Habari yako Ankal,
Naomba unifanyie msaada wa kuniwekea tangazo langu la kutafuta mchumba kwenye blog yako. Umri wa ninayemtafuta awe kuanzia miaka 34 mpaka 47. Awe anayependa na kujali familia. Mimi naishi nje ya nchi ingawa mwanaume aliye katika nchi yoyote anaweza kuniandikia. Mchumba ninayemtafuta awe na elimu ya chuo kikuu.
aliye tayari na nia ya dhati aniandikie kwenye barua pepe:
Mapema hayana elimu, unataka mwenye elimu ya chuo kikuu na wewe una elimu gani? au kuishi nje ya nchi ndiyo elimu yako. Taja pia umri wako.
ReplyDeleteanko huyu mdau ni wa kike au wa kiume?
ReplyDeletemdau znz-male
UTAPELI WA NIGERIA UNAANZA KUINGIA BONGO.
ReplyDeleteAhsante kwa taarifa,
ReplyDeleteTatizo kubwa la wasakaji wengi wanakuwa na mashariti na vigezo ambavyo havina mantiki, mtaji wala mshiko!
Mfano,
1.Wewe unatafuta mwenza aliyetayari kwa lolote kimaisha halafu unaweka shariti la Kigezo cha Elimu ya Chuo Kikuu, nani alikwambia kuwa kuendesha maisha lazima uwe na Shahada ya Chuo Kikuu?,,,wangapi wenye hizo Degree lakini miaka kibao wanahangaika kupiga photocopy na kuandaa CV wakiomba kazi hawapati?
JE UKO TAYARI UTAKUBALIANA NA MWENYE ELIMU YA CHUO KIKUU LAKINI HANA KAZI?
2.Nchi ya makazi, afadhali wewe umejitahidi kukubali mtu kutoka nchi yeyote ingawa wewe upo nje pia, pana wenzio walishatushukia humu Jamvini wakitoa mashariti kuwa Mwanaume naye awe anakaa huko Majuu!!!,,,sasa nani aliwaambia kuwa mume bora lazima atakuwa anatokea au anakaa huko Majuu?
3.Umri, nani alikwambieni ya kuwa Mwanaume anayefaa lazima awe na umri zaidi ya miaka 34?,,,ina maana wote walio chini ya miaka 34 hawana sifa za kuwa Wanaume bora?
Hamuoni wenzetu Wazungu huko kwao suala la ndoa halina vigezo vya umri unaweza kukuta Mume ana miaka 30 Mke ana miaka 50, au Mume ana miaka 57 Mke ana miaka 27.
Zindukeni, kwa sababu inaonyesha huu ugumu wa mashariti yenu ndio imekuwa sababu ya ninyi kukosa Kuolewa kwa muda mrefu hadi sasa.
kwanza wewe una umri gani, unafanya nini huko nje, una elimu kiasi gani, umewahi kuolewa, una watoto, je huko uliko umejiripua au bado ni mtanzania mwenzetu, uko tayari kuhama uliko na kumfuata mumeo aliko?
ReplyDeletejibu hayo kwanza hapa halafu ili tuone picha ilivyo.
mtanzania uk
Pole sana...Unapotafuta mchumba huna budi kusema wewe ni wa jinsia gani. Haitoshi kusema unatafuta mwanaume tu...Kuna ndoa za jinsia moja sasa hivi, hasa huko nje ya nchi.
ReplyDeletewewe ni mwanamke au mwanaume mbona maombi yako yako blank? una nia kweli wewe yaani??????????
ReplyDeleteSawa,
ReplyDeleteIla kwa Mashariti yako unaweza kumpata mwenye hiyo Shahada ya Chuo Kikuu lakini akawa 'bichwa nazi' yaani hana uwezo wa kiakili kwa kuendesha mambo ina maana hata ukimwachia Biashara ya Genge kuiendesha atashindwa!
Elewa ya kuwa kusoma sio kuelimika, pana ile akili ya asili ambayo ndio muhimu sana kwanza halafu ndio akili ya Chuo Kikuu !
Sasa si bora umpete mwanaume muuza Genge (asiye na Degree) ambaye ana akili za asili kuweza kuendesha maisha?
Bibie ,elewa Uadilifu wa Mwanaume au kutulia kwa mwanaume hakutegemei aina ya umri!
ReplyDeleteUnaweza pata babu babu akawa hajatulia au ukampata kijana akawa ametulia vizuri!