Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 13, 2012

    Ooh my God, hawa wazazi wanaweza kushtakiwa maana hii ni sehemu ya abuse kwa watoto

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 13, 2012

    Who could do something like that to their baby? If U are busy in SHAMBA or anywhere how about laying the baby on the ground? That's totally inhuman and unacceptable.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 13, 2012

    Huyu mama mwambie asirudie tena kufanya neno hili, maana tutamfunga sasa, kwanini anafanya hivi, huyo mtoto alilazimishwa kumzaa au ni nini hiki?
    NOBODY IS HAPPY WITH THAT.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 13, 2012

    huu ni unyanyasaji wa watoto. Nalaani kitendo hiki.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 13, 2012

    Huu ni unyanyasaji. Kama huyo mlezi alishindwa kumbeba mwenyewe si angemlaza mahali?

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 13, 2012

    Hongera sana mama mzazi. Chini huwa kuna pita nyoka , nge na wadudu wengi ambao wanaweza kumdhuru mtoto. hapa mama katumia busara ya kuzaliwa siyo ya shuleni, hapa mama yuko na jembe lake anaendelea na parizi,mtoto kawekwa ghorofani salama salimini. Obeja mayu. Zebedayo.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 13, 2012

    Huu ni utesaji wa watoto, huyu mtoto anaumia hapo na pia kuna uwezekano wa kuwepo na wadudu ambao wanaweza kumshambulia huyu mtoto. Inasikitisha na tunapaswa kuwahurumia watoto.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 13, 2012

    Mama wa huyo mtoto ashtakiwe manake Huu ni unyama kwa kweli africa kupata msaada wa kulea ni kibao.

    wako watu wanatafuta watoto hata wa kusingiziwa ila hawapati mwenzetu kapata ila ndio hivyo tena anamweka alelewe na mti mstzzzz

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 13, 2012

    watu wengi wanapiga kelele juu na kusema kuwa huo ni unyanyasaji wa mtoto, ambao kwa kwa kiasi fulani wako sawa kusema hivyo. Hata hivyo nyoote mnasahau kujiuliza ni sababu gani na kwa mazingira gani aliyonayo mama mzazi hadi kufika kumuweka mwanawe hapo? tatizo halianzii hapo kwa mzazi bali ni jamii nzima kwa kuruhusu wachache kuendelea kujinufaisha binafsi na kuwaacha wengi wetu tukiwa masikini wa kutupwa. Miaka arubaini na ushee ya tanzania na mkulima anashindwa kumpatia mwanawe matunzo bora wakati akiwa shambani!!! inauma sana!!!

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 13, 2012

    mtoto mwenyewe kalala usingizi, ila minazi ina wadudu wanatambaa, hata nyoka anatambaa kwenye mnazi. Ila Mama hafanyi kitu kama hiki, bila ya kufanya uchunguzi kwanza. Hebu huko nyuma angalieni kuna ukuta wa matofali, hapo shamba gani?. Basi mnapayuka tu, use your grey matter.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 13, 2012

    KAMA ULISHAWAHI KUONA CHATU KAMEZA MTU HUSUSAN WATOTO SHAMBANI HUWEZU KUMLAANI MAMA HUYU NA BUSARA ZAKE. KUMBUKA AFRICA SIO ULAYA HAKUnA BABY SITTER MAENEO hayo YA VIJIJINI. NI MIMI KAKA YENU WA ULAYA LAKINI BADO NAKUMBUKA HALI HALISI YA MAMA SHAMBANI,MTOTO MTINI, NA HUKU BABA KILABUNI NA ULABU WAKE. we have a long way to go, Mafisadi mtuonee huruma tuondoe umaskini na juboresha akili kwenye shule bora

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 13, 2012

    Hivi kuti la mnazi ama nazi ikimdondokea huyu mtoto, huyo aliyemweka mtoto hapo atasema bahati mbaya? Nafikiri huyo mtu anahitaji elimu ya kujua hatari na madhara yake ili wakati mwingine asifanye tena

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 13, 2012

    Ni hatari sana sana fikiria vidaka na nazi zinazoanguka toka kwenye mnazi zikimgonga kichwani,achilia hilo kuna nyoka wengi tu huwa wanapanda na kushuka toka mnazi wakati wowote hapo itakuwaje??ni hatari sana ingawa labda mazingira aliyopo ndio angalau safe kidogo!!duu malezi kwa usalama ni jambo gumu kidogo vijijini!!!

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 13, 2012

    hiki ni kielezo halisi cha maisha yamtanzania wa kawaida, katika hali kama hii katika nchi zilizoendelea angewekea matoy na vibembea huku mzazi akiendelea na kazi zake, mzazi anastahili pongezi kwa ubunifu wake badala ya kuanza kumlaumu

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 13, 2012

    Wajameni, sasa NAZI ikimuangukia kichwani huyu mtoto si itakuwa balaa, but I thibk the maza did with with love and not otherwise.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 13, 2012

    Hatuwezi kuzungumza sana kwa sababu hatujui mama yuko wapi au amepatwa na nini inawezekana yeye yuko ktk hali mbaya zaidi tuache kukurupuka

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 13, 2012

    Hongera Mama. hapa hakuna nge wala siafu wala wadudi watmbaao ardhini.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 14, 2012

    MAzoezi ya kupanda daladala yanaanzia mbali. Ni mwendo wa kuning'inia mlangoni huo ATAKAPO KUWA MKUBWA . Huyu mama anajua shida ya usafiri itakayo mkumba mwanae mbele ya safari. Nchi itakuwa hivyo hivyo kama ilivyo HIVI sasa PINDI mtoTO huyu ataKAPO kuwa na umri wa miaka 50. Shame on our infrastructure mikakati. MAFISADI ZIIIIIIIIIIIIII. ccm hoyeee....Chadema hoyeee..ni walewale tu.

    MZEE WA BUSARA.

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 15, 2012

    Wazazi wawili hapa Baba na Mama inatakiwa wakamatwe mara moja,,,

    Hii sio sawa ni ukiukwaji mkubwa wa haki za kibinaadamu, kwa sababu mtoto ni haki yake kuwa chini ya ungalizi wa mzazi mmojawapo au wote kwa pamoja kila dakika!

    Haiwezekani mtoto afungwe hivi peke yake,

    1.Je pakitokea mdudu mfano nyoka huku mtoto yupo peke yake itakuwaje?,

    2.Je mzazi aliyemweka hapo pasi na mzazi mwenzie kujua mtoto alipo, mzazi aliyemweka mtoto hapo akipata dharura labda ameanguka sehemu anaumwa, au amekamatwa na Polisi au ametekwa na watu wengine akapelekwa kwingineko, au ameenda sehemu akalewa akapitiwa na kukumbuka mtoto alimwacha peke yake ,je itakuwaje?

    Usimamizi wa mtoto muda wote kila sekunde inatakiwa awe chini ya uangalizi wa mlezi, mzazi au wazazi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...