Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Joh Makini akitoa shoo kali kwa wanafunzi wa vyuo vitatu vya elimu ya juu vya mkoani Iringa (Tumaini,Mkwawa na Ruaha),waliofika kwenye Bonanza la Ufunguzi wa Mashindano ya Excel With Grand Malt 2012,lililofanyika kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Tumaini,Mkoani Iringa jioni ya leo.
  Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Joh Makini akiendelea kukamua kwenye Bonanza la Ufunguzi wa Mashindano ya Excel With Grand Malt 2012,lililofanyika kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Tumaini,Mkoani Iringa jioni ya leo.
 Wachezaji wa Timu ya Chuo Kikuu cha Mkwawa Mkoani Morogoro,Wakishangilia ushindi wao Pamoja na Muwakilishi wa Kampuni ya Bia Tanzania Kanda ya Nyanda za Juu Kusini,Masumbuko Changwe (wa pili kulia mwenye fulana ya rangi ya chungwa) wakati wa Bonanza la Ufunguzi wa Mashindano ya Excel With Grand Malt 2012,uliofanyika kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Tumaini,Mkoani Iringa jioni ya leo.
 Muwakilishi wa Kampuni ya Bia Tanzania Kanda ya Nyanda za Juu Kusini,Masumbuko Changwe (kulia) akikabidhi zawadi mbali mbali kwa washindi walioshiriki Bonanza la Ufunguzi wa Mashindano ya Excel With Grand Malt 2012,kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Tumaini,Mkoani Iringa jioni ya leo.
 Muwakilishi wa Kampuni ya Bia Tanzania Kanda ya Nyanda za Juu Kusini,Masumbuko Changwe akizungumza na Washiriki wa Bonanza la Ufunguzi wa Mashindano ya Excel With Grand Malt 2012,kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Tumaini,Mkoani Iringa jioni ya leo.
 Mtatibu wa Bonanza la Ufunguzi wa Mashindano ya Excel With Grand Malt 2012,Bw. Victor (kulia) amkaribisha Muwakilishi wa Kampuni ya Bia Tanzania Kanda ya Nyanda za Juu Kusini,Masumbuko Changwe kuzungumza na Wanafunzi hao kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Tumaini,Mkoani Iringa jioni ya leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 14, 2012

    Angalia utamu wa maisha kama haya, umma wote unafurahia maisha , matunda yote haya na yajayo ,wengine eti hawayaoni, kama kina John Mashaka, wanapowashambulia wawekezaji, eti wanapora ardhi au kelele za nchi imeuzwa !!!!! yaani siwaelewi-kama kweli maoni yenu yana uchungu wowote na nchi yetu. Wakati mwingine huwa najiuliza ,au kwa vile baadhi yenu mko nchi za nje , sasa kilichowabakia mioyoni mwenu ni kuponda tu kila jambo lifanyikalo huku bongo, kulaumu wawekezaji ambao wametuletea maendeleo makubwa na sasa tunajulikana sana hapa duniani, vitendo hivyo jamani acheni !! hamtutendei haki hata kidogo. hebu kwanza cheki hizo tabasamu za watu wa Iringa na jinsi walivyo vaa, wanamelemeta safi tena jeans za nguvu ,mpaka watoto wadogo wametoka kinoma, cheki hiyo nyumba ya mkulima tofari za kuchoma, wewe mashaka huko USA huna nyumba na kama unayo basi una deni la miaka 25. Iringa Oyee !! Ulaya Ziii . jamani acheni kutuzingua na maisha yetu ya taratbu bila pressure. be careful with your maoni ,yasigeuke uchochezi na kutuchafulia amani. Au tukupigie picha za India uone njaa na watu walivyochoka mbaya-linganisha na hizi sura za Iringa-halafu ni umri wa kazi wote from 20 to 40 years old. Bongo kumbe ni taifa la vijana watupu.I love Tanzania.Zebedayo mna Nasa.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 14, 2012

    mdau wa hapo juu uliyetoa comment zako nakuliza jambo mmoja tu je ni kweli hawa ndugu zetu wana furaha za dhati ndani ya mioyo yao? ni kweli watanufaika na hawa wawekezaji? jeulize maswali haya ndani ya moyo wako je wewe unaweza kunufaika na uwezekezaji huu? achaa hizo, ni wachache tu wajanja wanao nufaika na nani kwakwambia iringa hakuna pressure ya maisha, vijana wengi walio kuwepo nje wamechomoka katika mkooa huu wee acha hizoo

    kama nyumbani hakuna pressure jeulize kwa nini kila leo vijana na wa zee wanataka kuchomoa waje majuuuu kila leo walio wasomi na walala hoi kama mimi,na walio toka katika familila zinazojiweza na walala hoi kama mimi. acha hizoo mkuu kukurupuka ovyo na kumlaumu mashaka

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...