Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akizindua rasmi Jukwaa la Uchumi wa Kijani, litakaloendelea kwa siku tatu Mkoani Iringa. Uzinduzi huo umefanyika leo Mei 8, 2012, katika Ukumbi wa Shule ya Msingi Mtakatifu Dominic Savio, mkoani Iringa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Shule ya Msingi Mtakatifu Dominic Savio, baada ya kuzindua rasmi Jukwaa la Uchumi wa Kijani, Leo Mei 8, 2012, litakalofanyika kwa Siku tatu mkoani Iringa.
Msanii wa Muziki wa Asili na Mashahiri, Mrisho Mpoto, akighani maneno yake yenye ujumbe Kuhusu Utunzaji wa Mazingira, mbele ya mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Uchumi wa Kijani, uliofanyika Mkoani Iringa leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya Uongozi, baada ya kuzindua rasmi Jukwaa la Uchumi wa Kijani, mkoani Iringa leo.Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...