Wazalendo
Kwa niaba ya Mtandao wa wanataaluma Tanzania (Tanzania Professionals Network- TPN) nawatangazia kuwa tunakusudia kuandaa kongamano kubwa la kitaifa la kujadili masuala ya kiuchumi (National Economic Forum).
Tunatarajia kongamano hili litafayika muda mfupi ujao ili watakaopata nafasi ya kuhudhuria basi watoe maoni ambayo yatatumika ili kuwasaidia wafanya maamuzi na watunga sera katika kuboresha bajeti na sera zetu na mipango yetu ya kuichumi ikiwa ni pamoja na ya sasa na bajeti za baadae ili kusaidia maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa Taifa letu la Tanzania.
Wote tunajua kuwa nchi yetu ina rasilimali nyingi kuliko nchi zote ukanda huu, wote tunajua kuwa nchi yetu imezungukwa na nchi nyingi ambazo uchumi wa nchi hizo unategemea miundombinu ya nchi yetu, wote tunajua ya kuwa nchi yetu ina utulivu na amani kuliko nchi zote za ukanda wetu , wote tunafahamu kuwa kuna sera na mipango mingi ya kitaifa ambayo imepitishwa na inafanyiwa kazi, Sasa swali la kujiuliza ni kwa nini hadi sasa bado tuko nyuma sana ? … na ni kwa nini nchi yetu ni moja ya mataifa masikini sana duniani ? nini kifanyike ili kututoa katika hali hii ?
basi tunaomba watazania wote wenye mawazo, mbinu na ujuzi washirikiane nasi katika kutafuta majibu ya maswali haya .
basi tunaomba watazania wote wenye mawazo, mbinu na ujuzi washirikiane nasi katika kutafuta majibu ya maswali haya .
Washiriki wa kongamano hili ni watanzania na wasio watanzania ili mradi ni wazalendo wenye mawazo ya kusaidia kutoa majibu ya maswali hayo, tunatarajia kwaalika Mawaziri, Wabunge, watunga erra kutoka taasisi muhimu, Wataalumu wa Fedha, Uchumi , uwekezaji na biashara na wakuu wa taasisi muhimu zinazohusika na uchumi, fedha na bisahara.
Siku ya Kongamano na ukumbi mtajulishwa baada ya maandalizi ya awali kukamilika, ila litafanyika katika jiji la Dar Es Salaam wiki ya kwanza ya mwezi juni.
Wale wote watakaopenda kutoa mada(Speakers) au kuwa wachangiaji wa mada (Panelists) wawasiliane nasi mapema iwezekanavyo kabla ya ijumaa ijayo tarehe 25/05/2012
Wale wote watakaopenda kudhamini kongamano hili tunaomba muwasiliane nami, Makamu wa Rais- Richard Kasesela (rkasesela@gmail.com ) au katibu Mkuu Mhe. Janet Mbene (maorchid@gmail.com).
Jioni ya kongamano hili ambalo litakuwa ni la siku moja tu kutakuwa na tafrija ndogo kwa washiriki wote (Cocktail) ya kuwapongeza na kuwashauri baadhi ya wanataaluma walioteliwa kushika nyadhifa mbalimbali katika nchi yetu.
Naomba mjitokeze kwa wingi kushiriki na kusaidia kufanikisha kongamano hili.
Nawatakia wote kila la heri na naomba tushikirikane.
Phares Magesa
Rais–TPN
+255 (0784/0767/013) 618320
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...