Na Mary Gwera-Mahakama ya Rufani (T)
JAJI wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania, Mhe. Jaji Eusebia Munuo ameteuliwa kuwa Rais wa Chama cha Majaji Wanawake Duniani, imebainika.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Dar es Salaam jana Munuo alisema kuwa uteuzi huo umefanyika mnamo tarehe 06.Mei mwaka huu katika Mkutano Mkuu wa Majaji Wanawake Duniani uliofanyika nchini Uingereza hivi karibuni.
“Nafasi hii ya Urais wa Chama cha Majaji Wanawake Duniani (IAWJ) nimeipata kufuatia aliyekuwa Rais wa Chama hiki kutoka Uingereza kumaliza muda wake, na tumekabidhiwa rasmi bendera ya Chama katika mkutano uliofanyika hivi karibuni nchini Uingereza,”alisema Jaji Munuo.
Aliongeza kuwa nafasi hii ataishikilia mpaka tarehe 9. Mei ya mwaka 2014 ambapo uchaguzi mwingine utafanyika na kumpata Rais kutoka nchi nyingine.
Hata hivyo alibainisha kuwa mkutano mwingine wa Chama hiki unatarajiwa kufanyika nchini katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa jijini Arusha mnamo kuanzia Mei 6-9 mwaka 2014 ambapo kiti hiki cha urais kitakabidhiwa kwa nchi nyingine.
Jaji Munuo ameahidi kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuendeleza na kupigania maslahi ya Majaji Wanawake na wanawake duniani.
Kwa upande wake, Jaji wa Mahakama ya Rufani (T), Mhe. Engella Kileo alibainisha kuwa uteuzi wa Mhe. Munuo umeleta faraja hasa kwa Majaji na Mahakimu wa nchi hii na hivyo kuahidi kushirikiana nae katika kufanikisha upatikanaji wa haki kwa usawa.
“Uteuzi wa Mhe. Munuo umefuatiwa na utendaji kazi wake pamoja na ushiriki wake ulio imara katika mikutano hii ambayo hufanyika nchi mbalimbali na hatimaye kupelekea wasifu wake kufahamika kwa wanachambalimbali wa chama hicho,” alisema Jaji Kileo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (JMAT).
Jaji Munuo alianza kazi rasmi mwaka 1970 kama Hakimu Mkazi wa kwanza mwanamke, na hivi sasa ni mmoja kati ya Majaji watano wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania.
Way to go Jaji Munuo! Hongera sana kwa kukabidhiwa jukumu kubwa la kimataifa.
ReplyDeleteTunaomba uwaonyeshe kwamba Watz wanaweza. Tuna imani kwamba umepewa kutokana na kuonekana kwamba unaweza.
Mungu akusaidie katika kutekeleza majukumu yako mapya.
Hongera sana Mama Munuo.
ReplyDeleteCongrats Mama.
ReplyDeleteHongera mama wa kichaga, Matunda ya URU hayoooo!!
ReplyDeletehaya sasa wakaskazini/wachaga mnawapiga vita hapa nyumbani sasa wanapeta nje ya nchi.
ReplyDeleteHongera Sana mama
ReplyDeleteNi faraja kwetu tunaowapenda na kuwajali wanawake na mabinti zetu.
nikuombe mama kama utapata nafasi uwatembelee mabinti zetu kule shuleni uwatonye siri za mafanikio ya mwanamke wa kiafrika kama wewe yaani kuanzia kwako, kwao na kwa watoto wao! Hawatakusahau milele,
Im proud of you madam
May God bless you
Hongera sana mama. Mungu akupe nguvu ukasimame imara na kuwa ushuhuda kwa wengine.
ReplyDelete--MD
ndio hao hao wanapeta ndani na nje ya nchi baada ya kuimaliza nchi.
ReplyDeletewewe anon (Fri May 11, 01:13:00 PM 2012) fanya kazi acha kulalama nchi za watu hamna short cuts ni kichwa chako tu/utendaji wako. Hamna cha majina wala nini so obviously mama Munuo deserve the post. Tukaze mwendo jamani sio kila kitu ni politics na malalamishi. Dunia inasogea fasta inabidi na sisi tuende nayo.
ReplyDelete