Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais,Bw. Richard Muyungi ambaye amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa kamati ya dunia ya sayansi mabadiliko ya tabia nchi, huko Durban africa ya kusini na kuanza kazi rasmi katika mutano unaendelea hapa ujerumani.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais,Bw. Richad Muyungi akiwa katika Ofisi yake mjini Bonn Ujerumani akiiwakilisha Tanzania kama Mwenyekiti wa Kamati ya Dunia ya Sayansi na Taaluma ya Mabadiliko ya Tabia nchi, kazi hiyo ameianza rasmi katika mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi unaoendela hapa Bonn Ujerumani
Tanzania kwa mara ya kwanza imepata nafasi kwa miaka miwili ijayo ya kuongoza Kamati ya umoja wa mataifa ya sayansi na taaluma ya mabadiliko ya tabia nchi, chini ya mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabia Nchi. Kamati imeanza kazi rasmi jana wiki hii, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 36 wa mabadiliko ya tabia nchi. Hayo yameelezwa leo katika mahujiano maalum na ofisa Mkuu wa programu ya Uendeshaji ya Sekretarieti ya Mkataba huu Bi Hanna Hoffmann, hapa Bonn, Ujerumani.
Bi Hanna Ameeleza kuwa Bw. Richard Muyungi ambae ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya mazingira kutoka katika ofisi ya Makamu wa Rais amepewa dhamana hiyo na nchi zote duniani wanachama wa mkataba huu kutokana na uzoefu wake mkubwa katika diplomasia ya mabadiliko ya tabianchi na upeo wa kutosha juu ya taaluma nzima ya sayansi ya mabadiliko ya tabianchi.
“Bw. Muyungi ni mwana diplomasia aliyebobea katika masuala ya mabadiliko ya tabianchi, ana elimu ya kutosha katika eneo hili na ni mzoefu sana na amekuwa akihudhuria na kuongoza mkutano mingi ya mabadiliko ya tabianchi hasa zaidi akiongoza kundi la nchi zinazoendelea, hivyo naamini kabisa, uteuzi wake ni muafaka na ataongoza vizuri kamati hii na masuala yote muhimu kama ulivyoona mwenyewe alivyoongoza leo mkutano kuhusu kilimo na mabadiliko ya tabianchi .” Alisisitiza.
Bi Hanna aliongeza kuwa Kundi la nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania ina nafasi kubwa zaidi ya kujifunza na kutumia njia za kuhimili na kukabilina na mabadiliko ya tabia nchi zaidi kutokana na nafasi yake ya uwenyekiti wa Kamati hii.
Kwa Upande wake Bw. Richard Muyungi ameeleza kuwa uteuzi huu uliofanyika rasmi Desemba mwaka jana na nchi zote wanachama huko Durban Afrika ya kusini, na kuanza rasmi leo, ni heshima kwa nchi na nafasi ya pekee kwa Tanzania kuweza kujifunza mengi na kupata fursa mbali mbali za kuweza kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi zinazoikabili Tanzania ikiwemo uhaba wa mvua, mafuriko, kuongezeka kwa kina cha bahari na, mvua zisizotarajiwa, na baadhi ya maeneo ya nchi kuelekea kuwa janga kutokana na mabadiliko haya.
Mkutano huu unaoendelea hapa mjini Bonn Ujerumani, ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa Dunia wa mabadiliko ya tabia nchi, ambao utawakutanisha wakuu wa nchi duniani utakaofanyika mjini Doha,Qatar, Novemba mwaka huu. Aidha utatoa mchango katika mkutano wa wakuu wa nchi kuhusu Maendeleo endelevu (Rio+20) utakaofanyika huko Rio, nchini Brazil baadaye mwezi Juni.
Pamoja na masuala ya Kilimo na mabadiliko ya tabianchi, Kamati hii pia inatafuta muafaka kuhusu suala la matumizi ya sekta ya misitu katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kuzingatia maslahi ya nchi zenye misitu inayonyonya gesi hizi, na taratibu za kusimamia na kutekeleza miradi ya kupunguza hewa ukaa katika nchi zinazoendelea bila kuathiri maendeleo ya nchi hizi.
Aidha katika mkutano huu, Masuala ya upatikanaji wa fedha ili kukabiliana na mabadilkio ya tabianchi kwa nchi maskini duniani na suala la nchi zilizoendelea kuongeza juhudi za kupunguza gesijoto zinazosababisha mabadiliko ya tabianchi yamepewa kipaumbele.
Mkuu Muyungi, Hongera sana sana, wewe pamoja na msafara wako ni wawakilishi safi sana wa nchi yetu, ninawatakieni kila la kheri katika mapambano hayo ya kupunguza athari za Climate Change.
ReplyDeleteMdau
You are a good man Richard, and a very good boss and committed worker. You really deserve the roses pouring onto your life. May God continue to bless you. Amen.
ReplyDeleteCongratulation and Best Wishes to Richard Muyungi and Tanzania Team on this new global assignment. With imminent impacts of climate change such as the shrinking of Mt. Kilimanjaro ice cap hence effect on tourism industry, flooding + destruction of infrastructure, raising of sea level thus damage on beach housing and habitats, draught / agricultura pests = hunger/food shorage, the challenge is big.
ReplyDeleteRichard Mazingira
Tanzania and the whole africa its our time to show this planet we can make it a better place for living. Congratulation and best wishes to Mr Richard Muyungi and Tanzania team.
ReplyDeleteardhi university
congratulation mhushimiwa Muyungi. hopely you could represent well our national issue and showing emphasis concern climatic changes in finding better solution,from my suggestion more mass education supposed to be provided in so far making people aware on measure taking. may God bless, "its only environment problems needs environmental solution, and your the one".
ReplyDelete