Na Woinde Shizza,Arusha

JESHI la polisi mkoani Arusha limetangaza kumsaka popote alipo hadi uvunguni mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki,Joshua Nassar(26)alimaarufu dogo janja likimtuhumu yeye na wenzake kutenda kosa la kutoa maneno ya uchochezi katika mkutano wa chadema uliofanyika jumamosi iliyopita katika viwanja vya NMC jijini Arusha.

Kwa mujibu wa Naibu kamishina wa polisi nchini,Isaya Mngulu alimtaka mbunge huyo kujisalimisha polisi hadi leo saa 12 jioni na baada ya hapo litaanzisha msako mkali wa kumkamata popote alipojificha,baada ya jitihada za kumtafuta kupitia simu yake ya mkononi  kuwa kushindikana baada ya kuwa imezimwa.

Mnguli alisema kuwa pamoja na kumsaka mbunge huyo,polisi  inawahoji makada kadhaa wa chadema ,akiwemo Ally Bananga aliyehamia chadema akitokea ccm,mwenyekiti wa Bavicha Taifa,John Heche  na Alphonce Mawazo ambaye pia amejiunga na chadema akitokea ccm.

Alisema kuwa watuhumiwa hao kwa pamoja walitamka maneno ya uchochezi yanayohatarisha uvunjifu wa amani na kuyataja  baadhi ya maneno hayo kuwa ni kutaka mikoa kadhaa ijitenge kama sudani kusini.

Aliyataja maneno hayo kuwa ni’’iwapo polisi haitawakamata watuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa mwenyekiti wa chadema kata ya Usa River,Msafiri Mbwambo,mkoa wa Arusha na baadhi ya mikoa kanda ya ziwa itajitenga kama Sudani kusini  na kwamba Rais Kikwete hata kanyaga Arusha.

Maneno mengine ni Ridhiwan Kikwete anawapenzi wengi wa kike ambao amekuwa akiwatambulisha kwa baba yake(kikwete) na Kikwete amekuwa akiwateua na kuwapa nyadhifa muhimu serikalini na kuifanya serikali ya Kiswahiba.

Katika hatua nyingine jeshi la polisi limefanikiwa kuwatia mbaroni na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa 7 wakiwemo watatu waliohusika na tukio la kumuua kwa kumchinja kama kuku  aliyekuwa mwenyekiti wa chadema kata ya Usa River, Msafiri Mbwambo lililotokea  April 27 mwaka huu wilayani Arumeru.

Mngulu aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni,Daudi Mkubwa,Mathias Kurwa na Said Mkwela ambao wote ni wakazi wa mkoani Arusha.


Alisema kuwa polisi ilifanya uchunguzi wa  matukio mengine  kadhaa ya mauaji  likiwemo tukio la kifo cha Matha Joseph (75)mkazi wa Nkoarenkoli wilayani Arumeru aliyeuawa kwa kupigwa na mawe kicha kuchomwa na moto kwa imani za kishirikina na tukio la kifo cha Noel Eliona Manang (25)mkazi wa Singís wilayani Arumeru aliyeuawa ka kupigwa risasi baada ya yeye na wenzake kuvamia shamba la mwekezaji la Mito miwili.

Alisema kuwa katika matukio hayo polisi ilifanikisha kukamata watuhumiwa 12 ambao kwa pamoja walihojiwa na saba kati yao walifikishwa mahakamani wakiwemo watatu waliohusika na tukio la kifo cha Matha Joseph aliyeuawa kwa imani za kishirikina kwa kuchomwa na moto na mmoja ni mlinzi  anayehusika kumpiga risasi Noel Manang baada ya marehemu kuvamia shamba la mwekezaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 07, 2012

    Jamani hivi wanasiasa wengine vichwa vyao viko sawa kweli, hivi wanafikiria siasa za uchochezi ndizo zitawawezesha kuongoza nchi, kwa kauli zao za kutisha wanaanza kutuonyesha wao ni watu wa aina gani wakija shika madaraka ya kuongoza nchi, lakini pia wasisahau kwamba kuna watu wamekula kiapo cha damu cha kulinda nchi na katiba yake, watutangazie sera zao lakini si kutaka kutuharibia nchi, Sudani kusini walimwaga damu. kama wanataka kujitenga waanze kwanza wao kumwaga damu na si kutuharibia tanzania yetu, siasa au uongozi haupatikani kwa matusi, vitisho na siasa uchwara. Mungu ibariki Tanzania na wapenda amani.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 07, 2012

    Hii kufuatilia vitu vidogo vidogo ndiyo maana Watanzania tunadhani kuwa Serikali inaipendelea CCM. Mngekaa kimya na kufanya uchunguzi kwanza hii habari ya kuwa kila kukicha viongozi wa Chadema wana kesi inaleta picha mbaya. Wenzenu huwa wanangoja mpaka mambo yaive ndiyo wanaingilia kati, siyo tu mtu ( kiongozi) anabwatuka kutaka umaarufu tayari anatafutwa na polisi, mnatuharibia sisi wenzenu ambao kwa kweli tunaitakia heri CCM.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 07, 2012

    Waheshimiwa Dr. Slaa na Mbowe chonde chonde jitahidini sana kuwawezesha na kuwafundisha vyema mafunzo ya uongozi bora wabunge wetu haswa hawa vijana kwa kuwa sasa wao wameshakuwa viongozi wa wananchi na wanatakiwa wawe mfano wa kuigwa sio matusi na mambo ya kiuni. Uvumilivu, staha, na uchaguzi wa maneno katika mihadhara ni msingi bora wa mawasiliano. Pia sisi tumewachagua kutuwakilisha bungeni na sio lupango.
    Alex bura, dar

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 07, 2012

    DUH... KAMA MANENO HAYA NI YA KWELI BASI HUYU KIJANA MWENZETU KAZIDI MIPAKA, KUMOSOA RAISI KUPO ILA KWA HESHIMA NA TAADHIMA. INASIKITISHA INAPOFIKIA WAKATI MTOTO AMBAYE RAISI ANAWEZA KUMZAA ANAROPOKA MANENO YASIYO NA HESHIMA...HII HATARI KABISA

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 07, 2012

    Watanzania mtajuta indapo mtawakabidhi Hawa wahuni nchi kuingoza.
    Si tupo ?

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 07, 2012

    yaani niliposoma tweet ya haya maneno nikasema nakupenda kote demokrasia lakini huyo dogo kabugi stepi. Dogo unaanza kuwaharibia wenzako maana hapa sasa watu wataanza kuwaamini wale wanaosema kwamba Chadema ni chama cha kanda ya kaskazini

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 07, 2012

    wanalewa sifa tu wahuni hawa!mi siwapendi hata kidogo!kilijifanya kitoto cha mchungaji hamna lolote!mchungaji ni mzazi wako wewe huna mpango!unafikiri sifa hzo zitakufanya uwe kama zito au mnyika??hovyoooooo!
    Cc wote tunataka mabadiliko lakini c usudani kama unafikiri sudan wanafaid hamia huko...
    Asseeeeee!
    By mkinga halisi!

    ReplyDelete
  8. Siasa ya vyama vingi ina faida na hasara zake.

    ReplyDelete
  9. hiyo inaitwa free speech supression jeshi la polisi linapotaka ku control maneno ya wanasiasa kwenye majukwaa ni vita ambayo ni ndefu na haina mwisho maneno ya majukwaani ya wanasiasa yaachwe kwenye majukwaa ya siasa kwani ni siasa tu jamani

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 08, 2012

    kunya anye kuku akinya bata kaharisha... mmemsahau lusinde sio? angekuwa ni mchadema mngepiga kelele mbona hatukuona yale matusi aliyoyaporomosha pale arusha humu ndani? michuzi uwe unalenga kotekote kama aljazeera sio upendeleo hapa si hii ni blog ya jamii? au ni jamii ya watu fulani?

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 08, 2012

    Tatizo huyu mtoto hajakomaa,yaani(imature) kwasababu sisi watu wa chadema hatutaki kuigawa Tanzania, sisi tunataka kuitawala Tanzania yote, hata akimuuliza mwenyekiti mh. mbowe utamsikia hivohivo, inatakiwa akalishwe chini afundwe kama mwali, labda ataelewa nini tumemtumakufanya kule Bungeni, sisemi watu waendelee kuuwawa hapana, bali twende polepole siyo kwa speed hivyo tusije iangusha Chadema yenyewe, sawa jamani.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 08, 2012

    Polisi acha hizo njaa zenu....huyu dogo anawachokoza nanyi mnachokozeka kama machizi... kazi mnaijua tunawaaminia msitafute sifa kupitia mgongo wa huyo dogo...Kichaa akikuvua nguo unachutama sio kumfukuza ukiwa uchi....Chadema ni damu changa bado inachemka ...nyie tulia kudogo angalieni mchezo..msikurupuke kufukuza vichaa

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 08, 2012

    CHADEMA KUWENI MAKINI. MTUJIHARIBIA WENYEWE. TUNATAKA MAENDELEO HAYA MAHADHARI KILA KUKICHA NI KUTENGENEZA BOMU.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 08, 2012

    Mbona yale ya Mh. Lusinde hamyasemi jamani? Pamoja na yote yale aliyoyasema jukwaani bado hamkumchukulia hatua!

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 08, 2012

    Huyu Joshua Nasari hana akili hata kidogo. Amekwisha sababisha watu kuuliwa na mashamba ya watu kuharibiwa, kwa kutangaza eti sasa "ruksa" watu kuvamia mali ya watu wengine. Tuchukue mfano wa Dolly Estate ambayo inawaajiri wazawa zaidi ya 1,000 (directly and indirectly). Dolly Estate ilikuwa inamilikiwa na Walowezi tangu 1902. Familia ya kwanza iliwauzia familia ya pili miaka ya karibuni. Nakumbuka kabisa kuwa Mwalimu Nyerere alikataa kuitafisha Dolly Estate 1970 kwa kuwa ilikuwa "model farm" ambayo ilikuwa ikitoa huduma za kijamii kwa wenyeji wa Usa River. Leo hii mhuni kama Nasari anawachochea wananchi wakateketeza mali na vitu vya watu hao ambao wao na wazazi wao wamezaliwa Tanganyika/Tanzania! Lakini Nasari ajue Mungu atamwadhibu hapa duniani na kesho mbele ya haki kwa kuchochea chuki za kishenzi kabisa.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 08, 2012

    HAPA SIO MATUSI SWALA LA KULETA SERA ZA KATAKA KUITENGA NCHI NA KUIGAWA LIZINGATIWE KABISA NA HAKUNA LINALO ZUNGUMZWA BURE KUNA KITU CHA SIRI VIJANA NI KAMA WATOTO HUROPOKA WANAYO SIKIA TOKA KWA WAZAZI. JESHI LA POLIS FANYENI HARAKA.ETI MAFANIKIO YANA KUJA MPAKA TUPIGANE VITA WAPI NIGERIA YA SASA WAPI IVORY COAST,WAPI CHALES TYLOR NA JESHI LAKE LA VIJANA IPO WAPI LIBERIA YA SASA???

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 08, 2012

    Chadema waache Ujinga wao huko huko Arusha wasituletee vita sasa.

    Tunataka Wanasiasa wanaotumia 'MEZA' kwa 'VIKAO' na 'KALAMU' kwa 'KARATASI' badala ya VURUGU NA UCHOCHEZI BILA SABABU.

    Masuala ya Kuyumba ki Fedha na Kiuchumi Duniani matatizo yake yanatutosha ni muda wa kuyatatua na hatuna nafasi VITA KULETWA NCHINI KUPITIA TIKETI YA CHADEMA !

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 08, 2012

    Hawa 'baadhi' ya Chaedema kwa Staili yao ya Siasa watafanya Chadema nzima isiwe na sifa za Kupewa Utawala.

    Hivi hamuoni tofauti ya Siasa kati ya Siasa za Chadema YA Arusha na Chadema ya Dar?

    Siasa anazoleta JOSHUA NASARI na GODBLESS LEMA ni sawa na aina ya Siasa Makini ya Mhe.ZITTO KABWE na Mhe.HALIMA MDEE?

    Kwa mtaji huo wa Siasa za machafuko NG'O hatuwapi Mamlaka ya Utawala !

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 08, 2012

    Wadau, sera ya kyadema inajulikana: 1. Watavunja muungano wa Tanzania. 2. Wataleta utawala wa majimbo na ukabila. 3. Mhimili mkuu wa utawala wao utakuwa ni udini. Kwa hivyo lazima tupambane nao by any means necessary!

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 08, 2012

    Joshua Nasari sio kosa lake !

    Ilibidi Uongozi wa Juu wa Chadema umpatie Semina Elekezi kabla ya kukurupukia Madaraka,,,hivi Makada wa Chama wanakazi gani?

    Hamfanyi Semina za ndani za Uelewa wa Kisiasa?

    Vyama vingine na Kanisani vinatoa Semina ninyi CDM je?

    Mnaona sasa Dogo anayakoroga?

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 10, 2012

    Huyu dogo nashawishika kusema amepita ubunge sababu ya chama, sioni kama ni mwanasiasa hodari "jembe" kama mh john mnyika, halima mdee, tundu lissu na zitto kabwe.. Dogo hajui siasa which means hajui ni dhamana gan kabeba kwa wana arumeru, chama chake na TZ kwa ujumla..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...