Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akipimwa urefu na mtaalamu wa mfuko wa bima ya afya ya jamii leo katika viwanja vya shule ya Sekondari msakila katika Manispaa ya Sumbawanga ikiwa ni uzinduzi rasmi wa huduma hiyo ambayo inatolewa bure na mfuko huo katika kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko pamoja na kujali afya zao. Shirika hilo lipo katika maadhimisho ya miaka 10 ya utoaji huduma nchini. Katika hotuba yake fupi Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi waweze kujua afya zao na kupata ushauri ambao unatolewa bure. Aidha aliwataka viongozi wa mfuko kutoa elimu ya afya kwa wananchi katika maeneo yote nchini haswa katika maeneo ya pembezoni kusaidia kupunguza gharama za mfuko zinazosababishwa na maradhi yanayoweza kuepukika.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akipima mapigo ya moyo (BP). Vipimo vingine vinavyotolewa ni uwiano wa sukari mwilini na ushauri bure kwa wananchi watakajitokeza kupimwa.
Wananchi wengi wamehamasiku kupima afya zao kama inavyoonekana pichani
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...