Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akihutubia wadau wa Mfuko wa Bima ya Afya Mkoani Rukwa katika ukumbi wa Manispaa ya Sumbawanga. Katika hotuba yake hiyo aliutaka mfuko kuboresha huduma zake mara kwa mara na kuhakikisha wanawafikia wananchi wengi zaidi kujenga uelewa wa mfuko na faida zake ili waweze kujiunga. Aidha aliutaka mfuko kushughulikia malalamiko yote yanayotolea na wadau juu ya huduma zinazotokana na mfuko kwa ustawi wa mfuko na jamii kwa ujumla. Mfuko wa Bima ya Afya nchini unaadhimisha miaka 10 ya kujituma na kuaminiwa ambapo kaulimbiu yake ni "Huduma za matibabu vijijini na huduma bora za afya kwa wote.   
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa,Injinia Stella Manyanya (katikati) akizungumza na wadau wa mfuko wa NHIF katika ukumbi wa Manispaa ya Sumbawanga. Kulia ni Mganga Mkuu Hospitali ya Mkoa wa Rukwa Dkt. Gurisha John William, Afisa Tawala Mkoa wa Rukwa Festo Chonya, Katibu Tawala Msaidizi Serikali za Mitaa Mkoa wa Katavi Lauteny Kanoni, Mjumbe wa Bodi ya NHIF, Naibu Mkurugenzi Mkuu Mfuko wa Bima ya Afya Nchini Hamis Mdee na Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Sabas Katepa.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya nchini Ndugu Hamis Mdee akizungumza kwenye mkutano huo. Alisema lengo kubwa la kufanya ziara Mkoani Rukwa ni kutoa taarifa za mfuko wa bima ya afya na mfuko wa afya ya jamii pamoja na kuelezea umuhimu wa mifuko hiyo kuhamasisha jamii kujiunga ili kuongeza ushiriki katika mifuko hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...