Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika mdahalo wakati wa Kongamano la Kimataifa la Uchumi kwa Afrika, akiwa na viongozi wengine wa nchi mbalimbali waliohudhuria.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa,Bw. Koffi Annan walipokutana katika hoteli ya Sheraton jijini Addis Ababa ambako wote walihudhuria Kongamano la Kimataifa la Uchumi kwa Afrika.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bishara la Kimataifa - World Trade Organisation (WTO)- Bw Paschal Lamy walipokutana kwa mazungumzo katika hoteli ya Sheraton jijini Addis Ababa ambako wote walihudhuria Kongamano la Kimataifa la Uchumi kwa Afrika.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akisalimiana na Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Canada Bi. Berly Oda walipokutana kwa mazungumzo katika hoteli ya Sheraton jijini Addis Ababa ambako wote walihudhuria Kongamano la Kimataifa la Uchumi kwa Afrika
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Nigeria Mh Goodluck Jonathan baada ya kuhudhuria dhifa ya kitaifa waliyoandaliwa na mwenyeji wao Waziri Mkuu wa Ethiopia Mh Meles Zenawi jijini Addis Ababa Alhamisi usiku. Kulia kwa Rais Kikwete ni Waziri wa Fedha wa Nigeria Bi.Ngozi Okonjo-Iweala ikiwa ni kielele cha Kongamano la Kimataifa la Uchumi kwa Afrika.PICHA NA IKULU.
jamani harakisheni hilo vazi la kitaifa. Mnaona wenzetu bila hata kutaja ni wa wapi wanaonekana.
ReplyDeleteWnaigeria wananifurahisha wanavyovaa, hasa kina mama. Halafu huyu Rais wa Nigeria anavaa nguo za kihindi. inafurahisha sana hawa watu wana misimamo katika mavazi, sio kama hawana suti lakini utamaduni wao wa mavazi wanauheshimu sana.
ReplyDeleteHuyo Waziri wa fedha wa Nigeria kama usingetujulisha.Nilijuwa ni mama Salma,maana wanafanana kweli kweli,,mavazi yake na miwani,,ama kweli Duniani wawili wawili.
ReplyDeleteAhlam UK