Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar akiwa na Mhe. Dan Boren, Mbunge wa Bunge la Marekani kutoka Oklahoma,aliyemtembelea ofisini kwakwe.
Mhe.Balozi Maajar akiwa katika picha ya pamoja na Mbunge Dan Boren,Mkurugenzi wa Bunge, Bi.Hilary Moffett,na kushoto na kulia na Bibi Lily Munanka Mkuu wa Utawala Ubalozini na Afisa Ubalozi Bw. Suleiman Saleh.

Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar,Jumatano Mei 9, 2012 alimpokea Ubalozini, Mhe. Dan Boren na kufanya naye mazungumzo ya uanzishwaji wa Tanzania Caucus katika Bunge la Marekani ambapo Tanzania itakuwa imepata mtetezi na msemaji bungeni humo kila linapotokea jambo linalohusu Tanzania.

Mhe. Boren ni mbunge wa Bunge la Marekani kutoka Wilaya ya Pili, Jimbo la Oklahoma, amehamasisha na hatimaye kuanzisha kundi la wabunge wenye mapenzi na Tanzania, kamati ndogo (caucus) ya kuisemea Tanzania kwenye Bunge la Marekani.

Mhe. Boren ambaye ni mbunge kutoka Chama Tawala cha Democrat ameasisi Kundi hilo hilo akishirikiana na wabunge wenzake kadhaa wa chama chake na wengine kutoka Chama cha Republican kutokana na kufurahishwa kwao na juhudi za Serikali ya Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika kuimarisha demokrasia, utawala bora pamoja na juhudi za kimaendeleo katika sekta za uchumi, nishati, kilimo na hifadhi ya mazingira.

Katika ziara yake hapa ubalozini Mhe. Boren aliyeambatana na Bi. Hilary Moffett, Mkurugenzi wa Sheria Bungeni, alimhakikishia Mhe. Balozi Maajar utayari wake wa kuisaidia Tanzania katika juhudi zake hizo.

Aidha alibainisha kwamba Tanzania ina changamoto nyingi sana mbele yake na hivyo kuwepo kwa sauti mpya ya kuisemea katika Bunge la Marekani ni jambo ambalo analiona litakuwa na manufaa makubwa kwa nchi.

Sambamba na hilo, Mhe. Boren alibainisha kwamba Tanzania imekuwa ni moja ya nchi ambazo Serikali ya Marekani inaziangalia kwa umakini kama mfano wa nchi bora na hivyo ameona ni vyema naye akaunga mkono juhudi hizo za Serikali ya Rais Barack Obama.

Kwa upande wake, Mhe.Balozi Mwanaidi Sinare Maajar alifurahishwa na kufarijika na ujio wa Mhe. Boren Ubalozini na kumueleza kwamba atashirikiana naye bega kwa bega na kuahidi kwamba muda wowote atakapohitajika kukutana na kamati hiyo ya Bw. Boren yupo tayari.

Mhe. Maajar alimshukuru Mhe.Boren kwa mwaliko wake kutembelea Jimbo la Oklahoma ili Tanzania ipate kueleweka zaidi na hivyo kufungua pazia la ushirikiano katika sekta mbali mbali za Uchumi, Kilimo, Nishati na Utalii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 12, 2012

    Ni jambo zuri lakini hatuwezi kuendelea bila kutegemea upendeleo toka kwa wahisani? Inawezekana kama tutawashirikisha watanzania wotr na kutumia vizuri rasilimali zetu..

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 12, 2012

    Nakubaliana na anon wa kwanza.... Watz tumezidi na kutaka urahisi, kwanini tutegemee favor ya watu ili kusogeza mambo yetu?? Wasomi wapo, rasilimali nyingi saana na nguvu tunazo tusichonacho ni will ya kutaka maendeleo

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 12, 2012

    mmhh!nahisi kama tumeshakua one of the USA states.Kama nyerere akifufuka leo na kulikuta hili tukio anaweza kuomba kufa tena haraka sana.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 12, 2012

    Jamani huu ni msingi wa kwenda mbele katika mahusiano. Suala hapa si kwamba ni wahisani bali ni win win situation. Mfano talii wageni wengi zaidi wataingia nchini pato la taifa kuzidi. Kilimo kikiendelea vizuri bidhaa zetu zitaingia soko la Marekani ambalo kila mmoja wetu anajua kwamba ni kubwa mno. Tuwe positive kama tna matattizo ya ndani hayo ni ya kwetu tujirekebishe tusonge mbele lakini dunia ya sasa ni ushirikiano.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 12, 2012

    Nakubaliana kabisa na mchangiaji hapo juu.Watanzania tuangalieni mbele. Hii ni dalili nzuri.Nchi yetu vita iliyo mbele yetu ni kumuunga mkono Rais wetu na Serikali kwa ujumla. Sio Rais akibadilisha baraza tuseme chupa nyingine mvinyo uleule.Au Ma DC wapya na kuwapa fursa watu kutoka kada mbali mbali wakiwemo wanahabari basi tuseme hawana sifa. Watanzania tubadilike ,Huyo Kikwete peke yake hawezi kufanya kila kitu ni jahazi letu sote na kila mmoja wetu hana budi kuwa na mtazamo wa kimaendeleo. Mbunge wa Marekani kuweza kuanzisha hiyo caucus si jambo dogo. Bunge lao linazijadili nchi kutokana na sera ya nchi ilivyo. Tanzania sio Kenya au Uganda au Burundi mbele ya Marekani. Upepo duniani umebadilika. Leo wengi wetu tunajua kamba wakenya wanadai mlima Kilimanjaro uko Kenya? Balozi anachofanya ni wajibu wake kuitangaza nchi yetu na hata Baba wa Taifa unadhani alikuwa haipendi Marekani?Kama kumbukumbu zangu ziko sawa alikwenda Marekani mara baada ya uhuru na kupokewa na Rais Keneddy akiwa na kina Kambona.Mwalimu aikuwa pia rafiki wa Rais Jimmy Carter. Marekani inatafuta marafiki wapya siku hadi siku sasa tutakavyojipanga kufaidika na hayo mahusiano hilo ni la Serikali yetu.
    Mdau Kigoma

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 12, 2012

    Mhe. Membe mambo ndio hayo.Huyo Kitine muache Mungu. Asikupotezee muda anajua alichofanya ana usongo na wewe tu.Amepitwa na wakati aende kwenye kilimo kwanza.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 12, 2012

    Mtu yeyote aweza kunicheka, ha ha ha
    Kwani nimeona gazeti la future, na kichwa cha habari chasema:

    OBAMA RE-ELECTED IN A LAND SLIDE.....

    Mark my words

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 12, 2012

    Bila ya kuwa na faida kwa kisiasa, kiuchumi na hasa hasa stretagically kiukanda na kijeshi, hamna msaada wala kusema kokote mmarekani atakaekupendelea. Yeye hana rafiki wa kudumu ila ana adui wa kudumu. Tutahadhari sana. Serikali ya dunia sisi hatukuingia tuko katika mchakato. Mabeberu hawana lugha nzuri yeyote.

    ReplyDelete
  9. Kama jinsi mnavyoweza kutambua na kukubali kuwa kuna watanzania hawawezi kupata elimu ya juu bila msaada wa bodi ya mikopo, hivyohivyo mfahamu kuwa Tanzania na nchi nyingine masikini zinahitaji kupigwa taf na nchi zilizoendelea katika harakati za maendeleo. Hii haimaanishi kwamba sisi wenyewe hatuendelei na jitihada, ila ni LAZIMA tuwe na mikakati ya mbalimbali mojawapo ikiwa ni kupokea misaada. We are all one race, a human race!

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 13, 2012

    Yaap hili ndo tatizo letu watanzania, tunategemea sana vichwa vya wageni hasa wa magharibi katika kutatua matatizo yetu mwenyewe. Bongo za mtanzani zimelala hazitaki kufikiri tena, Hivi zile $650 Milioni za millenium chalenge ziliishia wapi zimefanya lolote sijawahi kusikia kuhusu matumizi yake?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...