Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, amekutana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Terezya Huvisa, kwa mazungumzo na kupokea taarifa ya zoezi la Bomoa bomoa nyumba zilizojengwa maeneo ua Ufukweni, ambalo linatarajia kuanza hivi karibuni. Mazungumzo hayo yalifanyika Ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu Dar es Salaam leo Mei 17, 2012. Katika picha kutoka (kushoto) ni Katibu wa Wizara ya Ardhi, Veldiana Mashingia, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka (kulia) ni Mkurugenzi wa Mazingira, Dkt. Julius Ningu na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Terezya Huvisa, baada ya mazungumzo hayo. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...