Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu julius Nyerere akitokea Addis Ababa nchini Ethiopia alipokwenda kuhudhuria mkutano wa World Economic Forum(WEF).(picha na Freddy Maro)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 11, 2012

    INAKUWAJE MUHESHIMIWA ANAJISHIKIA MWAMVULI,AAA HII SI SAWA KABISA.MUHESHIMIWA MKUU WA MKOA NA WAHESHIMIWA WENYE SUTI VIPI?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 12, 2012

    acha ubwege wewe Anonymous fri may 11 07:48:00 kwani asishike mwamvuli yeye ni nani mungu au??si ni binadamu tu kama sisi ila ni jina tu anaitwa raisi, wabongo bado tuko nyuma tunapenda kunyenyekea watu sababu ya vyeo vyao, mwamvuli atashika na kula atakula mwenyewe hakuna mtu atakayemlisha.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 12, 2012

    Mheshimiwa ameonyesha kuwa yeye ni kiongozi tu, na si mtawala kama walivyo akina Museveni na wengineo.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 12, 2012

    ndo peoples' power sisi ndiyo tumewaajiri waheshimiwa hawa hivyo mambo ya ukubwa kuwashikia miavuli huku tunalowa wakati sisi tunawalipa mishahara imepitwa na wakati.

    Heshima ni kitu cha bure na hailetwi na kuwashikia miavuli.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 12, 2012

    mimi nataka hata hayo mambo yakupokeana yaondoke maana wanapoteza pesa za mafuta,usumbufu wa barabarani maana hao viongozi wote wakipita njia zinafungwa na kadhalika kwa hiyo wana uwezo wakukutana huko ikulu tu bila ya wao kwenda uwanjani kupunguza adha kwa wengine na kubana matumizi.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 12, 2012

    Anon wa kwanza, huyo yupo hapo kwa kuwa wewe ndio ulimweka hapo nikiwa na maana kwamba kura zetu wananchi ndio zilimfanya afike hapo na alikuwa kama wewe na mie before hivyo suala la kushika mwamvuli ni sawa kabisa, ningependa siku moja viongozi wetu katika kampeni za kupanda miti waache kuigiza kwa kupanda huku wametandikiwa zulia.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 12, 2012

    nimefurahishwa na rais kushika mwamvuli mwenyewe . yeye ni mtu kama sisi tu ! na ameonesha uzalendo wake !

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 12, 2012

    Sat May 12, 09:59:00 AM 2012
    We ndugu uzalendo wa mtu unaokana kwa kujishikia mwavuli!! Hebu nenda mbali zaidi ya hapo

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 12, 2012

    KIKWETE NI MTU WA WATU NA NI MZALENDO.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 12, 2012

    Anonymous said.....

    sio kosa kwa kwa kiongozi wa nchi kuchika mwamvuli mwenyewe, kwanza jamaa apendelei sana hata vitu vidogo kama kushika mwamvuli wamshikie, mimi nahisi hapendi kunyenyekewa sana ndio maana anafnya hivyo mwenyewe sio kwamba hawapendi kumshikia mwamvuli, nahisi atakuwa anakataa mwenyewe. maana nakumbuka kuna moja pia alikuwa morogoro hivi kama sijakosea mvua inanyesha anaenda kuhutubia kwenye jukwaa akawa ameshika mwamvuli mwenyewe, kwa hiyo hii si mara ya kwanza kwa jk kufnaya hivyo.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 12, 2012

    He watu wa humu ni mambumbumbu. Wameenda shule lakini wametoka na vyeti, Elimu wameiacha huko huko. Mtadesa, kama Chadeema inavyodesa.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 12, 2012

    unkala hivi ile ndege mpya ya kukodi ya ATCL ilishafika Tanzania? last week ilituwekea picha kwamba atcl wanaleta ndege siku ile ile, au bado iko angani. ukichukulia kutoka egypt mpaka bongo ni mbali so inawezekana ikachukua wiki angani kufika Dar:)) fuatilia!!!

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 12, 2012

    Kwekwekwe

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 13, 2012

    sasa jamani kulikuwa na haja ya zulia na mvua hizi? maana hilo zulia mpaka likauke na mvua zinaendelea si noma?

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 13, 2012

    Mnaacha kuongea ishu za maana mnaanza ku discuss ishu za mwamvuli watu wengine ujinga mtupu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...