Basi lililowabeba Twiga Stars likiwasili "Dodoma Hotel"
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akimkaribisha Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars),Bonifasi Mkwasa wakati walipowasili kwenye Hoteli ya Dodoma.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Betty Mkwasa akimkaribisha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars),Charles Bonifasi Mkwasa "Master" ambaye ni Mume wake.
Wachezaji wakivalishwa skafu
Timu ya Taifa ya wanawake ya mpira wa miguu Twiga Stars jana iliwasili Mkoani Dodoma kwa ziara ya siku Mbili ikiwa na msafara uliojumuisha wachezaji nyota 23 na viongozi watano (5).
Ziara ya Twiga Stars imekuja kufuatia mualiko wa chama cha soka Mkoani Dodoma DOREFA ambapo ikiwa Dodoma Twiga Stars itatembelea shule mbalimbali kutoa hamasa kwa wasichana kujiunga na michezo na kuona vivutio mbalimbali Mkoani Dodoma na kucheza mechi ya kirafiki na Timu ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Dodoma (copa coca cola).
Twiga Stars iliwasili Mjini Dodoma majira ya saa nane mchana alasiri na kulakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Betty Mkwasa na Uongozi wa Dorefa.
Msafara wa Twiga Stars uliongozwa na askari wa Jeshi la Polisi, msululu wa waendesha pikipiki almaarufu kama Bodaboda na magari mengi. Aidha makundi mbalimbali ya watu kama wanafunzi walijitokeza kwa wingi, baadae Twiga Stars ilikwenda “Dodoma Hotel” kwa mapumziko.
Akitoa salamu zake kwa wachezaji na Viongozi wa Twiga, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi aliwapongeza Twiga kwa kuitangaza vizuri Tanzania Kimataifa, pia amewataka watoe hamasa zaidi kwa wasichana ili wajiunge na michezo kwani pamoja na kuwa sehemu ya burudani lakini inatoa ajira.
Aidha amewataka Kocha na Viongozi wa Twiga kusaka wachezaji wenye vipaji kutoka Mikoa mbalimbali ya Tanzania ili wajiunge na Twiga badala ya kujikita zaidi Dar es Salaam.
Kufuatia kauli hiyo kocha wa Twiga Charles Bonifasi Mkwasa “Master” alishauri vyama vya soka vya Mikoa kuandaa timu na mashindano ya wanawake ili aweze kuchagua vipaji kutoka Mikoa hiyo.
Nae Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Betty Mkwasa alieleza kuwa kwa kuzingatia kuwa asilimia kubwa ya uongozi wa juu wa Mkoa wa Dodoma unashikiliwa na wanawake basi maazimio ni kuona mwamko wa Wasichana kwenye michezo unapanda.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...