Hivi karibuni nimekuwa nikipokea malalamiko mengi ya kukatika mara kwa mara kwa umeme katika maeneo ya Kigamboni na Mbagala.
Matatizo haya yanatokana na sababu kuu mbili: Moja, miundombinu ya umeme kuzidiwa na mahitaji na pili, uchakavu wa miundombinu.
Kwa hivi sasa, watumiaji wa umeme wa Kigamboni, Mbagala na Mkuranga wanapata mahitaji toka kwenye kituo kidogo kilichopo Ilala. Umeme unaotoka kwenye kituo hautoshelezi mahitaji ya maeneo yote yaliyotajwa hapo juu. Hali hii imepelekea baadhi ya maeneo kuwa na umeme ndogo na baadhi ya maeneo kukatika hususan nyakati za usiku.
HATUA ZINAZOCHUKULIWA KUTATUA TATIZO HILI
Hatua za muda mrefu:: Tanesco inatarajia kujenga Sub-station kubwa maeneo ya Mbagala ambayo itahudumua maeneo ya Kigamboni na Mbagala. Kazi hii inatarajia kuanza karibuni baada ya kukamilisha zoezi la fidia kwa wananchi waliobaki.
Hatua za muda mfupi: Tanesco inaendelea na ukarabati wa mfumo uliopo ili uweze kuihimili mahitaji ya sasa. Katika wiki hii, Tanesco ilikata umeme tarehe 22, 24 na leo 27 kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni ilikufanya kazi hii. Kwa mujibu wa Tanesco kazi hii inatarajia kukamilika wiki mbili zijazo.
Naomba tuvute subira wakati Tanesco wanalifanyia kazi tatizo la umeme kukatika mara kwa mara.
Ahsanteni.
Dkt.Faustine Ndugulile
Mbunge Kigamboni
Mnalea vikundi vya udini vyenye malengo ya kuvuruga hili taifa. Wajinga wachache wasipewe nafasi. Hatuko tayari vikundi kama hivi kutuvuruga kwa lipi kwanza. Mmechoma kanisa, je leo hii msikiti ungekuwa umechomwa ingekuwaje. Msifanye jambo ambalo hamtaki kufanyiwa.
ReplyDeleteNdugulile pongezi kwa kazi yako nzuri kwa wananchi wakigamboni nimekusoma sana ninaikubali kazi yako!na pia ninakupa ushauri fanya kila njia uimarishe vituo vya polisi sbb watu wengi wanashindwa kuhamia kwa ajili ya usalama haswa sehemu ya tuangoma!Ardhi wamewaahidi watu miundombinu na usalama lakini wameshakula pesa wamejisahau sasa kazi niyakwako kaka sbb tunajuwa unapenda watu wako!
ReplyDeleteHongera ndugu mbunge ,naona unafanya kazi ya Tanesco kwani wao wachoka customer care hamna kabisa.Inatokea katizo kubwa kama hili lazima kuwe na taarifa maalum lakini kwa Tanesco hamna kitu kama hicho nakupongeza Mbunge kwa taarifa hii.
ReplyDeletesasa sijui wale ambao hawako kwenye mtandao tunawafikia vipi?
pia tutafurahi hukitupa maendeleo ya huu mradi wa ujenzi wa mji mpya wa kisasa maana wananchi tuko njia panda .
Mwisho ndugu Mbunge,tunaomba namba yako ya simu kwani tuna mengi sisi wanakigamboni ya kukueleza.
Tupo pamoja! - GGN
ReplyDeleteDr.Faustine Ndugulile
ReplyDeleteMbunge wetu ahsante sana kwa maelezo yako na jitihada zako kubwa kwa kututumikia sisi Wapiga kura wako.
Tatizo kubwa ni kuwa IMEJENGEKA DHANA YA KUWA WATU WANAOKAA MBAGALA NI MABWEGE,
-----------------------------------
1.MWANAMUZIKI DIAMOND ALIIMBA WIMBO WAKE WA MBAGALA NA KUWAPOTOSHA WATU WENGI WAKICHUKULIA KUWA MBAGALA NI SEHEMU YA CHINI KABISA YA KIMAISHA NA NI KUCHAFU KILA SEHEMU NI MAJALALA TU, KITU AMBACHO SIO KWELI KWA VILE PANA MAENEO MENGINE JIJINI DAR NI MACHAFU SANA MFANO KEKO, TANDALE, KIGOGO NA BUGURUNI ''''MBAGALA NI KUSAFI SANA '''''YEYE DIAMOND ALIIMBA KUTIMIZA MIZANI NA VINA VYA MASHAIRI YA WIMBO WAKE NA SIO HALISI ALICHOIMBA.
Kama maneno ya Msanii wa Muziki Diamond yana ukweli, mbona na yeye mwenyewe anakuja DAR LIVE ambayo ipo Mbagala kutumbuiza muziki na kustarehe?
2.NA NDIO MAANA (WENGI WASIOKUWA NA AKILI HUWA WANASITA KUTAJA AU KUJIBU WANAPOKAA KUWA WANAKAA MBAGALA WAKIULIZWA NA WENGINE KWA VILE WANAAMINI WAKISEMA WANAKAA MBAGALA WATAONEKANA WAO NI WATU WA CHINI KIMAISHA)!
-----------------------------------
SASA KAMTAZAMO HAKO POTOFU HAPO JUU KTK NDANI YA MISTARI NO.1 NA NO.2 NDIO KANAFANYA MAMLAKA NA WADAU WENGI KAMA HAO TANESCO KUJIAMINI NA KUIFANYA MBAGALA KUWA NI SEHEMU YA MABWEGE NA KAMA KICHWA CHA MWENDAWAZIMU KWA KUKATA UMEME MARA KWA MARA.
Ni mimi Mdau wa MBAGALA
Barron (Tajiri wa Mbagala) Mohamed.
mohamedtzn@AOL.COM
asante mheshimiwa kwa kazi yako nzuri ni kweli wala hili la kukatika umeme limekuwa kero sana bila hata ta kuwa taarifa husika.Tanesco ni wazembe sana wao wameshindwa nini kutoa taarifa kama hizi kwa wateja wao? Pia mheshimiwa tunaomba sana utusaidie wswala la miundo mbinu katika viwanja vya kibada,hakuna barabara kabisa na hela hizo tulichangia wakati tunanunua viwanja hivyo na mpaka leo pale block 19 eneo la nyakwale kuna makaburi mabayo hayajatolewa na viwanja hivyo watu waliuziwa kama eneo la makazi. Inamaana gani pale sharia ya ardhi inaposema mtu anatakiwa kueneleza kiwanja mndani ya miaka mitatu?Leo ni maka wa sita tangu viwanja vile viuzwe na haiwezekani kuendeleza kama kuna makaburi na hakuna barabara za kufika huko?
ReplyDeletetafadhali Mheshimiwa tunaomba ufuatilie swala hili kwani ni kero sana.
Wabunge wote wangekuwa kama huyu wa Kigamboni tungepiga hatua moja mbele, kwani kazi ya mbuge pia ni kuwa kiungo kati ya wapiga kura wake na serikali ama watoa huduma, hongera mkuu tupe na taarifa zingine za maendeleo kama afya, elimu na maji
ReplyDeleteasante sana mhe. Ndugulile sasa tunaona matunda yako mheshimiwa wakazi wa mwanamtoti tunafuraha sana kuona ujenzi wa Daraja na jinsi unavyoenda kwa kasi, hadi usiku ujenzi unaendelea mhe. Ongera sana Faustine Ndugulile.
ReplyDeleteGastor wa SAYARI MPYA MWANAMTOTI.
Mimi ni mkazi wa Kigamboni pia ,nachukua nafasi hii kukupongeza kwa hilo na nataka niwasaidie watu wachacha ambao hawajui kugoogle,nitaiprint na kwenda kuzibandika walau wasio na access na mtandao wazipate na kama mradi utakuwa danganya toto basi wawe na pa kuanzia.
ReplyDeleteNakupongeza Mh. kitu ambach nasita kuamini kuhusu mradi huo ni uongo uliokithiri!! nasema hivo kwa sababu sio kwamba umeme unakatika mara chache, kwa mfano wakaazi wa huku mbagala kiburugwa KILA SIKU LAZIMA UMEME WAKATE. Hata hapa muda huu tupo gizani pamoja na miundombinu finyu, kiukweli WAFANYAKAZI WA TANESCO KURASINI NI WAZEMBE SANA, HAWANA HATA LUGHA NZURI KWA MTEJA NA WAMEJISAHAU. Kwani hata ukitoa taarifa kuhusu hitilafu yoyote wanajibu kama wapendavyo hata kabla hawajafanya utafiti wa kiutaalam kujua tatizo ni nini.kuna matatizo specific apart from hilo la miundombinu finyu. if I could be their leader honestly I would reshuffle all customer care persons at kurasini plus mafundi. wameizoa kazi kiasi kwamba they really dont care!!!!
ReplyDelete