Mbunge wa Arumeru Mashariki,Mh. Joshua Nassari (Chadema) akisalimiana na Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha, Afande Akili Mpwapwa katika makao makuu ya jeshi hilo mkoani hapa,alipojisalimisha baada ya kutakiwa kuripoti kituoni hapo
 Wakili Albert Msando akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya Jeshi hilo mkoani Arusha akiwa na  Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Mh. Joshua Nassari (Chadema) alipojisalimisha Polisi  yeye mwenyewe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 09, 2012

    Ulianza na Mungu hakika utaendelea kumtegemea katika mapambano ya kutetea wanyonge. Mungu akutangulie hyo ni mitikisiko kumbuka every new level has a new devil mtegemee Mungu nae hatakuacha

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 09, 2012

    Ndo kwanza unamaliza mwezi unaanza kupambana na sheria? Hii sio ishara nzuri kwako, unapoongea kwenye majukwaa ya kisiasa tumia busara sio jazba utachemsha na safari yako itakuwa fupi sana katika ulimwengu wa siasa! Nchi hii inaongozwa kwa utawala wa sheria na lazima tutii sheria hizo kwani hakuna aliyejuu ya sheria na ukivunja sheria utaingia pabaya! huwezi ukaropoka ovyo ovyo! Mjirekebishe vijana mmeanza kuchemsha!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 09, 2012

    sasa jamani tumewatuma mukatutete bungeni sasa na haya majukumu ya kwenda polisi kwa kesi kila siku mbona majukumu yatakuwa mengi? tuonee huruma wananchi wenu tunateseka sana na haya maisha magumu

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 09, 2012

    Demokrasia yetu bado haijakua,lakini ,iko njiani kukua ,tumetoka mbali. Huyu mbunge ,mimi silioni kosa lake ila inavyoonekana tu ni kwamba Polisi wanalazimisha siasa iwe upande mmoja , democracy maana yake ni uhuru wa kutoa maoni bila woga wowote, sasa basi sisi wapiga kura ndio tutakaokuwa mahakimu wakuona kwamba huyu mwana siasa ni mchochezi au ni muongo au mhuni, siyo Polisi watuambieni hili wala lile. Juzi juzi tu tuliona mtu kavaa t shirt ina picha ya nyani imeandikwa Obama,polisi hawakumkamata wala kumsaka hadi uvunguni,bali wananchi ndiyo waliomkosoa huyo bwana na yeye kujiona mjinga , kwetu polisi eti ni nguvu ya kutushikiza adabu sisi raia, siyo hivyooo !!!! nyie ni chombo cha kulinda raia na siyo kutufundisha tabia. Na kukiita chadema kwamba ni chama cha wahuni,inadhihirisha wazi kwamba bado mna kasumba ya chama tawala. badilikeni.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 09, 2012

    Wewe unaongea nini hapo juu,Unajua maana ya nchi kuendeshwa na utawala wa sheria?Hamna utawala wa sheria Tanzania.Ni mabavu,uonevu na rushwa imejaa kuanzia Mahakamani,Polisi hadi Serikali.Ukiwa fedha unaweza kununua mahakama hadi Polisi.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 09, 2012

    Hivi mbona huyo mbunge kaongea maneno mawili tena siku moja akakamatwa, je hao polisi wanaopokea rushwa kila siku barabarani na kwingineko mbona hawakamatwi. Huo ndio utawala wa sheria wanaoutekeleza? Walipaswa wawe mfano wa utawala wa sheria.

    Isitoshe maneno aliyosema Nasari ni kwa watu wa kanda ya kaskazini na Mwanza kujitenga na Tz. Kwani hiyo ni dhambi? Nchi ngapi zilipatikana kwa kujitenga? Kama watu wa kaskazini wameona wengine hampo tayari kutetea maslahi yenu kwa nini wasijitenge?

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 09, 2012

    Ni vyema kuanza na Mungu na kumaliza na Mungu.Lakini tuangalie vema na kukumbuka kuwa Mungu anataka unyenyekevu sana kama wataka kufanya kazi yoyote unayotaka kutumikia kwa kumtukuza.

    Mungu anasema heshimu mamlaka iliyopo,maana ni ya watu na imewekwa na watu kwa ajili yao.Palipo na watu na Mungu yupamoja nao.

    Kumbuka siku moja nawe waweza kuwa katika mamlaka,hivyo utataka watu waliochini yako waheshimu mamlaka.

    Umechaguliwa na watu,tulia ufanye kazi za watu usiwavuruge na kupandikiza chuki kati yao.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 09, 2012

    Huyo ndio Mbunge ameanza kazi akiwa madarakani !

    Dogo Joshua, ingefaa Uongozi wa chama chako ukuhamishie kwa muda CCM ili uhudhurie Mafunzo mafupi ya Uenezi na Ukada wa Chama cha Siasa.

    Una umuhimu wa kujifunza 'Speech Technology' yaani 'Utaalamu wa kutoa Hotuba'

    Ama sivyo Siasa itakuwa ni tasnia ngumu kwako kwa Mtaji huo !

    Huwezi kuchomoka hapo?

    Muda mwingi utakuwa unafukuzana na Mamlaka na Wana usalama badala ya Kuwahudumia Wapiga kura wako

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 09, 2012

    huyu dogo AJIFUNZE na kuacha kuropoka ropoka.......kuongea mambo mazito namna ile ni UJINGA na kukosa umakini

    MTANZANIA

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 09, 2012

    Sijaona Polisi washamba kama wa Tanzania. Katika siasa maneno tola kwa wapinzani ni litu cha kawaida sana sijaona cha ajabu wala cha kuhatarisha amani ni kukuza mambo kitoto sana!! Watakuja zoea ni utoto tuu wakikua wataacha..
    Mimi.

    ReplyDelete
  11. UJANA UNA MAMBO, MH. NASSARI WATANZANIA TUNAPENDA MABADILIKO NA SIO VITA YA KUANZA KUGOMBANIA MIPAKA TUPE SERA ZA MAANA SIO ETI KASKAZINI TUUNDE TAIFA LETU LA KAZI GANI HUU SI WAKATI WA WA WATU KUBEBA MAPANGA. TUNATAKA TUSIKIE UTATUSAIDIAJE KUJIKWAMUA KIUCHUMI SI VITA VYA KUDAI JAMHURI YA KASKAZINI, ACHA KULEWA SIFA UTAWAHARIBIA CHADEMA ONA SASA HATA M.KITI WAKO KAKUSHUSHUA UNA MAWAZO YA KITOTO, NENDA KAFANYIWE REHAB YA KISIASA USITULETEE VITA WENZIO.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 09, 2012

    Tatizo ni uelewa wa sera za chama. Kama dogo angekua amepikika vizuri; naamini angetoa maneno mazuri ambayo yangekua na maana hiyo hiyo. Hebu viongozi wa Chadema wapeni vijana sera zenu za maendeleo wazinadi. Chadema msijiingize kwenye kosa la CUF ya wapemba kwa manufaa ya pemba! Zanzibar ndogo.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 09, 2012

    Maana ya Upinzani wa Kisiasa:

    Sio uvunjaji wa sheria,ukorofi,ukiukaji wa taratibu na vurugu.

    Siasa ni zaidi ya Ustaarabu!

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 09, 2012

    Nyie polisi wa Tanzania mbona kukiwa na majambazi hamuangaiki kiasi hicho? tunaibiwa kila siku watu wanauliwa ovyo nendeni kigoma, karagwe na kwingineko majambazi yanateka magari kila mara wala hamuwakamati ila wanaotukana ndo mnaona wanawafaa zaidi hivi kazi yenu mnaijua ama ndo mnatumwa? Nyie wenyewe tunawajua mnavoteseka na tumishahara tuduchu leo hii wanajitokeza watu wanaoweza tetea hata nanyie mnufaike nyie ndo kila siku kuwakamata huwa najiuliza sana mna matatizo gani sielewi kabissa mbona lusinde alisema baba yake silaa ni Shoga sikusikia mmemkatamat kwa kutoa lugha chafu na akasema lema alipata bwana jela yote haya hamkuyasikia la huyu kijana ndo mmzezibua masikio? tendeni haki kwa wote jamani Mungu anawaangalia

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 09, 2012

    Mimi siyo mwanachama wa chama chochote na wala sipendi siasa.Nimesikiliza hotuba ya huyu mbunge wa arumeru inaonekana bado anajina yuko kwenye kampeni zake za kugombea ubunge, amesahau kuwa yeye ni mbunge wa serikali ya jamhuri ya muungano wa tanzania ambao ndio watunga sheria za nchi na wasimamizi wa sheria za nchi. ingekuwa ni kipindi cha nyerere angekuwa kiziwizini sasa hivi. huwezi kutangaza vita na nchi kama anavyoongea kuwa atajitenga kuanzia shinyanga mwanza na arusha wawe nchi moja na rais hataweza kukanyaga. unamtishia rais kwenda kwenye sehemu ya nchi yake. huyu sio mbunge ni gangster. serikali ipitie sheria za mihadhara la sivyo tutaelekea pabaya kwa kuwa na watu kama hawa. TUTAKUWA KAMA SUDAN KWELI...THIS IS VERY DANGEROUS. VIONGOZI WA CHADEMA PIA WANATAKIWA WALIFANYIE KAZI HILO. HOTUBA HAIKUWA NZURI KABISAAAAA

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 09, 2012

    Joshua Nasari Kisiasa bado upo Chekechea kaa na Wanasiasa Wakongwe kwanza wakupe Mikoba.

    Kuongea na watu wenye akili zao halafu ukasomeka sio kitu cha mchezo.

    Kuvalishwa hayo Magwanda ya Mgambo yaliyokuzidi vipimo 'over size' sio kigezo cha kuimairika Kisiasa !

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 09, 2012

    CHONDEE CHONDE HAWA VIJANA WALIOPATA UONGOZ CHADEEMA TARATIBU JAMAN TUMEFIKIA PAZURI ILA KWA MANENO YENU MNATAKA KUBOMOA HAMJUI MKIFANYA MISTAKE MOJA MNAWAPA CCM ADVANTAGE KUBWA.PLS BABA SLAA NA MBOWE EMBU KAENI NA VIJANA HAO MUWAPE MASOMO KWANZA WASITUHARIBIE MANA 2015 TWACHUKUA NCHI SO MSITUHARIBIEE.PLS PLS NINGEKUA NA NAMBA YA DR SLAA AU MBOWE NINGEMPIGIA.MWNY NAYO MSAADA TUTAN AU MKIWEZA MFIKISHIENI HUU UJUMBE.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 09, 2012

    huyu dogo amechemka sana!! he is an IDIOT!! viongozi wanaoneza propaganda za ubaguzi wa kidini, rangi au kama huyu mpuuzi anayeropoka hovyo majukwaani ni wa kuogopwa kama ukoma! Hafai

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 09, 2012

    Mtoto anapokuwa anajifunza kutembea mara nyingi atadondoka sana lakini haimaanishi kwamba wazazi wampige na kumzuia kutembea tena bali watamfuta vumbi na kumpa pole na ataendelea tena ataanguka hawamkatishi tamaa. Hivyo basi kama mnavosema kuwa uisivyo wanaomfahamu kwa ukaribu kaeni nae na pia viongozi wa chadema wamfunze kitu gani anatakiwa kuongea kwa wakati gani. Sidhani kama hawezi ubunge ila ni ugeni katika siasa kama ambavyo unaweza anza kazi mwezi wa kwanza kila unachoandika boss anakushangaa wewe kweli ulipewa cheti? ila boss mzuri hatakwambaia u mjinga bali atasema theory na practical ni tofauti basi huku kazini huwa tunafanya hivi na hivi then after muda kidogo unajikuta nawe umezoea. Kijana aonywe tu then afundwe aendelee na kazi ya kujenga taifa.
    ASANTENI
    MWANA CCM MPENDA HOJA ZA KUJENGA

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 09, 2012

    KUNa jinga moja huku linasema Chadema wasijiingize siasa za Cuf kudai Pemba,hili jitu halina akili wala elimu,

    CUF SIO WANODAI PEMA wananchi ndio wanaodai visiwa vyao Cuf haijasimama hata siku moja kusema tunataka kujitenga walichosema ni MUUNGANO WA SERIKALI TATU Watanganyika hamuoni ufahari kuwa na serikali yenu na Wazanzibari yao halafu tuna serikali ya Muungano hapooo,hvi hamuoni faida ya nyinyi kutambulika?

    sasa kama nyinyi hamtaki utajiri mbona hamvitoi visiwa likija suala la Zanzibar mbio mbio mko tayari kutatua keroo za Muungano kama havina faida mbona mnang'ang'ania ?

    Raha ya Ngoma uingie ucheze sasa na wewe kaishi kule Pemba au Unguja uone raha yake. Pumbaffuuuu

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 10, 2012

    Huyu hata wakati wa campaign alikuwa anamuiga Mbowe kusema, pozi zake na hata mwendo. Naona bado hajamaliza shule amezoea KUDESA kwa hivyo kimsikia Slaa akimwita kikwete yeye anadesa na kuengeza ya kwake, eeeh si lazima amzidi mwalimu kidogo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...