Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Rais wa Kampuni ya Mafuta ya STATOIL na ujumbe wake, ofisini kwake jijini Dar es salaam leo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mwenyekiti wa Tume ya Kamati ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba na wajumbe wa Tume hiyo baada ya kutembelea Ofisi za Tume jijini Dar es salaam leo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe baada ya kutembelea Ofisi za Tume ya Kamati ya Mabadiliko ya Katiba na kuzungumza na wajumbe wake, jijini Dar es salaam leo.Kulia ni Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Joseph Sinde Warioba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
hii tume mbona imejaa wastaafu,kutakuwa na mawazo mapya kweli?
ReplyDeleteKwa Tanzania kazi ipo.
ReplyDeleteKatiba inatakiwa iboreshwe kwa maoni ya wananchi.Inatakiwa itoe sheria msingi ya muundo wa kisiasa.
Kwa kuangalia haraka inaonyesha tayari tume ya katiba ina watu waina fulani,sidhani kama wanchi watashiriki kiukweli.
Tengeneza makundi yenye uwiano.
Mfano.
Waandishi wa habari wawe na wawakilishi wao.
Tayari kunawanasheria lakini Walemavu sidhani kama wana mwakilishi hapo ingawa tunaupungufu mkubwa sana kwenye haki za walemavu.
Watanzania waishio nje ya nchi?
Wanawake? wapo wachache ingawa tunaupungufu mkubwa kwenye ubora wa maisha ya mwanamke.
Tujuwe tunahitaji katiba itakayoenda na wakati(katiba iwe inaakisi msemo wa kweli wa ndani wa Mtanzania yeyote yule.
wakulima wadogowadogo sidhani kama wanamwakilishi hapo.
kwasababu wawakilishi wawe na uwezo wa kurudi kwa wananchi na kukusanya mawazo ya kweli kulingana na watu wenye uzoefu wa maisha ya Mtanzania vijijini na mjini ndani ya nchi na nje ya nchi.
Ok ,lakini inahitaji uwiano wa jinsia na uwezo.
Tume iliyoundwa inaonyesha ina hadhi ya kuboresha mawazo ya wananchi kabla ya Serikali kupitisha na si kukusanya mawazo.
Mkusanya mawazo anapaswa asitofautiane sana na mtoa mawazo.
Wewe ndio unatakiwa kutoa mawazo lakini usijipendelee ukasema unataka uwekewe ulinzi binafsi nyumbani kwako.
ReplyDeleteHukusikia CHADEMA wamesema kwamba imejaa waislam, sasa wewe wastaafu hivi mstaafu ni nani, Mwanafalsafa mmoja amesema : 'You learn from experience but you also learn from experience of the others' wastaafu ndio wenye data nyingi kutokana na experience za maisha. Wewe au mwalimu anaeanza kazi leo vyuo vikuu atajifananisha na Prof. Baregu. Huko nje mstaafu anaheshimika sana. Hebu wacheni ujinga jamani mnaharibu hii blog, hatuelimika kwa kusoma mawazo ya watu wasiokuwa na busara.
ReplyDelete