Na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imepiga marufuku mikusanyiko ya aina yoyote ikiwemo mihadhara ya aina mbalimbali ambayo haijapata kibali cha Serikali.
Akitoa taarifa ya Serikali,Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais ,Mohammed Aboud Mohammed amesema mbali na suala hilo,pia imewataka wananchi kuheshimu sheria.
Waziri Aboud amesema pia Serikali imeliagiza Jeshi la Polisi kuwatafuta na kuwafikisha katika vyombo vya sheria wale wote waliohusika na fujo zilizotokea jana na leo katika mji wa Zanzibar.
“Serikali inakemea vikali vitendo vyote vya hujuma na uharibifu wa mali zilizofanywa katika taasisi za umma,Dini na watu binafsi” Alisisitiza Waziri huyo.
Serikali imetoa mkono wa pole kwa wale wote walioathirika na vurugu hizo ikiwemo Taasisi na wananchi kwa ujumla na imeahidi kuchukua hatua kali dhidi ya wale wote waliohusika kufanya vurugu hizo.
Katika hatua nyengine, Waziri Aboud alisema Serikali inawaomba wazazi kuwadhibiti vijana wao kutojiingiza katika vitendo vya viovu ikiwa pamoja na vurugu,hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa atakayekiuka sheria na taratibu za nchi.
“Tunawaomba wananchi waendelee na shughuli zao kama kawaida na Serikali itaendelea kuhakikisha amani na usalama wakati wote” Alisema Waziri Aboud katika taarifa yake aliyosoma mbele ya vyombo vya habari katika studio za Shirika la Utangazaji Zanzibar.
Katika taarifa yake,wananchi pia wameombwa na Serikali kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kutoa taarifa za wahalifu na wale wote wanaotaka kuvunja amani katika jamii.
“Tunawaomba wananchi kushirikiana na Serikali kwa kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi pale ambapo itaonekana zipo dalili za uvunjifu wa amani katika maeneo yao” Alitoa wito Waziri Aboud.
Katika taarifa hiyo,Serikali imewakumbusha viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam na Jumuiya nyengine kufuata taratibu ikiwa wanataka kufanya mikutano au mihadhara inayojadili suala zima la kuandikwa kwa katiba ya Jamhuri ya Tanzania.
Awali, Waziri huyo alisema Serikali iliwaita viongozi wa uamsho kuzungumzia namna bora ya kufanya mikutano inayozungumza wanaotaka kuendesha mijadala ya katiba mpya kwamba watalazimika kufuata sheria na taratibu za Tume ya Katiba iliyoundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
iNGECHUKULIWAJE KAMA TAASISI FULANI YA KIKRISTU INGESIMAMA NAKUDAI UTANGANYIKA AU UZANZIBARI? MBONA MNALEA UJINGA.
ReplyDeleteMmm! tukiambiwa hii Zanzibar haina sheria ndio hivyo tena. Tume ya katiba iliyoundwa na Rais wa JMT ndio iongoze shughuli za jumuiya nyengine wakitaka kufanya mikutano na mihadhara yao.
ReplyDeleteSerikali sikilizeni raia wenu kabla mambo hayajakuwa mabaya mtakuja kujuta kama mnajiona mko na power sasa hivi watu wamechoka ninawapa nasaha mtanikumbuka!
ReplyDeleteMchangiaji wa kwanza anauliza ingechukuliwaje kama taasisi ya kikristu ingesimama na kudai utanganyika au uzanzibari?
ReplyDeleteMimi nasema tungechukulia kwamba wanataka kutuharibia nchi, ujinga ni ujinga tu bro. bila kujali ni nani anaeufanya.
Kama kuna mtu anadhani TZA ikiharibika ataweza kwenda kuishi ktk zile nchi amazo imani zetu zimetokea, ajue anajidanganya!
Sio SAUDI ARABIA, VATICAN wala ISRAELI wanakotaka ujinga!
Mimi nasikitishwa tu na serikali kupitia wizara ya mambo ya ndani kushindwa kuwachukulia hatua hawa UWAMSHO a.k.a BOKOHARAM.
Jukumu la kulinda usalama wa raia na mali zao ni la wiraza ya mambo ya ndani ambayo ni ya muungano sio ya SMZ. au jamani mmeshindwa kazi?
Mimi ni mwanasheria wa kujitegemea, nataka kujua hicho kikundi cha UAMSHO ni chama cha Siasa au ni nini, pia nataka kujua kimesajiliwa au la, na kama siyo chama cha siasa na hakijasajiliwa, hao viongozi wa Uamsho ni viongozi wa kikundi cha kihuni, na kinaonyesha kuchoshwa na AMANI iliyopo, dawa ni hao viongozi wakikundi ndo wakamatwe kabla hawajasababisha umwagaji damu na wawekwe kizuizini mara moja au wakitaka wasajili kiwe chama cha siasa hapo mambo yatawanogea hata mimi nitawaunga mkono, namna nyingine huwo ni UHUNI NA HATUWEZI KUFUGA WAHUNI, HII SIYO NCHI YA KIHUNI WAENDE KWA WAHUNI WENZAO SISI TUNATAKA KUISHI NA TUNAISHI MARA MOJA TU HAPA DUNIANI NA KWAHIYO HATUTAKI KUONDOKA HARAKA HAPANA, WAFE WAO SIYO SISI.
ReplyDeleteNaitwa Abdallah Juma-ughaibuni
Wengine inawauma wakiona wazanzibari wanadi nchi nyao.
ReplyDeleteHAKUNA SHERIA YA KUUMIZA WATU WENGINE KWA SABABU YA DINI YENU. MAWAZO YENU YASIWE KERO KWA WANANCHI WENGINE, SASA MNAVUNJA KANISA LIMEWAKOSEA NINI? MBONA HAO MLIOWACHOMEA KANISA HAWACHOMI MISIKITINI YENU? SIJUI MTASTAARABIKA LINI? NADHANI KUNAHITAJI NGUVU KUWAVUNJA VUNJA ILI MJIFUNZE NA MKAE KWA ADABU.
ReplyDeletemimi ni mwanasheria wa kujitegemea, na kweli bora ujitegemee mwenyewe mwanasheria makutu, na hata sijui nani atakaekubali umsimamie kesi yake, akili inaonekana ishapigwa na baridi yote imelala, ati me iko ughaibuni, upumbavu mtupu, bora uwo uwanasheria wako wa kujitegemea ukae uko uko ughaibuni kila wiki pesa za bure, mana nyie ndo wenye akili pumba hamfai kwa chambo wala kitoweo.
ReplyDeleteWewe Anoy wa Mon May 28, 02:29:00 AM 2012, kwa vile vikundi vilivyoleta mapinduzi kule Tunisia na Misri vilikuwa vimesajiliwa kisheria? Kwani vikundi vilivyoleta nchi Sudani ya Kusini vilikuwa vimesajiliwa na sheria za Sudani?
ReplyDeleteAkina mubarak na Gadaffi waliwaita watu kama hao wahuni, lakini wapo wapi? Huu sio wakati wa kuita watu wahuni. Huu ni wakati wa kuitana wahuni. Huu ni wakati wa kukaa chini na kutatua matatizo ya muungano. Kila mtu anajua kuwa muungano una matatizo lakini tunajifanya hatuyajui. Siku ambayo yatatukoea puani ndio tutajua.
Utasema huwezi kukaa chini na kujadiliana na wahuniu. Ule utawala wa Tunisia ulisema hivyo hivyo. Mubarak alisema hivyo hivyo. Gaddafi nae alisema hivyo hivyo? Lakini sasa wako wapi? Walioitwa "wahuni" ndo wameshika hizo nchi.
Mtu mhuni ni yule anayekimbia tatizo.
Mwanasheria wa kujitegemea loh! Ni bora ukaendelea kujitegemea,ndugu yangu, maana hakuna atakayekutegemea hata siku moja, kwa akili zenyewe hizo na uwezo wako mdogo wa ku-approach issues!
ReplyDeleteUnatutia aibu sisi wenzio tuliosomea fani hiyo. Nachelea kukuuliza hiyo sheria yako umeisomea kwenye Chuo gani. I better reserve my question and further comments!
You young boys knows nothing, just ignorant brats, ngojeeni 2015 ashike CHADEMA kama patakalika hapa. Ajali tu ikitokea binaadamu amekufa anasachiwa kabla ya kupewa msaada, pale ubungo gari la ngombe lilipata ajali, alikatwa mguu ngombe yuhai. Mnasema nini nyie mtachinjana wenyewe kwa wenyewe.
ReplyDeleteUzanzibar huu utakuja kuleta hathari kubwa sana.
ReplyDeleteUnajuwa kuna wakristo nao wapo tu wamenyamaza,inamaana tukileta udini na Usiasa ipo siku kwenye Mikoa ya Wakristo itakuwa na nchi za kikisto na mikoa ya waisilamu itakuwa na nchi za kiislam.
Pemba itakuwa nchi Unguja itakuwa nchi?
Mbeya itakuwa nchi ,Tanga itakuwa nchi?
Udini tu umewajaa na HAKUNA DINI BORA INAYOTEGEMEA SIASA.
Hivi kunawatu hawaangalii mbali na hata wanajaribu kudhani Mwalimu Nyerere alikuwa eti anajifanya ni Msomi?
Mwalimu Nyerere alikuwa msomi hakunaga.
ndiyo maana hatuuelewi muungano amabo yeye aliuweka kwa amani ya nchi yetu.
Ipeni Zanzibar miaka mitano ya kujitenga tuone kitatokea nini baada ya hapo?
Kwani hao UAMSHO ni chama cha siasa?mbona wanachanganya dini na siasa?
ReplyDeleteHatua za haraka inabidi zichukuliwe wakamatwe wawekwe kizuizini wakitoka wasajili chama cha siasa au waendelee kuhubiri dini .tusije tukakubali watu wachache wakatugawa kutokana na ujinga wao wa wakujazwa udini!
mnawaita watu wahuni wanao dai nchi yao iliyotekwa kiujanja ujaa hamnazo nyinyo wadanganyika daima mta danganyika unasema cha kimesajiliwa kwa mfano nzuri tu huko sudan ya kusuni, misri na tunisia watu wanataka kukomboa nchi yao katika mfumo kiristo hatutaki kutawaliwa na wakiristo
ReplyDeletena huyu aboud kunisiki itafika mwisho wake anajitapa tapa ovyoo kishatiwa mfukoni na kupewa pesa za ruzuku anavimba kichwa sasa.
ngojeni basi msubiri chama kisajiliwe,wadanganyika hatutaki sisi muungano hatuutapi tuachieni nchi yetu na huu uamsho tunawaamsha wazanzibari wote waamkee wajue maovu yanayotendewa kwa huu muungano.
watuchomee misikiti yetu kwani nchi yao hii, si wavamizi tu wamekuja katika nchi yetu mnawazimu sana nyinyi na huu ukiristo so ndo unaoleta utali na uhanisi katika nchi yetu na madawa ya kulevya na pombe mnadhani sisi tumechoma kanisa tu, kanisa ni chanzo za ufisadi na hatu taki sisi ufisadi tena katika visiwa hivi.
some historia baba wa kanisa na wala si baba wa taifa alijua wazi kwanza akituachia huru unguja na pemba tutajitawala wenyewe vizuri na bara mtakaa na ujinga wenu ndo kwa ufisadi wake akalaghai mwenzio lakini pia baba yetu wa taifa karume alikuwa hajalala si mjinga.
nendeni zenu tumeshachoka tunataka nchi yetu,
leo hii mnatembea kifua mbele kwa nguvu ya uislamu. baba yenu ya kanisa alifaziliwa, akalindwa na kubebwa kwa nguvu ya usilamu mpaka mkapata uhuru wa tanganyika some historia wewe siyo hii historia mnao wadanganya watu na watu sasa wamesha amka wajalala tena wapuuzi na wapumbavu ndo nyinyi wadanganyika siyo tena wazanzibari toka enzi na enzi tuko macho tulishaamkaa soma historia nyinyi wajinga mtajua na kutahayari na wengi mnaijua ndo maana mnataka kutawala kwa chuki na kutaka kuwabatiza watu kwa kilo ya dona lakini hatubatizikiii
Hivi wazanzibari wanavyodai kujitenga na nchi yao,swali ni JE wataweza kujiendesha kimaisha wenyewe?Kwanza ni wavivu tupa, waliozowea kucheza bao na kupiga bla bla jioni na kunywa kahawa kwenye vigenge! Pili ni sio watu wa kujituma wamezowea kukaa na kupewa,Yaani ni wachache sana wanaojituma! Ukiangalia watu wengi zanzibar wanaoendesha biashara na maendeleo ni watu waliotoka bara na sehemu nyingine za nchi!Na umeme na vyakula vingi vinatoka BARA! Sasa JE wakitaka kujiendesha wenyewe bila ya watu kutoka BARA wataweza?Hao ni mamwinyi waliozowea kukaa na kupewa na kufanyiwa kila kitu na kupewa misaada kutoka Arabia na nchi zingine! Wanapiga firimbi sanaaaa...Lakini hawajui matokeo yake kwa ujinga wao kama wakija kujitenga! Na ni bora wajitenge na wala sisi wa BARA hatuwataki pia,kwanza ni wavivu na wanatuletea ghasia tupu!ukiwauliza wewe ni mtanzania wanasema "HAPANA" Mie ni mzanzibari,Kwani hawajioni Rangi zao walivyochanganyika? Mababu na Mabibi zao walitokea bara na sehemu nyingine za Afrika walikuwa watumwa na waliolewa na waarabu na ndiyo maana wengi wao wapo mchanganyiko! Sasa wanajivunia nini? Elimu na Upeo wa maisha ni kitu kimoja muhimu sanaaaa...!Kaaeni mtafakari na mfikiri!
ReplyDeleteHuu muungano haukupatikana kwa upanga bali kwa mazungumzo,hivyo kama kunakwisha bali pia itakuwa kwa mazungumzo si kwa upanga.
ReplyDeleteHao wanaotaka mkato wanachokitu kingine wanachokitafuta kwa kupitia kusingizia kutotaka muungano.La sivo suala la dini na muungano linaingiaje hapa.
Kunawatu wanaunda vikundi kutafuta umaarufu tu.Utachanganyaje dini na muungano.Huu ni uwendawazimu tu.Mara nyingi watu wasojua dini/siasa vema ndo wanaleta vurugu na kuwakoroga wananchi.Wenye kujua hivo vitu hawana jazba wala hawaongea kwa kukoroma.
Kama kuna suala la muungano kuendelea au kutoendelea vitu hivi vinazungumzika.Ugomvi unatoka wapi?Wanaohusika wakae na wazungumze.Kwa nini watu wafe kwa ajili hiyo.Au kunawatu wnadhani wanaijua haki zaidi kuliko wengine!
Mwenyekujua ni mtaratibu,mstaarabu,anajua kushawishi bali asojua kitu anataka mkato,mabavu,hutumia upanga na maneno makali katika mazungumzo yake.
Dunia hii yote sasa maisha ni magumu sana.Shida zisitufanye tuanze kubaguana.Hata tukibaguana si kweli kuwa matatizo yetu yataisha au kuwa ndo tutapata pakubwa sana lahasha.Pengine ndo tutakwenda kwenye matatizo makubwa mno na tutaanza kujuta mara.
Roho za kibinafsi kamwe hazijengi wala hazileti heri asirani.Ni majuto tu.
Haya mazungumzo yangu hayalazimishi muungano ubaki,bali zaidi kutoa tahadhari kwa haya tunayoyafanya kuleta madhara baadaye,halafu na chuki mbaya zaidi baadye baina yetu.Iko njia ya kutafuta haki au ya kueneza dini si kwa mabavu au upanga.
Tafakari kwa makini kitu mnachokitafuta kama kweli ni lazima kifanywe kwa njia hiyo mnayoichukua.Msichanganye watu tu kwa ubinafsi wenu na kuchanganyikiwa kwenu.Msihukumu watu wengine kwa kutumia imani zetu.
Kuna nchi nyingi sana zimevunja muungano bila ugomvi wala matusi na mapanga.Kaaeni chini mambo yazungumzwe.Pengine nguvu ndo haitafanikiwa kabisa.Ni mazungumzo tu.
Watu wanathubutu kujilinganisha na Misri,Tunisia,Sudan,huko ni kuiga na kufuata mikumbo na kutumia mifano isiyofanana.Wazimu tu.
Ninyi mlionitukana na kunishambulia mimi mwanasheria wa kujitegemea, mtayakumbuka maneno yangu, endeleeni tu kuyatamani yale yaliyo tokea Tunisia,Misri na kwingineko, ninachoomba tu sadaka ile uitoe wewe uliye nishambulia yaani, kufa wewe na watoto wako, halafu watakao baki wafaidi hizo juhudi zako, maana tunawajua ninyi waisilamu wakujilipua, badala ya kusomesha watoto waende ughaibuni wakutumie Dollar we kaa hapohapo tegemea kuandamana ili ufe badala ya kuishi.
ReplyDeleteKama wewe unaakili, umechoma kanisa limekosa nini, kwani Kikwete ni askofu wa huko katika hilo kanisa, wewe na mimi nani mpumbavu zaidi,Wenzenu Misri au Tunisia walikuwa hawachanganyi mambo, walikuwa wanasema moja kwa moja tunataka uchumi mzuri, Siyo kama ninyi na umasikini wenu mara Muungano, mara Uisilamu ,Mara kanisa, Tuwaeleweje? hebu semeni kwanza kama kweli mna akili Timamu?
Nimeona nazungumza na watu ambao hawajaenda shule, naishia hapo, maana ukimkimbiza kichaa eti kachukua nguo zako wakati unaoga watu watasema wewe unayekimbia uchi ndo kichaa.
Abdallah Juma-Ughaibuni.
KAANE HIVYO HIVYO KUFIKIRIA WAZIMU MTUPU LAKIN KUNA SIKU NCHI YETU TUTAIPATA KAMA MNAONA KUCHANGANYA DINI NA SIASA SI SAWA NENDENI KAMULIZENI BABA YENU WA KANISA(NYERERE) AU MAASKOFU WENU KILA LEO WAO WANACHANGANYA DINI NA SIASA.
ReplyDeleteUNAFIKIRI WATU BADO VIPOFU WAMELALA AU WAMESINZIA, TUMESHAAMKA TOKA ZAMANI NA TUKO IMARAA
SOMA HISTORIA WEWE USILETA PUMBA HAPA NA KUCHAFUA HALI YA HEWA, HUIJUI HISTORIA YAKO YA BARA SEMBUSE UTAKE KURUKIA YA ZANZIBAR
TUTAIPATA NCHI YETU ONE DAY MKITAKA MSITAKE ONE DAY YEST TUTAJITAWALA WENYEWE.
NYERERE ALIKUWA ANAHOFIA SANA DINI YA KIISLAMU ITATAWALA VIZIWANI HAPA PEMBA NA ZANZIBAR NDO MAANA AKATAKA TUUNGANE KAMA SI UDINI NINI NA UFISADI VISIWA HIVI VILIKUWA VINA MUUMIZA KICHWA SANA NYERERE ALISHAWAHI KUSEMA ANGEKUWA NA UWEZO ANGEVISOGEZA MBALI KATIKA BARA LA HINDI ASK YOUR SELF WHY?
HALAFU HAPA MNATULETEA ASIJUI ZANZIBAR NI KA PLOT TU, AA SIJUI WAMERENGE WAZEMBE HAWAWEZIFUFANYA KAZI AAAH SIJUI MAHANISI,
WELL TUNATAKA NCHI YETU NA MTATUONA NA NYINYI NENDENI KWA WAZUNGU NA VATIKAN IENDELE KUKUSAIDIYENI NA SISI NDIO TUTASAIDIWA NA WAISLAMU WENZETU
baba yenu wa kanisa (nyerere) kaiga mifumo mingi tu ya nchi za jirani na nje kutawala wadanganyika kama nyinyi so whats the big deal tukitoa mifano ya misri, tunisia na sudani ya kusini, unakuwa kama hujasoma mkuu,au labda hujasoma because ungesoma ungejua kuiga kupo hata kukikaa pale mlimani unandika paper yako ya ku pressent in class unatoa mifanyo ya nchi.
ReplyDeletebwana eeh hapa hakuna kitu tunataka nchi yetu thats it kulumbana hakuna kitu na wakuu na maaskofu wameshajua sasa tumeshaanka wanatafuta mkakati wa kutuzibiti lakin Allah atasimama na sisi daima he will never let us down amin.