Hi Ankal.
Nipo na kwenye Basi la Shabiby kuelekea Dodoma,lakini mpaka sasa tupo hapa Maeneo ya Kibamba ambapo kuna ajali imetokea na kusababisha msongamano wa magari na kupelekea kuwa na line mbili mpaka tatu zote za kwenya upande mmoja (kuelekea moro).
Hivyo hakuna kupishana tena kama barabara zetu zilivyo na msongamano unazidi kuwa mkubwa,tunaomba uliwasilishe hili kwa wahusika ili waweze kulifanyika kazi haraka iwezekanavyo maana hali ni tete na hakuna askari Polisi wa usalama barabarani hata mmoja kwenye eneo hili.
Mdau J.J
kwa nini kumekuwa na line tatu badala ya mbili. Sasa hata kunasua tutaanzia wapi. Wote waliotanua na kuifanya hiyo ya tatu niwakute mahakamani leo leo.
ReplyDeleteNa bado itaendelea kutisha foleni za Morogoro road,Magufuli akisema ukweli anaonekana hafai hafikirii watu huyu bwana magufuri ndiye pekee atakayeweza kuondoa tatizo hili tumpe nguvu barabara haina hata njia mbadala,nyumba zimesongamana karibu na barabara hakuna hata mipango ya kuipanua hili tatizo linazidi kubwa sana na litatisha
ReplyDeleteDAWA YAKE POLISI WAGOME NA MUACHWE HAPO HAPO. HALI HIYO HUTOKEA MARA NYINGI, WATU BADALA YA KUSUBIRI SULUHU WANAJIFANYA KUWAHI NA KUISHIA KULETA MSONGAMANO USIO NA SULUHU!
ReplyDeleteHapo ajali,likibomoka je??
ReplyDeleteinakuaje kusiwe na mbadala---hili ni tz tu..niko china;wao sehemu kama hiyo wanaweka madaraja matatu na tunnel...wakijua dharula inaweza kutokea wakati wowote na mbadala unakuwepo!...leo daraja la ruvu likibomoka maisha tanzania yanasimama---mbadala wa bagamoyo baaadoo kufika kiwango