Chama Cha Mapinduzi kupitia kitengo cha Mawasiliano na Umma chini ya Idara ya Itikadi na Uenezi imeanzisha Blogu ambayo pamoja na kuhabarisha habari za mapema kabisa za shughuli za Chama, lakini itakuwa ikiyapa kipaombele pia kuhabarisha matukio mbalimbali tangu ya Kijamii, Siasa, Biashara, Uchumi, Burudani, Sanaa na Michezo na pia kupokea na kuyasambaza maoni ya wengine ili mradi yatakuwa na lengo linalotofautiana na ukiukwaji wa maadili ya vyombo vya habari.
Kwa heshima, Chama Cha Mapinduzi kinawasilisha kwako uitangaze Blogu hii kama utakavyoona inafaa, lakini pia uendelee kuanzia sasa kuwa mdau wa kuiperuzi ili kuwa chanzo chako cha kwanza cha kupata habari muhimu za kitaifa na kimataifa.
Baadhi ya dondoo muhimu kuhusiana na blogu hii zipo kwenye Logo iliyoambatanishwa na salam hizi.
Blog: CCM Chama Blog
mbona ina mambo yale yale ya hii blog? au ni tawi lako bwana anko? hawana jipya la kuweka huko?
ReplyDeleteOyeeeeeeeeeee oyee oyeeee hivi ndivyo sisi wapenzi na wanachama wa hiki chama makini tunavyotaka.
ReplyDeleteCCM ni lini mtatulia mfanye mambo yenu kisomi? Kila kitu ni kufanya kwa kukurupuka tu .. hamkai chini mkafanya kitu kwa umakini.
ReplyDeleteKwenye top banner/ heading mmeandika CCM Chama Blog then chini yake mmeandika www.ccmchama.blogspot.blogspot.com/ sasa hii ndio nini? Blog yenu sio hiyo mlitakiwa muandike www.ccmchama.blogspot.com. Yaani mpaka mnafikia kutangaza "public" na wala hamjaliona kosa hilo, lakini sishangai sana maana CCM ni chaka la watu sub-standard!
Mnakumbuka shuka wakati kumekucha? kaazi kweli kweli!
ReplyDeletenajuuuta kukufahamu! Siku nyingi tulishakutoa mioyoni mwetu
ReplyDeleteCHADEMA hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!
ReplyDeleteMmeiga mawazo ya NCCR-Mageuzi? maana wao wanayo siku nyingi;
ReplyDeletemawasilianonccr-mageuzi.blogspot.com/
CHADEMA hoyeeeeeeeeeeeeeeeeee!
ReplyDeletesory jamani, CCM mhhhhhhhhh! hahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!
Rangi hiyo ya kijani inaumiza macho sio lazima iwe kwa wingi hivyo....
ReplyDeleteSAFI SANA! PONGEZI NA HONGERA CCM. CHAMA PEKEE TANZANIA KISICHO NA UDINI, UKABILA NA UBAGUZI WA RANGI. CCM IMARA DAIMA!
ReplyDelete