Baadhi ya Wanachama na Wakereketwa wa Timu ya Yanga ya Jijini Dar,wakiongea na Waandishi wa habari waliofika kwenye Makao Makuu ya Klabu ya Timu hiyo,Mtaa wa Twiga na Jangwani leo.Wapenzi hao wa Timu hiyo ya Soka walifika Klabuni hapo wakidai kuwa wanataka Mwenyekiti wa Yanga,Lyod Nchunga aachie ngazi kwani hana Maslahi na timu hiyo,huku wengine wakikataa kuachia ngazi kwa kiongozi huyo.hali iliyopelekea mpaka askari wa Jeshi la Polisi kufika Klabuni hapo kwa kuhakikisha usalama unapatikana na hakuna madhara yeyote yatakayotokea.
 Kila Mwanayanga aliefika klabuni hapo alikuwa na jazba na uongozi wa juu.huyu nae alikuwa akimlalamikia Nchunga kuwa ndie aliesababisha timu yao kupata kichapo cha bao 5-0 dhidi ya watani wao Simba.
 Afande akiwaamuru wanayanga hao kuondoka klabuni hapo,lakini walikuwa wakiikaidi amri hiyo.
Mwenyekiti wa umoja wa Vijana wa Klabu ya Yanga, Bakili Makele akiongea na waandishi wa habari.
Bibi huyu alietambulika kwa jina la Bi. Mariam nae ni mkereketwa kweli kweli wa Yanga,nae alikuwa akisema kuwa anamuomba Lyoid Nchunga aachie ngazi kwani anawaharibia timu yao.


BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 11, 2012

    Looooooh!!!! Kufungwa kubayaaa!

    mnataka kuuana kwa sababu ya kufungwa tu.Arsenal ilifungwa 8,Man U ilifungwa 6,chelse juzi imefungwa 4.Nenda hata Spain hivyo hivyo.

    Sasa ninyi nani msifungwe 5?Hadi mnataka kufukuza viongozi.Kwani mara yenu ya kwanza kufungwa mengi!! Acha hiyo.Mimi nilidhani mtakaa chini muimarishe timu au sehemu zenye kasoro.

    Hata mkimleta nani mtafungwa tu kama mambo ni hayo.Na mkifungwa baada ya kubadili uongozi mtasema nini.Ondoeni kocha siyo mwenyekiti ndivyo wenzenu wanafanya.Hata hao wenzenu hawaondoi kocha kwa kufungwa mara moja.

    Poleni sana,malizeni matanga basi muanze mazoezi.Kwa sasa Simba hamuiwezi pamaoja na mhe RAIS yuko upande wenu.Sisi Mhe Sarungi,Kapuya watosha tu.

    Tutawaazimeni kocha wetu halafu mkiifunga Simba tu mrudisheni.Au Ankal unasemaje?

    Waacheni viongozi wafanye kazi.Mnaposhinda mbona hamsemi kitu na mnawabeba.Mwadhani kila siku mtashinda tu.Kwani wengine kwenye ligi wamekuja kufanya nini mshinde nyie tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...