Jamaa huyu ambaye alikuwa ameegesha gari pembezoni mwa barabara maeneo ya Masika,Mjini Morogoro akifunga chuma kwenye tairi la gari lake (ambalo alishuka nalo kutoka garini) ili aweze kufanya faulo ya kuliacha gari hilo katika eneo hilo ambalo haliruhusiwi kuegesha magari na kwenda kufanya shunguki zake.Tukio hili limetokea mchana huu Mjini Morogoro.
 Jamaa akiendelea na jukumu lake la kupiga pini tairi la Gari lake (halafu anaonekana ni mtaalamu kwenye kazi hii).
 alipomaliza akanyanyuka na kuendelea na mambo yake.
 Chuma lishakaaa...
Na kibao cha kuzuia kinaonekana kwa mbele pale.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 05, 2012

    ANKAL NIMEKUWA NIKIITUMIA HIYO MBINU KWA MIAKA MITATU SASA JIJINI DAR ES SALAAM (NA SIPO PEKE YANGU) NA INAFANYA KAZI VIZURI SANA KWANI WANAPOFIKA MGAMBO WAKIKUTA HICHO CHUMA WANAJUA TAYARI WENZAO WAMESHALIFANYIA KAZI.HIVYO INANIWEZESHA KUPAKI POPOTE NA KUFANYA SHUGHULIZANGU HADI NINAPOAMUA KUTOKA MAHALI HAPO.KUISHI MJINI FORM SIX TUMEAMUA KUWA WABUNIFU KAMA WAINGIZA VIRUS KWENYE MITANDAO.

    ReplyDelete
  2. Duuuh, kweli mjini shule. Hakika imetulia hiyo

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 05, 2012

    Dawa ni kumuengezea pini nyengine tu. Mgamo kazi kwenu, mambo hadharani.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 05, 2012

    Kweli "Fakhari MAMA wa ujinga". Unaiba, halafu unakwenda kujisifia kwa raia, hujuwi miongoni mwao mna hao mgambo, polisi na vyombo husika. Hetu fikiri na tafakari kabla hujaamuwa kusema au kutenda jambo.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 06, 2012

    we mdau wa kwanza huna akili,huo sio ujanja ni upuuzi.

    ReplyDelete
  6. Nyinyi mnaojisifu kwa maovu ndio mnaotusababishia msongamano wa mafoleni,fateni sheria bila shurti,usitete maovu yako.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...