Na Mwandishi Wetu

SHIRIKA la Ndege la Air Tanzania (ATCL) limepata ndege nyingine aina ya Boeing 737-500 ambayo inatarajia kuwasili leo hii (Alhamisi) kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, taarifa iliyotolewa na Kampuni hiyo jana ilieleza.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 108 imekodiwa kutoka katika kampuni ya Aero Vista iliyopo nchini Dubai na tayari imeshafanyiwa uchunguzi na timu ya wataalam kutoka katika Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) nchini Misri ilikoperekwa kwa ajili ya uchunguzi huo.

“Wataalam kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCCA) wamekamilisha uchunguzi wa ndege ambayo kwa sasa ipo jijini Cairo, Misri na ndege itarejea nchini kwetu leo hii mchana.

“Ndege hiyo imeshawekwa chata ya Kampuni ya ATCL na baada ya kuwasili tunetegemea itaanza kufanya safari mara moja,” Taarifa hiyo ilisema.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa ndege hiyo itakuwa na uwezo wa kuchukua abiria 12 kwenye daraja la kwanza (business class) pamoja na abiria 96 kwenye daraja la kawaida (economy class).

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Bw. Paul Chizi akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam wiki chache zilizopita alitoa maelezo kwa uchache juu ya ujio wa ndege hiyo lakini hakuweza kufafanua zaidi kuhusiana na ndege hiyo.

Chizi alisema kuwa mipango ya ujio wa ndege hiyo ilikuwa ni mipango ya muda mfupi iliyowekwa ili kuboresha huduma za ndege alisisitiza kuwa kampuni tayari ina mpango wa muda mrefu ambao utafanyiwa kazi kikamilifu.

ATCL hivikaribuni imezindua tovuti ikiwa katika jitihada za kuboresha huduma kwa wateja pamoja na kuongeza ubora wa ndege hiyo ya kitaifa.

Tovuti hiyo itawawezesha wateja kupata taarifa ya safari za ndege bila ya kufika katika ofisi za kampuni hiyo au mawakala na kuwawezesha wateja kutoa maoni yao kupitia mitandao ya kijamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 10, 2012

    ATCL:

    1.Mimi nimejaaliwa kuwa sina!
    2.Mimi Nimejaaliwa kuwa siwezi tu!
    3.Mimi nimejaaliwa nisifanikiwe!

    KTK KANUNI ZA KISAYANSI KAMWE HAKUNA KITU KAMA HICHO!

    Pana uwezeshaji wa kumtoa mtu mwathirika wa Madawa akawa hatumii tena, Pana Wataalam wa Ushauri Nasaha wakamtoa mtu ktk hulka ya uchezaji Kamari akaacha,

    Pana wawezeshaji wanaweza mpatia mtu asiyejiamini Ushauri Nasaha akajimudu na kujiamini kuendesha shughuli zake!

    Hii ATCL yetu ni wakati sasa wa kuipatia Ushauri Nasaha!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 10, 2012

    Tovuti ipi isiyopatikana kwenye google search.Aliyefanikiwa kuifungua naomba link.Nilijaribu kufungua ile tovuti tuliyotangaziwa wiki kadhaa zilizopita sikufanikiwa kuifungua.Hata hivyo nawapongeza ATCL kwa kujitahidi kuibuka upya..karibuni sana

    David V

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 10, 2012

    Inasikitisha sana kuwa bado tuna mawazo ya kukodi sio kununua ndege yetu.... yanikila usafiri ni shida Ndege za kukodi Treni ndio hakuna kabisa na City bus pia shida,, Hii serikali inachindwa nini kununu city bus,, Mwalimu aliweza mwaka 1975 alinunua maikarusi nakumbuka nilikuwa darasa la kwanza.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 10, 2012

    Hii kitu ni siasa inafanyika kwa pesa yetu sisi wa lala hoi. Inaeleweka kuwa ATCL inaendeshwa kwa hasara---it is high time such projects are killes. Ooooops nimesahau, kuna 10% ya watu hapa ndio maana wataendelea kukodi na kuzizamisha kwenye matope---10%

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 10, 2012

    jamani tutaendelea kupata hasara mpaka lini? kwani ni lazima kuwa na ATCL?? Mimi ningeshauri kama mnaona ni lazima kuwa na ATCL basi kwanza walipeni wafanyakazi wote mafao yao halafu waajirini upya kwa contract wale tu mnaowahitaji then anzeni na videge vidogo kama Coastal na Auric. Kwa madeni mliyokuwa nayo na ukiritimba wenu you can not compete with Precision na 540. Find a niche, leteni ndege itakayotua majini ama kivukoni ama slipway so you can beat the traffic for business travellers, Arusha Dar City au Zenj Dar City, flights between mikoa or between mikoa na nchi za jirani (how does one fly to Malawi?)

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 11, 2012

    Tanzania haina shirika la ndege. Nchi inatumiwa na kunyanyaswa na South Africa.

    Mdau Europe

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 11, 2012

    Wazee wenu walikaa pale wakala mpaka wakatajirika, Hii Dar es Salaam ilivamiwa na Mwalimu alishindwa mwisho ndio aliachia ngazi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...