Kwako Anko Michuzi,

Ni wakati muafaka kumuunga mkono Mheshimiwa Zitto Kabwe na Ndugu John Mashaka. Nimefurahishwa sana kuona wote wawili wametumia wakati wao kutoa hoja zao kwa hili. Ni muhimu kujadili hasa wakati huu ambapo katiba yetu inaangaliwa upya. Kwangu mimi wote wapo sahihi. Maoni safi na muda muafaka. Kila mtanzania ana haki kujadili linaloihusu nchi yake hii ni haki ya kikatiba.

Huu ni muda muafaka kwa wananchi wa bara na visiwani kuuliza maswali ya msingi kuhusu muungano. 

Huu ni muungano wa wananchi mamilioni wakiwemo wafanyakazi,wakulima,wavuvi,wafanyabishara,wanataaluma,waandishi wa habari, wanablogu,wanafunzi,viongozi wa dini, waumini wa dini zote, waishio Tanzania na walioko nje.n.k. 

 Ni muhimu basi hoja zote ziwekwe mezani na kujadiliwa. Ni wananchi wenye nchi yao waamue je muungano uweje? Mimi ni miongoni mwa wale wanaounga mkono muungano au 'unionists'. Siamini huu ni wakati wa utengano, dunia inazidi kuwa kijiji na umoja siku zote ni nguvu na utengano ni udhaifu. 

Mfano mzuri wa umoja ni East Africa Community - ilikufa sasa imeanzishwa upya kulingana na matakwa ya nchi ya sasa. Kuna mambo mengi ulimwenguni ya kiuchumi, kisiasa, kiulinzi na kibiashara ambayo yanahitaji umoja kupambana nayo.

Nionavyo mimi muhimu ni kwanza - Uwazi katika muungano, wananchi wajue wanaungana vipi na kwa nini na kwa faida ya nani kusiwe na siri katika sababu za muungano au jinsi ya kuungana. Wananchi wasikilizwe. Isiwe muungano unatumiwa na wanasiasa kujipatia kura kwa kuwagawa wananchi. 

Wakishachaguliwa wanaongelea kuongezewa posho yao na sio hali ya maisha ya waliowachagua. Matatizo mengi Tanzania yanatatulika, tatizo ni wanaogushwa ni wanyonge.

Pili muungano uwe flexible kulingana na mazingira yaliyopo wananchi wawe na uwezo wa kubadilisha makubaliano ya muungano kila baada ya miaka kadhaa [ kwa mfano kila miaka kumi muungano ufanyiwe review kuona kama unalipa kwa terms zilizopo au ubadilishwe kwa kuongeza au kupunguza vipengele].

Tatu kuwe na kipengele kwenye katiba ya Jamhuri wa muungano kisemacho kukiwa na kutokukubaliana kati ya bara na visiwani katika jambo lolote la muungano swala hili lipelekewe wananchi waamue kwa njia ya referendum.

Namna hii basi wananchi wenyewe wataumiliki muungano na sio wanasiasa ambao wengi wao wana hoja za msimu na kura.

Ningependa kuwaasa watanzania kutumia fursa hii kuboresha muungano na kuwahoji wanasiasa wanaoleta siasa za ubaguzi. Tukumbuke Dhambi ya ubaguzi haiishi. Tutaanza na watanganyika na wazanzibara halafu tutaendelea mwisho wake utakuwa nini?

Tanzania ni miongoni mwa nchi chahe Afrika zenye amani na utulivu. Watu wake ni makabila mbalimbali, wanaamini dini tofauti, wote wameungana pamoja wakiongea lugha moja. Tujivunie hilo na kulidumisha. Sasa hivi kila pande ya dunia mambo si mazuri mifano ya Afrika peke yake ni chungu nzima. 

Kwa mtizamo wangu wanasiasa wangeelekeza nguvu zao kuinua maisha ya watanzania kwa kutumia rasili mali za nchi badala ya kuleta siasa za utengano.Ufikie wakati tuwahoji wanasiasa wamefanya nini sio wanatoka chama gani? 

Tuifanye serikali iwe accountable to the people. Viongozi wajue wananchi tupo macho. Muda wa kudanganyana kutumia ubaguzi, utengano na ubabaishaji umekwisha.
Rasilimali za nchi hii zitumike kupambana na maadui wa nchi hii. Mungu ibariki Tanzania na watu wake.

Asante
Mdau

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 28, 2012

    Umenenan vizuri bila kupinda pinda.Wananchi kila jambo uwazi uwepo,siyo kusema hili ni la siri. Siri ni ya nani wakati kila mwananchi anaweza siku yeyote anaweza katika hicho kiti.Tukiwa wawazi nchi itapaa mara moja kiuchumi.Hafu watu waache tabia ya kuona upande mmoja umesema jamabo fulani eti kwa sababu yeye ni muislamu.Manake ndugu zetu wakristo muislamu akisema jambo na akiona lile jambo linawagusa waisilamu wanasema huyu kwa kuwa ni muislamu.Kwa mfano swala la Zito Kabwe kuhusu mafuta na gesi ya Zanzibar na Tanganyika.Inabidi tuwe tunachambua mambo na kujua uhalisia wake,tusikurupuke.Tujibu kwa kutumia hoja.Kwa namna hiyo tutapiga hatua kwenye nchi kama hatuna akili nzuri.Kila la kheri.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 28, 2012

    huyu jamaa kaongea maneno anbayo sio mabaya ila watu wamechoka,mimi siishi bongo lakini kila nikirudi kutembea maisha yanazidi kua magumu,na watu wengine hasa hawa wanasiasa serikalini wanaishi maisha laini,yaani kiswahili husema kula na kipofu no wamejisahau kabisa,hili pira litafika mpaka bara subiri.

    ReplyDelete
  3. Che GuavaraMay 28, 2012

    Dr. shayo asante kwa mchango wako japo hukataka kuweka jina lako kamili.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 28, 2012

    Hakuna sababu ya kulazimisha ndoa,

    Hao Wazanzibari waende zao kwao na Wabara waliopo huko Zenji warudi huku Bara.

    KTK DUNIA HII YENYE HEKA HEKA KWA MATATIZO NYETI KAMA MASUALA YA KUFILISIKA KIUCHUMI NA KIFEDHA YALIYOPO, HAKUNA KITU KIGUMU KAMA KUMBEMBELEZA MTU KWA SUALA AMBALO YEYE MUHUSIKA ANANUFAIKA NALO (MUUNGANO)

    HII KITU '''MUUNGANO''' BARA INAPATA HASARA SANA KWA KUIBEBA ZANZIBARI.

    KWA NINI KUNDI LA UAMSHO WASITUMIE BUSARA NA TARATIBU ILI KUFIKIA AZMA KWA NJIA SAHIHI NA BADALA YAKE KUTUMIA NJIA YA KIHUNI?

    1.YUPO KIONGOZI WA DINI KADHI ZANZIBAR KWA NINI WASIANZIE HAPO?

    2.YUPO MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD KIONGOZI AMBAYE YEMO SERIKALINI KWA NINI WASIANZIE KWAKE?

    3.KULIKUWA NA UGUMU GANI WA KUTUMIA SHERIA NA TARATIBU KWA KUOMBA KIBALIA CHA MAANDAMANO KABLA?

    NI KUWA WAZENJI NI GOI GOI, WANATAKA KUTUMIA MGONGO WA DINI KULETA MACHAFUKO, PIA NA WANADEKA SANA WANATAKA KILA MMOJA APEWE HUDUMA ZOTE ZA MAISHA (KULA, KULALA NA KUVAA) NA SERIKALI !, KITU AMBACHO HATA SERIKALI YA MAREKANI HAIWEZI!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 28, 2012

    Haja zako zinaonesha kuwa na mawazo ya kibusara,lakini hapo hapo unaweka kibwakizo chako katika njia panda,nasema hivi kwa kuona hukufanya kupinga muungano ila uwe wa kukubalika na watu wa nchi hizo zilizoungana.

    Mimi sina haja ya kukukosowa najuwa wazi kuwa maneno yako ulosema ni yakuimarisha jamii njema na utu wa binaadamu katika nashirikiano.
    Lakini suala la muungano huu upo tafauti na hio ulofananisha,kama E.A.C ni shirikisho hakuna nchi ilopoteza uraia wake wala kiti U.N.Ndio kusema tunahitaji muungano wa kila taifa liwe na dola kamili kama ilovo hizo nchi ulofananisha.

    Ikiwa utawala ni mtamu hata mwezio anauhitaji na yy isiwe hadiriki kuonja kitamu hio itakuwa ni zulma na ukandamizaji.kwa upande mwengine.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 28, 2012

    Swala kwamba muungano uendelee kuwapo au usiwapo lazima litokane na wananchi wenyewe pamoja na viongozi kuzijua faida na hasara za muungano.

    Wzanzibar ni wavivu na goigoi wengi wao, wana ardhi yenye rutuba hawalimi vyakutosha na nyumba zao za tembe juu wameweka dishi aliloletwa na amy.

    Wanamtazamo hasi, ambao sisi wabara lazima tujiepushe nao,UDINI. Kwanza wanadhania kuwa wabara wote ni wakristo. Kelele zote kwamba muungano uwepo au usiwepo, zinapigwa na wao na sio wabara. Wabara wanapoongelea muungano ni hasa baada ya kuchoshwa na huyu kupe asiyebebeka.

    Swali ambalo tunatakiwa kujiuliza, nani anafaidika na muungano, wazanzibar, wabara au VIONGOZI?

    Jamani, neno udini lisitutenganishe, kwani wewe unachokiabudu kinaathiri nini maisha yangu ya dini ingine, pili tumeshaona dini zote na wasio na dini. Tuelewe kitu kimoja, wazanzibar huwa ni wabaguzi, hata mkiwa nje ya nchi wao hujitenga ktka makundi yao.

    Kibanga Msese

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 28, 2012

    Hao jamaa wa UAMSHO waliokamatwa huko Zenji waletwe kuja kuswekwa LUPANGO za Bara kwa vile huko kwao hakuna Magereza kuna Vyuo vya Mafunzo!

    Hawa waje waone ya kuwa inafikia mtu anaenda haja kubwa na ndogo kwenye Ndoo ama Debe!

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 28, 2012

    Mchangiaji wa mwisho,akili zako nadhani zimeingia mafuta ya taa! Hapa hatutafuti mchawi nani. Hapa tunajaribu kutafuta dawa ya 'ugonjwa' huu sugu. Ili hata kama muungano utavunjika basi watu waendelee kuishi kwa usalama na amani na kwa undugu,kama walivyokuwa wakiishi kabla ya muungano.

    Lakini hata pande zote mbili zikiamua kuwa na muungano,basi ziwe na muungano uliokuwa wazi na wenye manufaa kwa pande zote mbili,bila ya upande mmoja kuukandamiza mwengine kwa kisingizio cha wingi wa idadi ya watu, ukubwa wa eneo n.k

    Naomba nimpongeze sana ,Mwandishi wa makala haya. Hawa ndio watu tunaowahitaji kwa sasa.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 28, 2012

    MIMI NAANZA KUWA NA WASIWASI KUWEPO KWAKE HUYU MASHAKA. MADA ZOTE NZURI HUMU IWE NI MASHAKA. LUGHA STAHIKI NI MASHAKA, BUSARA NI MASHAKA UJINIUS NI MASHAKA ALAFU WATU WANAMFUATA KAMA VIPOFU. TANGU BLOG YA MICHUZI IANZISHWE, MADA YOYOTE ANAYOTOA MASHAKA INACHANGIWA NA WATU UTAFIKIRI WAMECHANGANYIKIWA KOMENTS 100 KIDOGO. HAKUNA KITU KINGINE CHOCHOTE KILE KINACHOCHANGIWA HUMU KAMA MADA ZA MASHAKA. NA HII INANNIPA WASIWASI KUAMINI KWAMBA MASHAKA NI UBUNIFU WA MICHUZI MWENYEWE KUCHANGAMSHA GENGE NA KUVUTIA WASOMAJI ZAIDI KWENYE BLOG YAKE. MASHAKA NI MTU FEKI ALOTENGENEZA MICHUZI KUCHOKONOA HISIA ZA WATU KUHUSU MADA TOFAUTI. MASHAKA NI MTU MWNEYE KIPAJI CHA KIPEKEE, WENGINE WAMUITE GINIAS, WENGINE NABII, WENGINE WAMUONE KAMA MKOMBOZI, MAKINI, MWENYE BUSARA MKARIMU LAKINI HAKUNA MTU AMBAYE WAMEWAHI KUMUONA. MASHAKA KAJENGEWA UMAARUFU MKUBWA BILA YEYE KUJITOKEZA MBELE YA JAMII IWEJE HUYU7 MTU MMOJA NDO HAWE GUMZO KILA SEHEMU NA HAKUNA HATA MTU MMOJA AMBAYE AMEWAHI KUMUONA. NINA WASIWASI NA MICHUZI. HAKUNA MTU MMOJA ANAYEWEZA KUWA NA AKILI NYINGI HIVI ZA KUWEZA KUGUSA WATU. HUYU MASHAKA NI MICHUZI NA WAANDISHI WENZAKE HUKO DAILY NEWS. YETU MACHO TUNASUBIRI SIKU MICHUZI ATAKAPOFUNGUAK NA KUKIRI KWAMBA YEYE MWENYEWE NDIYE YOHANA MASHAKA. THRE IS NOTHING LIKE MASHAKA I SAID IT. MASHAKA NI JIN LILILOTENGENEZWA NA WANA USALAMA KUKUSANYA MAONI YA RAIA KUHUSU MASWALA MAZITO HUMU NCHINI MSITUCHEZEE AKILI. NO HUMAN BEING CAN BE THAT SMART. MNATUCHEFUA

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 28, 2012

    Ndugu mtuma mada sinabudi kukupongeza, ila suala la Muungano ni maridhiano na sisi huku visiwani inaonyesha walio na sauti hawataki na wanaotaka kwa kukaa kimya inadhibitisha kuridhiya hawo wasio taka. Kama leo ndugu zetu wamefika kutamka wazi wazi na kudiriki hata kuhatarisha maisha ya raia wasio na hatia kwa kulipuwa nyumba za ibada na kuchoma moto basi tuwaulize wale wa Zenji walio Kariakoo hadi Mwanza jee wanaonaje hili. Serikali ya Zanzibar imeshindwa nguvu za kuhimili hii hali naona sasa ni jukumu la viongozi wa Muungano kulishuhulikia kwa maisha ya raia na usalama wao ni jukumu la Serikali. Ikibidi tugawane vipande na kila mtu arudi kwao masaa ishirini na nne.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 28, 2012

    asante sana mdau kwa mada na uchambuzi wako mzuri. huu mjadala umetupa picha kamili jinsi zitto kwabwe alivyomchanga kwenye maswala mazitto ameonge amengi mara mafuta, mara uongozi, mara serikali tatu, mara mwalimu wake wa lugha lakini mwisho wa siku kaangushwa chali na nguli john mashaka. kwa hakika hatuweza kuwafananisha mashaka na zitto. na kamwe zitto hatoweza kuendelea na majigambo yake ya kujiona yeye ndo yeye. dawa yake imepatikana mwaka huu wa 2012

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 28, 2012

    Maoni safi. Tatizo hii hali ya kuonyesha upande fulani unalzimisha muungano ndio tatizo. Muundo wa muungano ni tatizo lisilo siri tena. Tumekosa viongozi wenye ujasiri kufanya maamuzi. Inapelekea vikundi vichache venye nia mbaya ku hijack tatizo hili kwa interest zao. Ndugu zangu wa bara, huu si muda wa kuwatelekeza ndugu zetu wa zanzibara. They need us more than anytime....siamini hii jumuia inawakilisha maoni ya wazanzibar wote! Referendum huru pekee italeta suluhu na utaendelea pamoja, iwe kama tanzania au ndani ya jumuia ya afrika mashariki.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 28, 2012

    Ndugu yangu uliyetoa maoni hapo acha Jazba mimi ni Mtanganyika halisi nina hasira na hao wazanzibar pengine zaidi yako lakini kwa Wa-zanzibar kutoka kwenye muungano soi sababu ya wao kufukuzwa Tanganyika, wanaweza kutoka kwenye muungano na wakaendelea kuishi Tanganyika kama kawaida kwa sababu bado watakuwa kwenye East Africa, mbona kuna Wachina, wakenya na watu kutoka mataifa mbalimbali wanaishi Tanganyika kwani tuna Muungano nao? Iweje leo Wa-zanzibar wakitoka kwenye muungano wafukuzwe na sisi wa-Tanganyika tufukuzwe kwao, nimekusamehe hayo yote yanakutoka kwa jazba au pengine upo shallow katika hili.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 28, 2012

    tatizo la Zitto ni elimu duni. Hawa wanasiasa wetu have very minimal training. wanapoweza kuandika vi atiko uchwara na kuweza kubwabwaja bungeni wanajiona wao ndio wao. hapa zitto kachemsha kwa kuropoka bila kutafakari mambo mengi na ndio maana wengi wamemuunga mkono mashaka kutokana na umakini wake wa kutumia maneno yenye busara. ni hayo tu na watu kama zitto wanaweza kuwa hatari kwa amani ya taifa kutokana na uropokaji wao. mbaya zaidi zitto anajiona kana kwamba hakuna mtanzania mwingine mwenye uwezo wa kuchambua mambo kama yeye. this is too bad for him kwa maana wengi wameshatambua kiboko yake ni jonh mashaka

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 28, 2012

    Mi sioni chochote cha muhimu kilichoandikwa,cha msingi mi nauliza watanzania wote,Je Muungano upo katika somo gani Tanzania,na lini tulielimishwa faida za Muungano na katika elimu gani?ukiwachia exam question ya lini Tanganyika na Zanzibar iliungana.

    Pili Watanzania kwa upande wa Bara wana mawazo finyu sana,wanafikiri kuvunjika kwa Muungano ni uhasama,na vita ndio maana mtoa maoni mmoja amesema ati wabara warudi kwao wapemba waende kwao,si yeye tu bali watanganyika wengi wana mawazo hayo,Tatu Muungano tuungane tu lakini kila mtu awe na nchi yake,Scotland wanajiandaa kujitoa na UK,EU yote sasa imeshaanza kuathirika kwa matatizo hayo hayo,Umoja ni nguvu ni sera za CCM,"The strongest man in the world is the one who lives alone" An enemy of the people kumbukeni hapo.Na mdau unosema mnaibeba Zanzibar kwannini tna mnajibebesha mizigo msioweza? waachieni wenyewe Zanzibar wajibebe! watu wamechoka na wasiotaka mabadiliko ni wapumbavu.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 29, 2012

    Waafrica achana na mental slavery. Tumieni nguvu zenu kwenye elimu,afya na ustawii wako kijumla. Ni kero kupoteza muda kuanza kutafarakana wakati maendeleo ni duni. Songa mbele tusirudi nyuma. Boresha muungano sio utengano. Tamaa za vyeo ndio zitatupeleka pabaya. Leteni uamsho kuwa elimu iboreshwe,huduma za afya na jamii pia.

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 29, 2012

    Kipengele cha pili cha muandishi na muda alioutoa (miaka 10) ndio aliouweka Marehemu Mzee Karume wakati wa kuungana, lakini kwa bahati mbaya yeye mwenywe hakuwa hai na wala walifuata hawakuweza kufuatilia maagizo haya.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 29, 2012

    Acheni kuondoka kwenye mada jamani. Ivi kweli ni haki kuupinga undugu wetu badala ya kuupinga umaskini? Iweje leo hii tuanze usisi na uwao kweli? Badala ya kulaumu viongozi hawatoi maelekezo jinsi ya kupambana na umaskini tunaanza kugombana wenyewe kwa wenyewe. Mhh ama kweli kua uyaone.

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 29, 2012

    Zanzibaris have a right to have their state/country. The slogan 'tunataka nchi yetu' is very clear. However can we identify the problem in the status quo before we move to the next step? Is this the majority view? When I wrote my opinion above I did not intend to make decisions for millions of people in Zanzibar and Pemba. My intention was to air my contribution/opinion to this important discussion. I must say I have much respect for the Zanzibaris and I do not question their potential. I studied, lived and worked with Zanzibaris and they are generous, kind and hardworking, no question about that. I know Zanzibar has a lot of distinguished personalities, can we please hear their views.

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 29, 2012

    michuzi comment yangu umebania no problem mkuu ni blog yako waweke vichogo wenzio tuu na utuone sisi hatujui kuchangia madaa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...