Mkuu wa kitengo cha ramani kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Vincent Mugaya akitoa ufafanuzi kwa makamu wa rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal kuhusu moja ya ramani inayoonyesha maeneo ya sensa ya watu na makazi 2012 jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiangalia ramani ya Tanzania inayoonyesha maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya sensa ya watu na makazi itakayofanyika mwezi Agosti leo mjini Tabora wakati wa ufungaji wa awamu ya kwanza ya utengaji wa maeneo ya sensa ya watu na makazi huku akiwataka wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo ambalo litaendeshwa kwa usiri na kuongeza kuwa takwimu zitakazopatikana zitatumika katika shughuli za maendeleo na si vinginevyo.
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal akizungumza jambo na mkuu wa mkoa wa Tabora Bi. Fatma Mwasa wakati wa sherehe za ufungaji wa awamu ya kwanza ya utengaji wa maeneo ya sensa ya watu na makazi katika viwanja vya Chipukizi mkoani Tabora.
Wadau wa sensa ya watu na makazi 2012 Bw. Bakari Kimwanga kutoka gazeti la Mtanzania (kushoto) na Bw. Said Ameir kutoka Ofisi ya taifa ya Takwimu (kulia) wakiwa ndani ya msitu wa tula wilayani Uyui kwenye barabara kuu itokayo mkoani Tabora mara baada ya kukamilika kwa shughuli za ufungaji wa awamu ya kwanza ya utengaji wa maeneo ya sensa ya watu na makazi zilizofanyika kitaifa mkoani humo.
Kijana mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja akiwa katika viwanja vya Chipukizi mjini Tabora kushuhudia ufungaji wa awamu ya kwanza ya utengaji wa maeneo ya Sensa ya watu na Makazi.
Vijana wa kikosi cha ulinzi wa jadi cha Sungusungu (waliokaa chini) pamoja na wananchi wa mkoa wa Tabora wakifuatilia zoezi la ufungaji wa awamu ya kwanza ya utengaji wa maeneo ya sensa ya watu na makazi mkoani Tabora.Picha na Aron Msigwa -MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 11, 2012

    Angalia nyuso za wananchi, Tabora imejaa vijana wabichi from age 20 to 40 hawana kazi, umri huu ndiyo safi kwa kuutumia kujenga nchi na vijana hawa kunufaika na jasho lao-lakini wapi !! Kina Maige ndo kwanza wanajilimbikiza mali,nyumba yake ya kuishi yenye dola LAKI 7 Nyerere alisema (quote) tusipowangalia hawa wengi hawa !! watakuja siku moja kututoa mbio maofisini kwetu. Maige hilo jumba lako hilo,linaweza kuwa lisikalike,kama hawa sungu sungu watataka haki yao. Nyerere alikuwa mtu wa kuona mbali.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...