Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu akizungumza na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo,waandishi wa habari na viongozi wa dini katika kikao maalumu cha kuhamasisha watu kujiandaa na zoezi la sensa ya watu na makazi kilichofanyika mjini Songea.Kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa,Sevelin Tossi na kushoto ni Mkuu Mpya wa Wilaya ya Songea,Joseph Mkirikiti.
Mwanasiasa mkongwe Nnchini,Alhaji Mustafa Songambele akizungumza wakati wa kikao cha sensa katika ukumbi wa Songea Club mjini Songea.
baadhi ya wajumbe waliohudhulia kikao cha uhamasishaji wa sensa ya watu na na makazi mkoani Ruvuma, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa,Mh. Said Mwambungu mjini Songea.PICHA NA MUHIDIN AMRI WA GLOBU YA JAMII.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 24, 2012

    Namkumbuka huyu Mzee Mstafa Songambele,Huyu ndiye aliye mtorosha Mwl. Julius Kambarage Nyerere, Kutoka Dar-es salaam Ya mama Bibi Titi Mohamed, Wakati Wazungu wanamtafuta Mwl. Nyerere Kwa kusababisha vuguvugu kali la siasa za kudai uhuru miaka ile ya sitini(60S) wakati mama yetu Bibi Titi Mohamed anapika mbombe za kienyeji pale Manzese na hela alizokuwa anapata anampa Mwl. nyerere aendeshee Siasa, ilikuwa karibu kabisa na ushindi wa kupata uhuru, wazungu wakaona wanataka kunyang'anywa tonge mdomoni ndipo walipo anza kumtafuta Mwl. nyerere, ndipo Huyu Mzee MStafa Songambele alipomchukua Mwl. Nyerere na kumtorosha mpaka Songea mkoani Ruvuma na akaenda kuficha kwenye eneo moja pale Songea linaitwa Majengo, sijui ni kwa siku ngapi lakini ndo ilivyokuwa.
    Tukitaka kujua zaidi kuhusu story za huyu Mzee na matukio haya ya kisiasa, hebu tumwombe mwandishi wetu wa blog hii pale Songea amhoji huyu Mzee kwa undani zaidi, utamsikia mambo haya.
    mimi naitwa Xavery komba-USA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...