Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda na Ujumbe wake wakioneshwa na Ndg. Koichiro Maeda Mkurugenzi wa Makumbusho ya Hiroshima mchoro wa madhara ya Bomu la Atomic lilirushwa katika Mji wa Hiroshima wakati wa vita kuu ya pili mwaka 1954 jinsi mji huo ulivyokuwa siku hiyo baada ya kulipuliwa.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwa katika Picha ya Pamoja na Mzee. Keijiro Matsushima shuhuda aliyenusurika katika Bomu la Atomic lilisambaratisha mji wa Hiroshima.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akisaini kitabu cha Kumbukumbu na kuandika ujumbe wa kulaani matumizi ya silaha za Nuclear baada ya kumaliza kutembelea makumbusho yenye picha na matukio yaliyotokea siku bomu la Atomic lilivyo sambaratisha mji wa Hiroshima.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimkabidhi Ndg. Koichiro Maeda Mkurugenzi wa Makumbusho ya Hiroshima ujumbe kutoka kwa timu ya wabunge aliongozana nayo ziara hiyo wenye kulaan matumizi ya silaha za Nuclear Dunian.
Jengo pekee lililosalia baada ya bomu la Atomic kutoa na kusambaratisha mji wa Hiroshima. Hivi sasa jengo hilo limehifadhiwa kati hali yake kwa kumbukumbu ya tukio hilo.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda na Ujumbe wake wakitizama picha iliyopigwa baada ya kulipuliwa Mji wa Hiroshima mwaka 1945 na Bomu la Atomic. Picha hiyo ilipigwa tarehe 6 agosti 1945 mda mchache baada ya kulipuliwa kwa mji huo.
Mhe. Tundu Lissu akiuliza swali kuhusu mda uliochukua kuujenga upya mji huo
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimsikiliza kwa makini mmoja wa mashuhuda aliyenusurika katika Mlipuko wa Bomu la Atomic Mzee. Keijiro Matsushima siku lilipoteketeza mji wa Hiroshima tarehe 6 Agosti 1945 ambapo zaidi ya watu 66,000 walifariki 92,000 hawakujulikana walipokuwa mpaka sasa na 129,558 walijeruhiwa vibaya. Mzee Matsushima alikuwa na umri wa miaka 16 siku hiyo na siku ya mlipuko alikuwa darasani km 2 katika chuo cha Hiroshima Technical College ambapo katika darasa alilokuwapo wanafunzi kadhaa walifariki pia kutokana na mionzi mikali ya bomu hilo. Hivi sasa Mzee Matsushima ana miaka 83. Kushoto kwa Mhe. Spika ni Mhe. Godfrey zambi na Mhe. Anne Kilango Malecela.
Shuhuda aliyenusurika katika Mlipuko wa Bomu la Atomic Mzee. Keijiro Matsushima akiwaonesha katika ramani waheshimiwa Wabunge na Mhe. Spika eneo alipokuwa siku bomu linalipuka na sehemu bomu lilopolipukia.Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 17, 2012

    Hongereni wwajapan kwa kuwaonesha viongozi wetu umuhimu wa makumbusho za taifa. Sidhani kama kuna hata mmoja kati yao ambae amesha wahi kutembelea Makumbusho za Tanzania, na Wageni wakitaifa wanao kuja TZ hawapewi nafasi ya Kuzitembelea Makumbusho zetu, hii inatokana na Viongozi wengi kuto kujua Umuhimu wa Makumbusho za Taifa, wanadhani kuwa makumbusho nisehemu ya kuhifadhi vitu vya zamazi tu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 17, 2012

    Naona kama nimesahau historia hivi vita ya pili ilikuwa mwaka gani? si 1945 au 1954 kama mlivyoandika? tujikumbushe historia tusiandike tu

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 18, 2012

    wewe ndio mbumbumbu kweli kama hujui vita vya dunia vilianza na kumalizika lini nenda google stupid kudesa tu basi ndio mmezoweya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...