Da' Chemi Chemponda na mwanae  Elechi aliyelamba nondozzz  Chuo Kikuu cha Brandeis University, Marekani

Wadau,  Da' Chemi Chemponda anafurahi kutangaza kwamba manae Elechi Henry Kadete amekula nondozzz ya  Bachelor of Arts' kutoka Chuo Kikuu cha Brandeis University, Waltham, Massachusetts, Marekani.  Major yake ilikuwa ni Business.  Sherehe ilikuwa jumapili iliyopita. Kweli safari ilikuwa ndefu na kulikuwa na matuta mengi njiani, lakini kafika. Baba yake marehemu Prof. Henry Kadete, lazima anatabasamu kutoka mbinguni.

Brandeis ni Chuo Kikuu cha Wayahudi, lakini wanapokea wanafunzi kutoka nchi mbalimbali na dini mbalimbali.  Imam alisoma sala ya kufungua sherehe. Baadaye Rabbi wa Kiyahudi, na Padre wa Kikristo walitoa sala za kufunga sherehe.
Hongera Elechi!

L-R Dr. Aleck Che-Mpomda (babu), Da' Chemi Chemponda,  Elechi, Camara (kaka), Malaika (mama mdogo) na Mrs. Che-Mponda (bibi)  Watoto wadogo ni watoto wa Malaika. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 25, 2012

    wanafanana midomo..hongera !

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 25, 2012

    Wow hongera sana mama na mtoto na umshukuru Mungu kwa wema alo kujalia kumtuza Elechi mpaka sasa amepata degree yake. Hongera kwa babu na bibi pia; a very touching family nimewapenda. Count yourself very lucky to have both parents at your side.bll

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 25, 2012

    hongereni sana, babu na bibi huwa wana uhusiano mzito sana na wajukuu zao, mara nyingine wazazi hatuwaelewi watoto wetu kama vile wazazi wetu wanavyowaelewa. Familia imeonesha upendo na umoja. Keep it up. Congrats young man God Bless you

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 25, 2012

    Safi sana!Naona familia imekamilika,,,Jitahidi Elechi.Kijana,umepiga hatua kimaisha Mwenyezi Mungu Akuongoze....

    Ahlam UK

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 25, 2012

    Hongera kwa kazi nzuri ya kulea Dada Chemi!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 25, 2012

    hii ni changamoto kwa watu tusio na nondoz huku majuu. kila mwaka time kama hizi za graduations kila kona roho huwa inaniuma hope na mie iko siku nitavaa joho

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 26, 2012

    Hongera.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...