Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal akipokewa na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Tabora wakiongozwa na Mkuu wa mkoa huo Bi. Fatma Mwasa (aliyevaa kilemba) na viongozi kutoka ofisi ya taifa ya Takwimu mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa mkoa huo kwa ziara ya siku mbili ambapo pamoja na mambo mengine atafunga awamu ya kwanza ya kutenga maeneo ya maandalizi ya Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 kitaifa katika viwanja vya Chipukizi mkoani Tabora.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal akipata maelezo kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Tabora Bw. Mussa Chang’a (mwenye suti nyeupe) kuhusu vikundi mbalimbali vya burudani vilivyokuwa vikitumbuiza wakati wa mapokezi yake mkoani Tabora.
Mkuu wa mkoa wa Tabora Bi. Fatma Mwasa akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya mkoa wa Tabora kwa makamu wa rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal. Kulia ni waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa.
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal akizungumza na viongozi wa mkoa wa Tabora mara baada ya kupokea taarifa ya maendeleo ya mkoa huo ambapo ametoa wito kwa viongozi hao kufanya kazi kwa bidii na pia kuwahamasisha wananchi kushiriki katika sensa ya watu na makazi itakayofanyika nchi nzima kuanzia tarehe 26 mwezi Agosti.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa (kushoto) akizungumza jambo na mkuu wa mkoa wa Tabora Bi. Fatma Mwasa(kulia) mjini Tabora.

Na Aron Msigwa – MAELEZO,Tabora.

Makamu wa Rais Dkt. Maohammed Gharib Bilal amewataka viongozi kote nchini wawe mfano wa kuigwa kwa kutoa ushirikiano na kukubali kuhesabiwa wakati wa zoezi la sensa ya watu na makazi itakayofanyika nchi nzima mwezi Agosi mwaka huu.

Akizungumza na viongozi wa mkoa wa Tabora leo mara baada ya kuwasili kwa ziara ya siku mbili Dkt. Bilal amesema sensa ya watu na makazi ni muhimu kwa taifa kwani itatoa mwelekeo wa nini cha kufanya kwa maendeleo ya taifa.

Amesema viongozi bila kujali nafasi walizonazo wanalojukumu kubwa la kuhahkikisha kuwa zoezi la sensa ya watu na makazi linafanyika kwa ufanisi mkubwa kutokana na mikakakati na maandalizi mazuri yaliyofanywa na ofisi ya taifa ya Takwimu.

Amefafanua kuwa kila mtanzania ni mshiriki wa zoezi hilo huku akitoa wito kwa wananchi wote kujitokeza na kutoa ushirikiano siku ya sensa ili waweze kuhesabiwa katika maeneo yao.

“Sisi sote ni washiriki wa zoezi hili , sote lazima tukubali kuhesabiwa hivyo jukumu letu ni kuhamasishaba ili tuweze kuleta mabadiliko” amesema.

Ameongeza kuwa upatikanaji wa takwimu sahihi za idadi ya watu na makazi pamoja na hali ya kiuchumi utatoa dira ya upangaji wa mipango mizuri ya maendeleo ya taifa.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Tabora Bi. Fatma Mwasa akitoa salaam za mkoa huo na taarifa ya utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo amesema mkoa wake umepiga hatua kimaendeleo licha ya changamoto mbalimbali zilizopo.

Amezitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na tatizo la ajira, bei za bidhaa kupanda mara kwa mara kutokana na ukosefu wa miundombinu inayoufungua mkoa huo na mikoa mingine pamoja na tatizo la upatikanaji wa maji ambalo ameiomba serikali kutekeleza mradi wa maji kutoka ziwa Victoria.

Aidha ameipongeza serikali kwa kuuchagua mkoa wa Tabora kuwa mwenyeji wa ufungaji wa awamu ya kwanza kitaifa ya kutenga maeneo ya maandalizi ya sensa ya watu na makazi itakayofanyika nchi nzima mwezi Agosti mwaka huu.

Ikumbukwe kuwa zoezi lz sensa ya watu na makazi la mwaka huu litakalodumu kwa siku saba linafanyika ikiwa ni miaka 10 baada ya sensa ya mwisho iliyofanyika mwaka 2002 wakati sensa nyingine zilifanyika nchini miaka ya 1967, 1978 na mwaka 1988.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 09, 2012

    MASHAKA ANALYSTS OF WOLSTRIT USA DONT WORK IN TANZANIA AND AFRICA. YOU PREDICT OF ECONOMIC CRIISIS. tanzania haijapata economic crisis, so this analyst dont work here but in america. mimi hizi nitaita longolongo zenu za huko marekani. wamarekani ni watu wasio aminika kabisa heri ndugu zetu wachina kusema kweli kwa sababu maendeleo yao hapa tanzania yanaonekana kila sehemu. wachina ndio watu wanaotuletea maendeleo bila masharti ya kutuibia ardhi

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 09, 2012

    jamani hawa viongozi kazi yao ni kutembea tu ? kwani kila kukicha naona wapo sijuhi wapi sijuhi wapi , ifisini akuna paper works za kufanay ?

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 09, 2012

    jeshi raha saana, mwenye cheo kikubwa akaa kulia, angalia hapo magereza SSP yuko kulia kwa meja wa JW.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 09, 2012

    we anony wa 04.12 hebu jifunze kuandika. sijuhi na ifisini ndio nini

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...