Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar

Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Said Ali Mbarouk amesema licha ya fujo ambazo zilitokea May 26 na 27 Usalama umeimarishwa vya kutosha na kuwataka Watalii waendelee kuja kufanya shuguli zao bila ya woga wowote.

Amesema Serikali inabeba jukumu la usalama wa Wageni ambao wanakuja Zanzibar na kufahamisha kuwa fujo lililotokea halikuathiri Sekta ya Utalii na maeneo yake muhimu.

Waziri Mbarouk ameyaeleza hayo alipokuwa akizungumza na Wawakilishi wa Mabalozi waliopo Nchini kuhusiana na fujo lililotokea jana na juzi kufuatia kukamatwa kwa kiongozi mmoja wa Jumuiya ya Kidini ya UAMSHO.

Amefahamisha kuwa maeneo muhimu ya Utalii yakiwemo Mji Mkongwe,Fukwe za bahari na Hoteli ni sehemu salama ambazo watu wanajishughulisha na kazi zao za kawaida na kuwaomba Mabalozi hao kuwafahamisha vyema wenzao kile ambacho kimetokea.

Amesema Jumatatu ya leo Afisi za Serikali na zile za binafsi ziliweza kufanya kazi ambapo kwa upande wa wananchi wa kawaida nao waliweza kuendeleza harakati zao za kila siku kutokana na hali kuwa salama.

Mbarouk ameeleza kuwa Jeshi la Polisi kwa ufanisi mkubwa liliweza kutuliza vyema fujo za waandamanaji bila ya kuwepo taarifa yoyote ya kifo au kujeruhiwa kwa mtu yeyote.

Waziri Mbaruk amesema kilichotokea ni watu kutumuia uhuru wao wa kidemokrasia wa kuelezea hisia zao ambazo baadae ziliashiria vitendo vya vurugu jambo ambalo liliwasababisha Polisi kuchukua hatua za kutuliza vurugu hizo.

Mbarouk amesema Serikali imejipanga vyema kuhakikisha inaendelea kuilinda haki ya kidemokrasia bila ya kutokea vitendo vyoyote vinavyoashiria kuhatarisha amani Nchini.

Amesema Taarifa ya Serikali imetolewa Jana na Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohammed Aboud ambayo iliagiza vikosi vyote vya ulinzi kuwa macho kwa lengo la kutuliza usalama sambamba na kuwakamata wale wote waliohusika na fujo hizo.

Kwa upande wao Wawakilishi wa Mabalozi hao walimweleza Waziri huyo kuhakikisha amani inarudi kama kawaida ili watu waweze kuishi bila ya hofu Mkutano huo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 28, 2012

    UMASHO:

    Sawa Kiongozi, isipokuwa Bara tunauthamini Muungano na tunataka Ustaarabu zaidi kuliko mabavu na fujo,

    Ni muhimu umwaeleze kundi lenye jina hilo hapo juu ya kuwa Muungano ulipatikana kwa njia ya mezani na hivyo kama ni kuvunjika uvunjike kwa njia ya mezani.

    Waleleze wadai hoja zao kwa utaratibu na ustaarabu zaidi kama Waumini safi.

    Kama wataleta ujinga kuhatarisha amani nchini tutawapandisha Boti kuja kuwafungia Magereza ya Bara ya LUPANGO (kUJISAIDIA KWA MTONDOO-ndani ya debe au ndoo) kwa vile huko kwenu vifungo ni rahisi na Hakuna Lupango kuna Vyuo vya Mafunzo!

    Waeleze pia ya kuwa Uislamu hata Bara tunaujua na kuwa ni JAZBA sio sehemu ya Itikadi ya Dini yetu Tukufu!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 29, 2012

    maneno yako ni murwa kabisa sina hata cha kuongeza

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 29, 2012

    wewe mdau hapo juu usijifanye mbabe sana au wewe ndo nguvu ya dola nani kakwambia mungano umepatika kwa njia ya mezani, nani? kwanza tumemwaga damu yetu halauf huyo baba yenu akaja kuturubuni wacha hizo na subutu mtuchukuwe huko kwenu unajeza nini na vya moto basi jaribuni

    hatutaki muungano na nyinyi watu wa mrima na kwa maandishi yako wewe si muuslamu hata kidogo jazba baba yenu wa taifa ndo alianzisha yeye alivyopata uhuru na kuwatia watu ndani walio mfadhili na kumstiri mpaka kafika kuwa rais.

    soma historia wewe usituletee pumba hapa tunataka nchi yetu na hatulali wala kusinzia mpaka tuipate nchi yetu NO MORE MUUNGANO wa kukabwa koo

    na msiusamini muungano kwa nini watu wa bara kwa vile mnanufaika nao kuliko watu wa zanzibar so peleka pumba zako mbele kwa mbele wewe.

    na michuzi usipendele kubania hii comment yangu yake umeiweka na yangu yote iweke bila ku edit thank you mheshimiwa

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 29, 2012

    Wewe Bwege mtoa Maoni wa pili hapo juu Anonymous wa Tue May 29, 01:00:00 PM 2012

    'NO MORE MUUNGANO'

    Kigezo cha kuwa Muislamu safi sio kuunga mkono ujinga kama uliofanywa na Waislamu wenzetu UAMSHO Zanzibar.

    Ndio ninyi 'Mabwege' mnaofikiri harakati za Kidini na Uumini safi ni kufanya mauaji kama Al Shaabab na Al Qaida, kitu ambacho sio kweli!!!.

    Wewe Mdau kama ni Muislamu safi, nipe Aya au Hadithi inayosisitiza kuwa UISLAMU ni MAUAJI au FUJO na VURUGU ?

    KWA KUWA MUNGU ANATUSISITIZA KUOMBA VITU KWA HEKIMA BUSARA NA UTARATIBU NDIO MAANA HATA KTK SERIKALI WOTE WALIOFANYA UJINGA WAO WATU WA KUNDI LA UAMSHO WATAFIKISHWA MBELE YA SHERIA ZA KIDUNIA ZA MAHAKAMA ZA SERIKALI KABLA YA KUKABILIANA NA MAHAKAMA NA SHERIA YA MWENYEZI MUNGU HAPO BAADAE!,,,,UPO HAPO wewe Bwege 'NO MORE MUUNGANO ?

    Hata kama baba yetu wa mrima ndio alileta Muungano na ninyi mkaghiribiwa, kama Waislamu mnatakiwa muukatae Muungano kwa hoja na njia ya busara.

    NINYI MNADAI NCHI YENU AU MNADADAI WILAYA ZENU MBILI (2) PEMBA NA UNGUJA?

    KAMA NI HIVYO ITAKUWA KAZI MAANA KILA WILAYA YA BARA PIA ITATAKA IJITENGE!!!

    Haiwezekenai mpate kwa kuwa wengi zikipigwa kura za Maoni mnaokataa Muungano mtazidiwa na wanaotaka Muungano ,mfano mpo 1,000,000 watakaotaka muungano watakuwa zaidi ya 500,000 kwa hivyo haiwezekani kuwaridhisha watu chini ya LAKI TANO !!!!

    Mbona Maalim Seif Sharrif Hamad mpinga Muungano mwenzenu wa zamani hamumlaumu kwa kuchelewesha kuvunja Muungano?

    KWA HIVYO KWA MANENO HAYO JUU NI KUWA MUUNGANO NI NDOA YA KUDUMU, KAMA HAMTAKI MPANDE MAJAHAZI MWENDE KWENU OMANI!!!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 29, 2012

    Wazanzibari wanaofaa ni wale wa MAPINDUZI DAIMA!

    Kwa kuwa inaonekana wasiotaka Muungano ni WALEWALE WALIOPINDULIWA MWAKA 1964 NI WAARABU ambao hawana nchi hapa Afrika!!!

    WAARABU WAELEWE KUWA ZANZIBAR NI SEHEMU YA TABORA HAWANA NCHI HAPA, WANATAKIWA WAENDELEE KUPAMBANA NA 'ARAB SPRING' PAMOJA NA 'MTIKISIKO WA KIFEDHA NA KIUCHUMI' KWAO HUKO.

    KWA HIYO HAWA WALIOPINDULIWA WASIOTAKA MUUNGANO WAENDE KWAO ARABUNI!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 29, 2012

    Hahahaa!. Eti wametumia Uhuru wao wa kidemokrasia wa kuelezea hisia zao ambazo baadae viliashiria vitendo vya vurugu jambo ambalo liliwasababisha Polisi kuchukua hatua za kutuliza vurugu hizo.

    Sasa, ikiwa walitumia uhuru wao wa kujieleza ni kwanini muliwakamata watu na kuwapandisha mahakamani kwa koso la kuandamana na kupinga muungano.

    Vyanzo vingi vinatwambia watu waliandamana kwa amani mwanzo mpaka mwisho, ila ni baada ya polisi kumkamata kiongozi wa Jumuiya ndio hapo vurugu zilianza. jee nani ni mvunjifu wa amani hiyo iliyopo.

    Nawe mdau wa mwanzo kama unadhani kuwekwa chuo cha mafuzo maana yake ni rahisi njoo ujaribu nawe upate huo urahisi unaofikiria. Pia na wewe hufai kwani unachembe za udictator na uvunjifu wa sheria.

    Wazanzibari wanahaki ya kudai uhuru wao kikamilifu, na kudai haki zao za msingi. Hakuna uhuru wa Mezani hapa kwani wakilifanya hivyo tokea 1964, 1967. 1971, 1984 hadi leo hakuna jipya isipokuwa kuzidi kupuuzwa hadi Rais wa Jumbe kung'olewa madara yote na Nyerere mwaka huo 1984. Soma historia utapata ukweli na sio Udictotor wako huo.

    Pamoja na hayo T. bara (nchi ya kusadikika) ingaliheshimu mkataba wa muungano hayo yote yasingalitokea lakini sasa too late, Waz'bar wanataka taifa lao.

    Zanzibar itabaki kuwa ya Wazanzibari na Tanzania Bara nchi ya kusadikika itakuwa ya kwenu.

    Na Mdau- Huu si Muungano bali mbanano, ukorofi, kulazimishana na kupindishapindisha ukweli na makubaliano halisi.

    ReplyDelete
  7. wafungwa baraMay 29, 2012

    sisi wafungwa wa huku bara tunawasubiri hao wafungwa watarajiwa ZANZIBAR hakuna gereza wao wanasema chuo cha mafunzo,jamani tuleteeni hao ndugu zetu tuwafundishe muungano ulivyo,tunaamini wataelewa na watakuwa waalimu wazuri na kuwafundisha ndugu zao,chondechonde tuleeteeni jamani hao

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...