CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kinawajulisha wadau mbalimbali kuwa mwili wa aliyekuwa Mhariri wa Habari za Michezo wa gazeti la Mtanzania Rachel Mwiligwa utaagwa kesho Jumatatu Mei 14, 2012 saa nne kamili asubuhi Kanisa la Anglikana Ubungo, ambalo lipo nyuma ya majengo ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Ubungo jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Msemaji wa familia, Alex Chimila, taratibu za kuaga mwili wa marehemu zitaanza saa 4:00 asubuhi na kumalizika saa 6:00 mchana, tayari kwa msafara wa kwenda kuzika katika Makaburi ya Tegeta A, Goba, jijini Dar es Salaam.

Uamuzi wa kuaga mwili kwenye eneo hilo una lengo la kutoa nafasi kwa wadau mbalimbali kupata fursa ya kushiriki kwenye tukio hilo.

Tunawaomba waandishi wa habari za michezo na wadau wengine wa michezo na burudani kujitokeza kwa wingi asubuhi kwenda kumuaga mpendwa wetu. Rachel alikumbwa na mauti usiku wa kuamkia juzi kwenye hospitali ya Mwananyamla, Dar es Salaam.

Nawasilisha.
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
13/05/2012

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...