MAREHEMU LUCY S. WAMBURA (MAMA LUCA)
Ilikuwa kama ndoto lakini ni kweli yalitimia, tunaamini kimwili hauko nasi lakini kiroho tunakukumbuka daima mpendwa wetu. Upendo wako kwa familia hautasahaulika kamwe na hakuna wa kuliziba pengo.
Ni miaka 11 sasa imepita tangu ulipotutoka mpendwa wetu dada Lucy S. Wambura (Mama Luca), Unakumbukwa daima na mama yako kipenzi Mama Lucy (Annastazia) na wadogo zako wote Dory, Grace, Theo, Tinna, Pendo na Anna wanoa Mr, Iddi, Jacky, Luca, Josepha (Kurwa) na Joan (Doto).
Kutakuwa na Misa ya kumwombea marehemu siku ya Jumamosi tarehe
05-05-2012 katika kanisa la Parokia ya bikira Maria mama wa huruma Mbezi Beach-Tanki Bovu saa 12:30asubuhi na baada ya misa kutembela nyumba ya milele alipolala mpendwa wetu Lucy, Makaburi ya kinondoni.
Wote mnakaribishwa.
Raha ya milele umpe eeeh bwana na mwanga wa milele umuangazi apunzike kwa amani – Amina
Wewe unalazimisha watume picha lakini mwenyewe hutaki kuweka ya kwako. Weka ya kwako tuone ulivyokomaa na vibarua vya masaa 24 kwa 24 ya UK. Rudi Tz utapata mara moja. Kila la heri mdogo wangu, ila inatia huruma!
ReplyDelete