Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kigali baada ya kupokelewa na Mwenyeji wake Spika wa Bunge la Rwanda Mhe. Rose Mukantabana (Kushoto). Mhe. Makinda yupo Kigali Rwanda kuhudhuria Mkutano wa Saba wa Maspika wa Mabunge wananchama wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika leo
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akizungumza na Mwenyeji wake Spika wa Bunge la Rwanda Mhe. Rose Mukantabana mara baada ya Kuwasili Mjini Kigali kuhudhuria Mkutano wa Saba wa Maspika wa Mabunge wa Nchi wananchama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika leo.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akipata maelezo ya awali kuhusu Mkutano huo kutoka kwa maafisa wa Bunge la Tanzania. Wa kwanza Kushoto ni Bi. Justina Shauri , Afisa Dawati wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Bunge la Tanzania na Ndg. Charles Mloka, Mkurugenzi wa Kamati za Bunge anayemuwakilisha Katibu wa Bunge katika Mkutano huo.
Mhe. Makinda na Mwenyeji wake wakiondoka Uwanja wa Ndege mara baada ya Kuwasili.Picha na Owen Mwandumbya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 07, 2012

    Inaonekana uwanja wa ndege wa wenzetu umetulia kweli kweli.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 07, 2012

    Wadau niliskia kwa kagame viongozi na serikali wanatumia gari za kawaida saana mbona hilo kama KILIMO KWANZA V8?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...