Mtoto wa ajabu amezaliwa katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma, mjini Songea, ambapo maumbile yake ya sehemu za siri  ya jinsia tofauti yako kichwani na sehemu zingine mbili ziko sehemu za kawaida.


Mtoto huyo amehifadhiwa katika chumba cha uangalizi maalumu katika hospitali hiyo, kwa lengo la kujaribu kupunguza msongamano wa watu ambao wamekuwa wakimiminika kumshuhudia.


Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali hiyo,  Dkt Mathayo Chanangula, alisema mtoto huyo alizaliwa Aprili 25, mwaka huu, saa saba mchana akiwa na uzito wa kilo 1.9 licha ya kutimiza miezi tisa ya kuzaliwa.


Dkt Chanangula alifafanua kuwa kwa kawaida mtoto anatakiwa kuzaliwa na uzito wa kilo 2.5. Pia alieleza sababu za kitaalamu zilizosababisha mtoto huyo kuzaliwa katika hali hiyo kuwa ni unywaji wa dawa zisizostahili kwa mama mjamzito kabla ya kutimiza miezi mitatu ya ujauzito.


Mtoto huyo kila anaponyonya, sehemu hiyo za siri ya jinsia ya kiume iliyo kichwani kwake inasimama kama vile anataka kujisaidia haja ndogo.


Naye muuguzi mkunga wa hospitali hiyo, Philomena Mwingira, alisema mtoto huyo amezaliwa akiwa na maumbile yasiyo ya kawaida, hivyo hawawezi kumuacha nje badala yake wameamua kumhifadhi katika chumba maalumu na kwamba wanaendelea kumfariji mama huyo kukubaliana na hali hiyo.


Wazazi wa mtoto huyo, Stumai Ausi na Abdallah Saidi, wakazi wa Msamala mjini Songea, wameiomba jamii na wataalamu mbalimbali kuwasaidia kumaliza tatizo la mtoto wao ili aweze kurejea katika maumbile yake ya kawaida.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 06, 2012

    ka michuzi mi kwa utaalam wangu mdogo nafikiri hiyo sio madawa kama doctor alivyosema , walikuwa twins lakini formulation ya huyo mwingine haikuwa kamili ndio maana akajiunga na mwenzake, ni hayo tu

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 06, 2012

    This looks like Anencephaly to me, which is basically the abscence of large part of the skull and brain,they also tend to have heart defects.
    Causes;
    1,Upper part of the neural tube fails to close, mainly due to enviromental toxins, including drugs and low folic acid during the pregancy, crucially during the first 12 weeks.

    2,Giving a pregnant woman any antifolate medication during the first 12 weeks of pregancy is a recipe to disaster; ie SEPTRIN which has sulfamethoxazole and Trimethoprim, the latter is an antifolate.

    Treatment; None available, supportive.

    Prevention; Give folic acid 400mcg once a day to all pregant women at booking to at least 12 weeks of pregancy,ideally folic acid should be started before the woman is pregant, increase the dose to 5mg once a day if a woman has KIFAFA (Epilepsy), OBESE, or has a previous history of giving birth to an anencephaly child or spina bifida.

    NOTE WELL:My explanation is just a summary, based on what I have seen on the clip.

    Dr Gangwe Bitozi, Mamtoni.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 06, 2012

    mwisho wa sura zetu dunian.its evolution tyme tjiandae

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 06, 2012

    08.44PM
    Sorry for the TYPO, Pregant should have been Pregnant.
    Dr Gangwe Bitozi, Mamtoni.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 06, 2012

    kwa. vile serikali kupitia afya na ustawi wa jamii haitamsaidia huyu mtoto, wanajamii tujitokeze kumdsidia afike muhimbili au ccbrt. kwenye wataalam waweze kurekebisha hali mapema. nina amini akichelewa kupata tib sahihi mapema kazi itakuwa ngumu na gharama itakuwakubwa zaidi
    ..

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 07, 2012

    Mdau wa Sun May06,08:49:00
    Wacha ujinga ww utakuja kusema nini mwanao akiwa kama hivyo au ahata ww mwenyewe maana hujafa hujaumbika.
    Anyway,khs hii hali ya huyu mtoto mtu yoyote ambae amepata kusoma medicine hata bachelor tu si lazima awe Gynacologist anaweza kufaham kwamba it is neural tube defect kama alivyoeleza daktari ingawa daktar alipata tabu kulifafanua tatizo vzr kwa lugha yakawaida ili mtu asiekua na ufahamu wa maswala ya tima aweze kuelewa.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 07, 2012

    Mwenyezi mungu mwenyewe ndie mjuzzi , hizo ni kudra zake analolipanga liwe basi huwa,sio dawa wala nini, huumba mwenyewe ajuwavyo, kwa hiyo mama na baba mzazi muwe na subira na mushukuru kwa kile alichokupeni mwenyezi mungu na yeye ndio muweza na wala musikufuru kwa hilo.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 07, 2012

    I like Africans we don't like to take responsibility every accident, every kifo all magonjwa no kupenda kwa Mwemyezi Mungu. I believe in God but asking why is one of the Best God given gift which sets us apart from other creatures

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 07, 2012

    Huo ni ujumbe mahsusi kwetu wanadamu kutoka kwa muumba wetu. Kwa wale wanaoamini hivi hamjawahi kusikia kuwa kuna watu watafufuliwa sehemu za siri zikiwa kichwani sijui usoni mwao? Mfano ndio huu, hasa wale wazinifu wa kisiri siri wale watafufuka na sehemu za siri zikiwa zimeota usoni/kichwani. Mungu mwenyewe ndie anaejua.

    Na kuna watu watafufuliwa wakiwa na sura za wanyama kulingana na matendo yao. Kuna mtoto amezaliwa Tanga hivi karibuni akiwa na sura ya mnyama.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 07, 2012

    Huo ni ujumbe mahsusi kwetu wanadamu kutoka kwa muumba wetu. Kwa wale wanaoamini hivi hamjawahi kusikia kuwa kuna watu watafufuliwa sehemu za siri zikiwa kichwani sijui usoni mwao? Mfano ndio huu, hasa wale wazinifu wa kisiri siri wale watafufuka na sehemu za siri zikiwa zimeota usoni/kichwani. Mungu mwenyewe ndie anaejua.

    Na kuna watu watafufuliwa wakiwa na sura za wanyama kulingana na matendo yao. Kuna mtoto amezaliwa Tanga hivi karibuni akiwa na sura ya mnyama.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...