Jamaa huyu ambaye alikuwa ameegesha gari pembezoni mwa barabara maeneo ya Masika,Mjini Morogoro akifunga chuma kwenye tairi la gari lake (ambalo alishuka nalo kutoka garini) ili aweze kufanya faulo ya kuliacha gari hilo katika eneo hilo ambalo haliruhusiwi kuegesha magari na kwenda kufanya shunguki zake.Tukio hili limetokea mchana huu Mjini Morogoro.
Jamaa akiendelea na jukumu lake la kupiga pini tairi la Gari lake (halafu anaonekana ni mtaalamu kwenye kazi hii).
alipomaliza akanyanyuka na kuendelea na mambo yake.
Chuma lishakaaa...
Na kibao cha kuzuia kinaonekana kwa mbele pale.
ANKAL NIMEKUWA NIKIITUMIA HIYO MBINU KWA MIAKA MITATU SASA JIJINI DAR ES SALAAM (NA SIPO PEKE YANGU) NA INAFANYA KAZI VIZURI SANA KWANI WANAPOFIKA MGAMBO WAKIKUTA HICHO CHUMA WANAJUA TAYARI WENZAO WAMESHALIFANYIA KAZI.HIVYO INANIWEZESHA KUPAKI POPOTE NA KUFANYA SHUGHULIZANGU HADI NINAPOAMUA KUTOKA MAHALI HAPO.KUISHI MJINI FORM SIX TUMEAMUA KUWA WABUNIFU KAMA WAINGIZA VIRUS KWENYE MITANDAO.
ReplyDeleteDuuuh, kweli mjini shule. Hakika imetulia hiyo
ReplyDeleteDawa ni kumuengezea pini nyengine tu. Mgamo kazi kwenu, mambo hadharani.
ReplyDeleteKweli "Fakhari MAMA wa ujinga". Unaiba, halafu unakwenda kujisifia kwa raia, hujuwi miongoni mwao mna hao mgambo, polisi na vyombo husika. Hetu fikiri na tafakari kabla hujaamuwa kusema au kutenda jambo.
ReplyDeletewe mdau wa kwanza huna akili,huo sio ujanja ni upuuzi.
ReplyDeleteNyinyi mnaojisifu kwa maovu ndio mnaotusababishia msongamano wa mafoleni,fateni sheria bila shurti,usitete maovu yako.
ReplyDelete