Na Woinde Shizza,Arusha

Serekali ya LIBERIA imepokea msaada wa mkopo wa jumla ya dola milioni 46.50 kutoka Benki ya maendeleo ya Africa AFDB ambayo inalenga katika kuingia mfuko wa kilimo pamoja na uhifadhi wa chakula.

Mkopo huo ulishuhudiwa na kutiwa saini makubaliano yaliyofanyika katika mkutano wa  AFBD unaondelea jjijini hapa na kamishna wa tume ya uwekezaji toka nchini Liberia Natty B. Davis pamoja na kutiwa saini na makamu wa Raisi wa sekta ya uwekezaji nchini LIBERIA Kamal Elkeshen.

kamishna wa tume ya uwekezaji toka nchini Liberia Natty B. Davis baada ya kutia saini makubaliano hayo amesema kuwa msaada huo wa mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Africa ni wa mara ya kwanza kwa nchi yao toka walipoanzisha ushirikiano na AFDB

Alisema kuwa anapenda kuiambia sekretariti ya Benki ya Maendeleo ya Africa AFDB kuwa msaada huo wa mkopo utaisadia serekali ya Liberia katika sera zake ilizonazo za kuwasaidia wananchi wake waishio vijijini.

Katika mkopo huo uliotolewa na Benki ya Maendeleo Barani Africa wamengia makubaliano na Liberia kuweka uhusiano mzuri na wafadhili wa jumuiya za kimataifa ambapo itaisaidia nchi hiyo kujiondoa na umaskini hasa hasa katika sekta ya kilimo pamoja na uhifadhi wa chakula

Pamoja na mkopo huo kulenga kusaidia usalama wa chakula nchini LIBERIA pia msaada huo umelenga katika sekta ya wakulima wadogo wadogo katika ukulima hadi uzalishaji hii ikiwa na lengo la kuondoa tatizo la jira sambamba na kuweka uhai wa kilimo cha vijijini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...