MAREHEMU KENNETH MTENZI MBEYELA

Leo tarehe 07/05/2012, Baba yetu Mpenzi unatimiza miaka ishirini toka ulipoitikia wito wa MUNGU Baba.
Tunakukumbuka siku zote kwa kufuata mafundisho yako kiasi kwamba tunaona kama ni jana tu ulipotuacha.
Tunamshukuru MUNGU daima kwa malezi mema na msingi bora wa maisha uliyotupa kwani yanatupa muongozo katika maisha yetu kila siku.
Upendo wako, ucheshi, ukarimu na moyo wa ushirikiano ilikuwa ni kiungo kwa familia, ukoo wa Mkongwa, na hata majirani.
Tulikupenda mno, lakini  upendo wa MUNGU umezidi.Mapenzi ya Bwana yatimizwe.
Tunamshukuru MUNGU kwa kuwa kazi aliyokubariki kuitenda duniani uliimaliza.
Neno la MUNGU linatufundisha Kushukuru Kwa kila jambo;Nasi tunamshukuru MUNGU daima.
Unakumbukwa sana na watoto wako, wajukuu na vitukuu.
         Bwana alitoana Bwana ametwaa jina la Bwana lihimidiwe.
Amina.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Tunakukumbuka sana mjomba wetu, tunakukumbuka kwa mengi mazuri, upendo uliokuwa nao hakuna wa kukulinganisha. NI KWELI VIZURI HAVIISHI.
    Mungu ailaze roho yako mahali pema peponi.
    AMEN.

    L. Nyalusi

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 07, 2012

    Alikuwa ni mwanayanga imara na mwaminifu!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 07, 2012

    R.I.P baba yetu daima tutakukumbuka, ila pole jana yanga wameumizwa ile mbaya hadi aibu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 07, 2012

    Yanga jana imefungwa 5 kwa nunge na Simba Sc.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 07, 2012

    NAMKUMBUKA SANA MZEE HUYU ALIKUWA NA TIMU YAKE KUBWA SANA PALE NYUMBANI NJOMBE INAITWA KAYE SPORTS CLUB,ILITISHA WATU WA KIGOMA WANAIKUMBUKA KAMA SIKOSEI ILIFIKA NUSU FAINAL KLABU BINGWA YA TANZANIA IKATOLEWA NA SIMBA MWAKA 1973

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 07, 2012

    Namkumbuka sana huyu Mzee! alikuwa jirani yangu pale Indira Gandhi au Market street! alipenda sana soka! Mungu aendelee kukulaza mahala pema Amen Mzee Mbeyela

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 07, 2012

    Duh! Poleni. Nakumbuka kama alishawahi kuishi Iringa vile na mmoja wa watoto wake alikuwa rafiki yangu. Kama kumbukumbu zangu ni za kweli naomba mawasiliano na mmoja wa watoto wake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...