IDADI ya abiria wa Shirika la ndege la Air Tanzania (ATCL) imezidi kuongezeka kila kukicha kutokana na wananchi kuonyesha uzalendo na imani kwa kampuni hiyo , Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL Paul Chizi amesema.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari jana Chizi alisema kutokana na imani hiyo, kampuni yake imejizatiti kuleta mabadiriko makubwa katika sekta ya usafiri wa anga kupitia mpango  wa maendeleo wa miaka mitano wa shirika hilo.

Chizi alisema tangu uzinduzi wa safari za Dar es Salaam-Kilimanjaro-Mwanza wiki moja iliyopita kwa kutumia ndege ya aina ya Boeing 737-500,kampuni yake imekuwa ikijaza abiria takribani 106 katika kila safari kwa siku tatu mfulilizo ikiwemo na siku ya jana hali ambayo inaashiria kuwa wananchi wameanza kuwa na imani na huduma zinazotolewa na shirika lake.

 “Ndege yetu kwa takribani siku tatu zilizopita imekuwa ikija katika safari zote za Dar es Salaam-Kilimanjaro-Mwanza . Sikujua kuwa tutakuwa na uwezo wa kurejea na kupata mapokezi ya namna hii kwa haraka kutokana na kuwa kuna watoa huduma wengine katika njia hii . “Baada ya wananchi kuonyesha imani na uzalendo,tutaendelea na kuongeza nguvu zetu katika kutoa huduma zetu kwa wakati na kwa bei nafuu. Nawaomba wananchi kuendelea na uzalendo wanaouonyesha kwa faida ya kampuni yetu na nchi nzima kwa ujumla,” alisema.

Chizi alisema kuwa mipango ya kampuni hiyo ya kupata ndege nyingine ambayo itatumika katika safari za kimataifa katika miezi mitatu mpaka sita ijayo inaenda vizuri na kuongeza kuwa kampuni itatoa taarifa kamili wakati muafaka utakapofika. “Kutokana ukweli kuwa tunatarajia kuanza safari za kimataifa, ni dhahiri kuwa ndege ambayo  tunategemea kuleta lazima iwe kubwa,” aliongeza.

Alisema kuwa kampuni yake kwa sasa imejikita katika utekelezaji wa mpango wake wa maendeleo wa miaka mitano utakaosaidia kuongeza ubora katika kampuni hiyo na kuboresha utoaji huduma kwa ujumla.“Tutajikita katika kuongeza ubora wa huduma tunazozitoa na vilevile kuchukua nafasi ile tuliyoipoteza hapo nyuma. Tunamatarajio ya kupata ndege nyingine ya Boeing na mazungumzo yameshaanza na tumefikia pazuri,” alisema.

Kurudi kwa huduma za ndege ya ATCL kumeanzisha  vita ya viwango vya bei za usafiri wa anga bada ya ATCL kutoza bei ya shilingi 199,00 kwa safari zake kwenda na kurudi (return ticket) na kusababisha watoa huduma wengine wakiwemo Precision Air nao kupunguza gharama zao ile ilikukabiriana na ATCL. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 27, 2012

    Go go go ATCL the wings of Kilimajaro,yeahlazima tupende shirika letu la ndege.ndiyo nembo yetu hiyo.Bwana Chizi,tatizo siyo kwamba ATCL hamjui biashara ya ndege..mko juu sana isipokuwa tuvitendea kazi(ndege) ndiyo tatizo.Hizo safari za kimataifa ATC enzi zile imeruka.Mafisadi ndiyo wametuvuruga sana hapa katikati.Mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 27, 2012

    Serikali inabidi ifikie wakati na kukubali kuwa ujamaa umeshindakana. Serikali inabidi ijitoe kwenye masuala ya biashara na kuiachia sekta binafsi kufanya haya mambo.

    I wonder why they don't sell ATCL to Precision Air. Mashirika yote yalikuwa ya serikali yamekufa. Bado tu tunabisha?

    Long Live Free Market Cpitalism!

    ReplyDelete
  3. Mungu ibariki ATCL, Mungu ibariki Tanzania yetu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 27, 2012

    kujaza abiria siyo hoja bari kufanya kazi kwa juhudi na maarifa siyo polojo poloj tu mashirika yanayo fanya kazi kwa bidii na maarifa tunayaona wala hayafilisiki

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 28, 2012

    Ujamaa ni mfumo usioleta faida, kwa sababu ujamaa ni adui wa ujasiriamali. Wajasiriamali wanazingatia kanuni za uwekezaji(kibiashara) zinazoleta tija.

    Tunawaomba chadema wakitaka tuwape kura wasiturudishe nyuma kwa kuturudishia ujamaa. Ujamaa ni mfumo wa wafanyakazi na wakulima pekee yake.

    Ujamaa unachukia utajiri na unachukia matajiri.

    Ujasiriamali ni mfumo wa kutajirisha watu kwa kufundisha misingi ya ukweli ya kupata faida katika investments.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 28, 2012

    ATCL mko juuu ila ndege moja tu haitoshi ongeza zingine kana tisa (9)ziwe kuni ndio tuanze uzalendo maana kudumisha kamapuni kwanza hii ndio msingi wa maendeleo hata nauli zikishushwa haitakuwa tatizo maana zile za kutoka nje zitafidia zile za ndani. Hivi hawa jamaa wa precision wana namaba kubwa ya ndege za nadani na nje je mtaweza kushindana nao? manaa kwa mtazamo wangu mkichukua za mrahaba kutoka mkoa wa shinyanga tu ndege za kumwaga ni kipau mbele tu WATANZANIA TUNAWEZA MNOOOOOO.! BIG UP ATCL

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 28, 2012

    yaani wewe taahira kweli. Tuuze shirika kwa Masonic company. Give me a break tutakufa kiofficer.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 28, 2012

    Tatizo ni dogo tu na liko katika mashirika yote ya umma.Serikali iache kuingilia utendaji wa mashirika haya.Hilo la kuuza ATCL kwa nani sijui halikubariki kwani mmoja wa wamiliki wa hilo shirika alikuwa waziri mwenye dhamana ya kusimamia ATCL.Na inawezekana kabisa alifanya maamuzi ya kuua shirika kwa makusudi ili lile lake binafsi lishamiri

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 28, 2012

    Shirika letu tunalipenda ila ubabaishaji, wizi, rushwa na ubadhirifu wa fedha za umma viezidi kwa viongozi na hata waajiriwa wa chini. Mkiacha ubabaishaji mbona shirika litakua sasa hivi na kuongeza ndege zingine? Huo ni ukweli usiofichika.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 28, 2012

    Wanaosema ATCL iuzwe ni watu wasio na fikra,mbona kampuni kubwa kama british airways, KLM, Emirates zinamilikiwa na serikali za hizo nchi?...swala ni kuuza shares, ila serikali ibaki na shares kubwa zaidi ili iweze kuwa na maamuzi na hilo shirika, a developed country must have a national flag carrier..period!.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...