Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Severin Tossi(kushoto) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Njombe John Mahali .Mwenge wa Uhuru umepokelewa leo mkoani Ruvuma katika kijiji cha Ngelenge wilaya ya Ludewa kabla haujaanza mbio zake mkoani Ruvuma.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kapt.Honest E.Mwanossa akifungua jengo la hosteli ya wasichana katika shule ya sekondari ya Mbambabay wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2012 Kapt.Honest E.Mwanossa akimsaidia kubeba ndoo ya maji Bi .Hilda Ngoya mkazi wa kijiji cha Nkaya wilaya ya Nyasa mara baada ya kiongozi huyo kuzindua kisima cha maji kilichoghalimu Tsh 14.9 milioni.Mwenge wa Uhuru utakuwepo mkoani Ruvuma kwa siku sita.Picha na Muhidin Amri wa Globu Jamii,Ruvuma.

Kufungua jengo la hosteli ya wasichana mwaka 2012 kwa kumtwika msichana ndoo ya maji ni kuendelea kumdhalilisha mtoto wa kike na kurudisha nyuma maendeleo ya nchi! Wake up people!!
ReplyDeleteHii habari ya mwenge wa uhuru ni miongoni mwa vitu vilivyopitwa na wakati. Ni kuongeza tu matumizi ya serikali yasiyokuwa ya lazima. Badala ya kuzunguka nao kila mwaka pengine ungezuka tu mwaka wa uchaguzi na sensa kuhamasisha watu. Otherwise uwe kimya.
ReplyDeletehivi mwenge una faida gani,nimekuwa nikisikia bajei kubwa ya mwenge lakini sioni matunda yake,kwani usiwe unakimbizwa kila baada ya miaka kumi hiyo hela yake ikatumika kufanya vitu vingine vya msingi kama vile elimu-kufadhili wanachuo,afya -kujenga majengo na kutoa vifaa vya mahospitalini na kunusuru hawa wanaotuleta duniani wasilale chini kama nyoka.
ReplyDeleteulaji wa wajanja huooooooo
ReplyDelete