MAREHEMU KENNETH MTENZI MBEYELA
Leo tarehe 07/05/2012, Baba yetu Mpenzi unatimiza miaka ishirini toka ulipoitikia wito wa MUNGU Baba.
Tunakukumbuka siku zote kwa kufuata mafundisho yako kiasi kwamba tunaona kama ni jana tu ulipotuacha.
Tunamshukuru MUNGU daima kwa malezi mema na msingi bora wa maisha uliyotupa kwani yanatupa muongozo katika maisha yetu kila siku.
Upendo wako, ucheshi, ukarimu na moyo wa ushirikiano ilikuwa ni kiungo kwa familia, ukoo wa Mkongwa, na hata majirani.
Tulikupenda mno, lakini upendo wa MUNGU umezidi.Mapenzi ya Bwana yatimizwe.
Tunamshukuru MUNGU kwa kuwa kazi aliyokubariki kuitenda duniani uliimaliza.
Neno la MUNGU linatufundisha Kushukuru Kwa kila jambo;Nasi tunamshukuru MUNGU daima.
Unakumbukwa sana na watoto wako, wajukuu na vitukuu.
Bwana alitoana Bwana ametwaa jina la Bwana lihimidiwe.
Amina.
Tunakukumbuka sana mjomba wetu, tunakukumbuka kwa mengi mazuri, upendo uliokuwa nao hakuna wa kukulinganisha. NI KWELI VIZURI HAVIISHI.
ReplyDeleteMungu ailaze roho yako mahali pema peponi.
AMEN.
L. Nyalusi
Alikuwa ni mwanayanga imara na mwaminifu!
ReplyDeleteR.I.P baba yetu daima tutakukumbuka, ila pole jana yanga wameumizwa ile mbaya hadi aibu.
ReplyDeleteYanga jana imefungwa 5 kwa nunge na Simba Sc.
ReplyDeleteNAMKUMBUKA SANA MZEE HUYU ALIKUWA NA TIMU YAKE KUBWA SANA PALE NYUMBANI NJOMBE INAITWA KAYE SPORTS CLUB,ILITISHA WATU WA KIGOMA WANAIKUMBUKA KAMA SIKOSEI ILIFIKA NUSU FAINAL KLABU BINGWA YA TANZANIA IKATOLEWA NA SIMBA MWAKA 1973
ReplyDeleteNamkumbuka sana huyu Mzee! alikuwa jirani yangu pale Indira Gandhi au Market street! alipenda sana soka! Mungu aendelee kukulaza mahala pema Amen Mzee Mbeyela
ReplyDeleteDuh! Poleni. Nakumbuka kama alishawahi kuishi Iringa vile na mmoja wa watoto wake alikuwa rafiki yangu. Kama kumbukumbu zangu ni za kweli naomba mawasiliano na mmoja wa watoto wake.
ReplyDelete