona linafaa.
Uwazi (declaration):
Zitto Kabwe ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini na mfuatiliaji wa karibu wa Tasnia ya Mafuta na Gesi Asilia akiwa amesomea mfumo wa uchumi wa katika tasnia ya madini na mafuta (fiscal regime in Mineral and Petroleum sector). Zitto pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma ambayo inasimamia mahesabu na utendaji wa Shirika la TPDC. Makala hii imeandikwa baada ya ziara ya Mafunzo ya Wabunge kutembelea nchi ya Uholanzi kwa ufadhili wa Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo. Katika ziara hiyo Wabunge hao walikutana na Wakuu wa Shirika la Mafuta la Shell ambapo walizungumzia pia suala la vitalu namba 9, 10, 11 na 12.
Tulishirikiana umeme iweje mafuta yawe pande tofauti, muhimu tusinyimane matumizi wala mapato , we need symbiotic union.
ReplyDeleteLiving in symbiosis, or having an interdependent relationship: Many people feel the relationship between humans and dogs is symbiotic.
Zitto Kabwe umetadhmini kwa kina kuhusu swala la mafuta, kuwa nnje ya muungano maana yake nini ? Nini adhali na faida zake ? Kitu cha kwanza nakutahadhalisha kwamba kwa mawazo yako, itabidi mipaka ya nchi iwekwe, Zanzibar na Tanganyika. Kuonyesha mafuta katika eneo hili ni ya Zanzibar na ya eneo hili ni ya Tanganyika. Pili unafahamu kuwa mafuta yakuwa kwenye mkondo hayatuami tu, Je unadhani tukishaanza kuwekeana mipaka nini kitafuata ? Je uchimbaji utakuwaje na nini adhali zake kama mkondo huo uko huku na huku. KWA HAYO MACHACHE NAKUSHAURI UWE UNAFATAFAKARI NA KUFANYA UTAFITI WA KINA KABLA YA KUSEMA HASA MANENO MAMBO YANAYOWEZA KUFUFUATA UTOFAUTI KWA WATANZANIA
ReplyDeleteNIGERIA GAS TRILLION KADHAA, ANGOLA, MSUMBIJI, ALGERIA, NA SASA TANZANIA NAO WATAZALISHA TRILLION ZA GAS/MAFUTA.
ReplyDeleteHIVI NYIE WAWANASIASA MNADANGANYA WATU KAMA WATOTO WANAOPEWA PIPI.
NIJA, ANGOLA, MSUMBIJI NA HATA HUKO BONGO, TUELEZENI NI MWANANCHI GANI ANAYENUFAIKA NA MALI ASILI HIYO.
KAZI KUENDESHA MAGARI YA KIFAAHARI, KUTIBIWA NJE YA NCHI, WAKATI WALALAHOI HAWANA HATA ASPIRIN HOSPITALI.
CONGO DU ZAIRE INA KILA MALI YA KUMFANYA KILA MTU TAJIRI. LAKINI MAMILIONI YOTE YANAJAA KWENYE AKAUNTI ZA WKUBWA HUKO JERSEY NA SWISS BANK.
KWA HIYO NDGUGU KABWE, MFANO MZURI NIMEKUPA HUO. HAO WANAOTAKA KUJITENGA WAJITENGE TU. MBONA SUDAN SASA ZIPO MBILI SEMBUSE TANZANIA AMBAKO ZANZIBAR INA JINA LAKE. HAITOITWA TANZAN ANYWAY. JUST ZANZIBAR!!!
ZENJI NI SAWA NA MTOTO ALIYEBALGHE ANATAKA KUHAMA KWA WAZAZI WAKE AKAJITEGEMEE. NANI APUNGUZIWAYE MZIGO HAPO?
SCOTLAND KADHALIKA IPO KWENYE PROCESS YA KUJITENGA UK. KWA HIYO SI JAMBO JIPYA...MNANG'ANG'ANIA NINI?
WAKIJITENGA SHERIA MPYA NA KATIBA MPYA YA TANZANIA (BILA ZANZIBAR) ITUNGWE NA KILA MPEMBA AU MUUNGUJA AISHIE TANZANIA, AREJEE KWAO...SIMPLE.
WAKITAKA KUISHI ARDHI YA TANZANIA, WAOMBE KIBALI CHA KUISHI IKIWA PAMOJA NA KULIPA ADA YA MAKAZI KWENYE OFISI ZA UHAMIAJI TENA KWA DOLA A KIMAEKANI!
WAKITAKA KUISHI KIBIASHARA KUVUA SAMAKI, KUUZA VIDUKA MKOBA, GENGE LA NYANYA NA DAGAAA, WALIPISHWE KODI ZA BIASHARA. HAWAWEZI MLANGO UPO WAZI.
WAKONGO, WACHINA WAPO HAPO NA WANALIPA KODI YA MAKAZI KILA MIEZI 12 AU MIAKA 2/3. HAWAWEZI SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
KWENYE USAFIRI KADHALIKA VYOMBO VYA NCHI KAVU NA MAJINI, VIWEKE UWAZI VIMESAJILIWA WAPI NA VIKIINGIA NA KUTOKA KODI KIMATAIFA ILIPWE KAMA KAWA.
MZANZIBARA
AGREED!
ReplyDeleteUnatetea waislam wenzako!! jifunze kutenganisha dini na serikali. Mnafiki mkubwa wewe.
ReplyDeletekaka zitto, hakuna anayekufikia mpaka sasa..unafaa kuwa rais siku za usoni..ushauri wangu kwako tu ni kwamba isije ikawa nguvu za soda..hoja zako hakuna wa kupinga, hata akipinga anakuwa hawezi kujibu hoja..nakubaliana na wewe 100% ila sasa tunataka mawazo ya wenye uwezo wa kufikiri kutoka zanz kama wanaweza kuafikiana na hili maana mm kwa sasa niko zanz na inavyoonekana wengi wao hawataki kabisa kabisa muungano na hawana hoja za msingi ila bendera fuata upepo tu...naomba uongee na sheni, sharif bilal uwape wazo hili ili walifikishe kwa waznz nina iman wataliafiki..mim binafsi napenda muungano uwepo lakn tu uboreshwe kwenye uonevu.
ReplyDeleteNdugu Zitto, Energy is national security and I strongly disagree with you that this should not be union matter.
ReplyDeleteJamani tulieni !!! nchi sasa hivi ina vijana wenye hekima ,busara na waaminifu,ndiyo maana kuna dalili ya mabadiliko kote Zanzibar na Tanganyika (Tanzania) kumbukeni jamani,tangu tujitawale tulikuwa hatuna uhuru wa kuuliza au kuona nini kinafanywa na serikali yetu,hii imechangia sana kubaki nyuma ki maendeleo katika nchi yetu. Tuna viongozi wenye uchungu na kiu ya maendeleo wapyaa kama kina Zitto, Mnyika, Makamba na wengine wengi-ndugu zanguni, tuwapeni muda,haraka haraka haina baraka,utengano ni udhaifu.Itakuwa vigumu kuitenga Zanzibar,je ?? hao wanyamwezi walioko Zanzibar mtawapeleka wapi ?? nyie wachache mnaotaka kutugawa, hebu chunguzeni kwanza, mambo mengi sana hamyajui ila jeuri na kashifa,hii inaonyesha kukosa busara na hekima, tuwaachieni watu wenye kujua kiundani kama kina ZITTO waturekebishie pale palipojipinda. Lazima tukubali kuongozwa ,haiwezekani wote tukawa viongozi au wote tukawa watunga sheria.Kamwe hatutafika mbali bali tutachinjana tu. Naiomba serikali iongeze ulinzi katika kipindi hiki kigumu cha kurekebisha mambo,hao wachache wanaotaka kuchochea vurugu, basi virungu vya FFU vitumike,hatuwezi kuishi kwa woga na vitisho vya wachache.Pia naiomba serikali iendeshe operation saka saka kwa wale waliojichukulia sheria mikononi mwao,huko GEITA na kuwaua wanawake vikongwe eti kwa kuwatuhumu kuwa wachawi. Habari nilizozisoma katika gazzeti la Nipashe ,zimenifanya nitoe machozi . Ujinga huu , utokomezwe kwa nguvu za dola, hali kama hii ya GEITA inaweza kujitokeza Zanzibar,kuwa saka ambao siyo Wazanzibari na kuwa piga hadi kufa. Wapenda amani, nawasihi sana ,tuzikemee tabia hizi za uchochezi-Zanzibar kutageuka GEITA, tuliwashangaa wenzetu watusi na wahutu walipochinjana, sasa yanakuja na kwetu. Zebedayo.
ReplyDeletehaya wasiopenda ukweli mbona leo kimya au kasema mtu wa upande wa kwenu?
ReplyDeleteJAMANI WATANZANIA MIMI KWA MAWAZO YANGU TUACHANE NA HAO WAZANZIBARI KWANI NINI TUNAKOSA KUTOKA KWAO HATA TANGA KARAFUU YAWEZA PANDIKA NA IKAVUNWA , WATU NI WASHENZI WAJINGA , HAWANA ELIMU. WALA MAANDISHI YAO HAYASOMEKI WAACHENI NA WAFUKUZWE WOTE HAPA BARA NA WOTE HAO SIJUI PEMBA ,UNGUJA, ZANZIBAR SIJUI USHENZI GANI WAWEKEWE VIZA KUJA BONGO, NA NA WASIPATE VIZA YA ZAIDI YA WIKI 2 KAMA HIO GAS YAO WANA WEZA KUICHIMBA ACHA WACHIMBE HATA BARA TUTACHIMBA IKO NYINGI TU ZAIDI YA HUKO, KAMA MASHOGA HATA BARA WAKO KWA NINI WASIFUKUZWE NA WAO KAMA MBW`? NA ATAKAE OVERSTAY ,APIGWE LIFE DEPORTATION. MIMI UKWELI NINAHASIRA NAO SIO SIRI.
ReplyDeleteZITOO
ReplyDeleteleo nimekubaliana na hoja zako kabisa,ila juzi ulionghea utumbo juu ya suala la muungano,big up,leo sina maneno umemamiliza kila kitu.
Tatizo la nchi hii ni URAIA na kukosa ELIMU.
ReplyDeleteNimegundua wengi wa wachangiaji wanaohimiza mfarakano wa nchi yetu aidha sio raia kwa asili au hawaijui hitoria ya TZA na watu wake.
Watza wakumbuke, watu wa pwani wana uhusiano wa karibu zaidi kijografia, utamaduni, lugha na historia na W'z'bari kuliko hata ilivyo kwa mikoa ya bara.
Vile vile; nyanda za juu kusini; Mbeya, Iringa, Rukwa nk. wana ukaribu sana na Wakongo wazambia nk.
Tukija kanda ya ziwa kumejaa Waganda, wanyarwanda, na warundi.
Kanda ya kaskazini kumejaa wakenya na wasomali.
Kwa hivyo watz. wakumbuke wanapohimiza kuvunjika kwa muungano ili wapemba waende, wakati wao wanawapa uraia jamaa zao wa kirundi, kinyarwana na kufuga majamazi wa kikenya na kisomali kule kaskazini hatutawaelewa!!
nchi ya scotland ndani ya the united kingdom of great britain pia ina hodhi rasilimali ya mafuta.
ReplyDeletewatanzania tusiwe wavivu wa kufikiri, jambo analoongea mh. zitto linaweza kujadiliwa bila jazba kua lipo nje ya makubaliano ya muungano.
hivyo mafuta yanayogundulika zanzibar au tanganyika yafaa huhodhiwa na nchi husika ktk muungano.
mwisho wa siku mjadala uwe ni kiasi gani kutoka kila nchi ichangie ili kuendesha shughuli za ulinzi, usalama n.k shughuli ambazo ni za muungano.
mdau
stone town.
Mbona mtu akiwa muislamu akichangia jambo linalo wagusa waislamu wakristo husema wewe kwa kuwa ni muislamu ndiyo maana unawatetea waislamu wenzako,hata kama kuna ukweli ndani yake.Kwa mtindo huu tutafika kweli,manake inaonekana mtu achambui mada anaangalia dini ya mtu tu na siyo ukweli wa jambo.Nafikiri Watanzania tubadirike kama kweli tunataka kuleta maendeleo katika nchi yetu,la sivyo tutaendelea kuwa vibaraka/manamba wa wakoloni bila ya sisi wenyewe kujijua.
ReplyDeleteZITO ENDELEA KUWASOMESHA!!!
ReplyDeleteSISI TUNASISITIZA, HATUWEZI KUVUNJA MUUNGANO WALA KUGAWA NCHI KWASABABU YA WAHUNI WACHECHE!
ZANZIBAR KUNA AL SHABAB na HUKU TUNAO 'LOARD RESISTSNCE ARMY' WASKILIZIA TU!
Mh Zitto, vizuri ulipo wajulisha kitu kilicho na ukweli na uhalisi wake.watanganyika wengine wana agizo la kanisa akisema Muislam hata jambo njema hulipinga,hio ndio sera yao
ReplyDeleteHawana busara watu wa aina hio,huwa vichwa vitupu hoja zao kama vitoto vya njiani.kila wazo la wenzao au haki ya wengine wao huwauma katika nyoyo zao.Niwepesi kupinga haki za jamii moja kama walivopinga O.I.C na Mahakama ya Kadhi.
ukiwashinda kwa hoja husingizia ukabila na iman ya mtu,hawana upeo wa kuishi kijamii.
Huu sio wakati wa kuwadanganya watoto wenu tena kwamba ukicheza na muisilamu atakupandisha majin.kuweni na hoja za kujibu.na hao L.R.A ni ushahidi wa uwongozi wenu.
Walipeni pia wasukuma kwa kufanya dhahabu yao mali ya muungano.
ReplyDeleteJibu la yote hayo ni ujio wa katba mpya Wazanziri tunaangalia mambo upya ndio maana hivi sasa tunnapiga kelele TUNATAKA TUULIZWE KAMA MUUNGANO TUNAUTAKA kama hatukuulizwa hiyo katiba mpya tutaikataa katika KURA YA MAONI. Ili kujenga misingi madhubuti ya ukweli ni lazima watu waulizwe,hakuna ubishi kwamba muungano wetu wananchi hawkushirikishwa ndio maana kila kitu kinachofanywa nchi hii watawala hawataki kuulizwa wala kukosolewa.
ReplyDeleteLa muhimu ni watanzania pande zote mbili za muungano kujiuliza ni ushirikiano wa aina gani na katika lipi unahitajika ili kuboresha tija kwa pande zote za muuungano na makubaliono yakifikiwa basi hilo liendelezwe.
ReplyDeleteUkweli ni kwamba Zanzibar wakibakia na miliki ya taifa lao na Tanganyika pia wakabakia na miliki ya taifa lao mahusiano pande zote mbili yatakuwa mazuri zaidi na yenye tija kwa pande zote. Hivyo Wazanzibar wabakie na raslimali zao na bara na zao.
Mgogoro unaonukia udini uliotoke Zanzibar hivi karibuni umewahi kutokea pengi duniani ampapo waislamu ni wengi kuliko madhehebu mengine. Kuepusha hayo kurudia ni madhehebu mengine kujiondoa katika mataifa kama hayo.
Haina haja wakristu kujipeleka huko ukristu, pombe na nyama yanguruwe havikubaliki.